TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Halafu kuna watu wakiambiwa ukweli utasikia ooh wanakwepa kodi akili zingine za kijinga toka tani elfu 40 mpaka tani 1000 si hatari hiyo..kisha TRA wanakuja na mbwembwe za kukusanya kodi kwa 98.9% sijui kama wana mapenzi mema na nchi hii au ni kumfurahisha boss wao
 
Kamati ya bunge viwanda yasema ni lazima kuitishwa kikao cha wadau wa.bandar........Kwani kwa kipindi.cha nyuma Bandari ya Dar es Salam muda kama huu wanakuwa.wameshapokea Mizigo ya Tani Elfu arobaini lakini cha ajabu mpaka kufikia sasa ni tani elfu moja tuuu......Sasa wanaulizana wanaitaka TRA iwaambie ni wapi hapo wanapata hayo mapato wanayosema yanaongezeka kila siku. Lakini pia kamati imewatupia lawama wanamshauri rais kuwa hawamshauri vizuri........????????????????????????????????????????????????????????

Bado tunaendelea na filamu ya nchi yakusadikika.....
Source:ITV News
 
Naona kuna hii kadhia ya mizigo kupungua bandarini
Kamati ya Bunge imekutana na wadau Bandarini na wamekiri mizigo kupungua na kuomba wahusika kukutana na kutafuta suluhisho, huku wakiwalaumu Wataalam kwa kushindwa kumshauri Mh Rais vizuri

Chanzo ITV news


Upinzani walilalamika Sana hili la bandari na utalii lakini jamaa akasema yeye Ni baunsa WA njaa, njaa ikimuona inakimbia nasubiri mwisho wa mpambano nani ataibuka kidedea ingawa mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka kisa watu wameficha noti
 
Kamati ya bunge leo imeshangaa baada ya kufika bandari ya dar na kukuta hali ya bandari ikiwa kavu haina mizigo.. Wakati huo mkurugenzi wa TPA akikiri wazi kwamba kwa sasa hali ya bandari sio nzuri

Kamati hiyo imeiwatupia lawama washauri wa rais kwa kushindwa kumshauri vizuri rais kuhusu kupungua mizigo bandarini

Pia kamati hiyo imetaka tra waseme wazi Pesa zinazoongezeka kila mwezi zinatoka wapi waki hali ya bandari ni mbaya

Pia kamati imeomba mjadara wa haraka kunusuru hali ya bandari ya dar es salaam

Chanzo: ITV habari
 
Kazi ya wabunge Ni kuishauri serikali kazi ya Waziri Ni kumshauri raisi kila ngazi ina ukomo wake ila kwa mtukufu sijui kama atakibali ingawa naamini hakuna baunsa WA njaa
Yap,ndo maana nikasema wabunge wangeshauri vyema kuhusu hilo katika kikao cha bajeti kilichopita basi mawaziri wangefikisha ushauri huo kwa Rais ila kama waliona hakuna tatizo wasibebeshe mzigo huo watu wengine ila waseme tu kila mmoja hajafanya kile kinachotakiwa.
 
Juzi kati kuna huyo boss wa bandari alisema...bandari mambo safi mizigo ni mingi....leo wamekanusha..
kaka usimuonee dg alikuwa sawa hutakiwi kuwa tofauti na mamlaka eeeh we si umeona kama cdm wenyewe wameghairi ukuta sembuse dg kumridhisha mkuu
 
1.Mamlaka ya bandari yakiri upungufu wa mizigo bandarini.
2.Kamati za bunge zaitaka TRA ieleze inatoa wapi hizo kodi wakati idara nyingine zinalalamika hali sio nzuri
3.Kamati za bunge zawalaumu washauri wa Rais kushindwa kumshauri kwa mambo yanayohitaji UTAALAMU.



ITV habari saa 2
Labda kuna mtambo wa kufyatua mihela ama la ni zile noti za maruhani kama sio pesa za chumaulete
 
Wataalamu wanapofanya mambo kisiasa. Ukweli ni kwamba, bandarini hali ni mbaya ila wakisema ukweli wanaogopa kutumbuliwa.

Hata TRA waseme hizo hela wanatoa wapi, usije kukuta kuna double counting na data za kupikwa.
 
Back
Top Bottom