TP MAZEMBE ndiyo timu itakayoidhihirishia timu ya SIMBA kwamba haikustaili kabisa kufika hapo ilipofika.

Fact, fact fazu nyie mamikiya mmefunga goli ngapi ugenini?

Simba ina akili mingi sana

Imefungwa goli nyingi lakini imepita yenyewe,yaani kiufupi wanajua kugonga kwenyewe,wataalam wa mapenzi wanasema jamaa wanahit G spot,sio mchezo hata kidogo kuifikia hiyo kitu unahitaji utaalam,kutokukata tamaa na ubobezi,ndicho walichonacho Simba.
 


Huyu mchambuzi underdog anafahamika. Ameumbuka vibaya na hadhi yake inazidi kushuka siku baada ya siku.
Ni ujuaji wa roho mbaya ndio tatizo. Huwezi ukachambua mpira ukiwa umejaa chuki na visasi. Wajifunze kwa wachambuzi mahiri akina Mwalimu Kashasha, Ally Mayai, Edo Kumwembe, n.k
Eti ooh watu hawataki kuambiwa ukweli, ina maana huyu underdog anaifahamu Simba vizuri kuliko kocha wa timu?
 
Kama tulimtoa zamaleki bingwa mtetezi kipindi kile nothing is impossible cha msingi simba wajipange, halafu fahamu tp mazembe bingwa wake huko Congo ni ASvita ambaye tumekula kichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watakunywa sumu mwaka huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba wa nyika hawezi kutishwa na vikelele vya chura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dauda alikuja zaidi yako lakini amelala nyasi... Wewe tukuache uropoke kwa kuwa Yanga yako haimo na hauoni AIBU
 
Unakumbuka tu kwenye makundi ila umesahaua kua kwenye mtoano simba ndo timu iliyofunga magoli mengi Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa Yanga sijui wakoje tu... kuna kipindi wanashangilia kupata droo dhidi ya SIMBA.
Na siku hizi wana'enjoy kufungwa goli 1-0 na Simba... ila wako bize na simba kuliko timu yao
 
Kijana wa yanga naona unatokwa povu sana juu ya simba. Kwanza napenda ujue kwamba timu ya simba inabadilika kutokana na umuhimu wa mechi. Sote ni mashahidi kabla ya kuingia kwenye makundi mechi zilikua ni kama hatua tunayoiendea. Tulianza na waswati wakala 4 - 1 tukaenda kwao wakala 5 - 0 tukaenda zambia tukapigwa 2 - 1 tukaja home wakachezea kichapo 3 - 1 tukaingia makundi. Katika mechi za makundi simba ilijikita sana kwenye mechi za nyumbani ili kukusanya point 9 natukafanikiwa. Sasa tumebadilika gozi litapigwa kisawa sawa na waliodhani simba wanafungika kirahisi ugenini watajuta kutufahamu.
 

Ligi ni ligi ina mkakati wake na mtoano ni mtoano nao una mkakati wake.

Je hufahamu ya kwamba wakati wa kugombea kuingia makundi ya ligi ya mabingwa, Simba iliongoza Africa kwa kufunga mabao mengi au unajifanya kusahau, na ilifunga nje ndani.
Simba 4 Mbabane 1, Mbabane 0 Simba 4
Nkana 2 Simba 1, Simba 3 Nkana 1
Aggregate 12 - 4
 
Uzi za hivi ambazo ni za wale wanaoteseka zinagarauka hapa JF kabla ya mchezo wa mwisho wa Simba ..SIMBA akipindua meza ,mambo yanakua kimya..yote kwa yote robo fainali ni mafanikio makubwa kwa sasa hatakama mnateseka


Kulitaka MWANA kulipewa MWANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…