TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Halafu kuna watu wakiambiwa ukweli utasikia ooh wanakwepa kodi akili zingine za kijinga toka tani elfu 40 mpaka tani 1000 si hatari hiyo..kisha TRA wanakuja na mbwembwe za kukusanya kodi kwa 98.9% sijui kama wana mapenzi mema na nchi hii au ni kumfurahisha boss wao

Sasa unataka waseme kweli afukuzwe kazi. Hata kama me natoa tu takwimu kama bwana mkubwa anavyotaka. Bandari inaingiza ngapi trilioni mbili...😵😵
 
Walioficha pesa majumbani kwao wanawajua lakini wanawaogopa ni wale waliopokea rushwa za mabilioni toka kwa Ruge na kutumia mifuko ya Rambo na ndoo za plastic kwenda kubebea rushwa toka kwa Ruge akina Chenge, Ngeleja, Tibaijuka, maofisa wa ndani ya Ikulu na wengineo lakini wanawagwaya kuwagusa labda nao wameshatembeza bulungutu. Hivi ile kesi ya Tibaijuka ya kudaiwa kulipa kodi kutoka kwenye rushwa aliyopokea iliishia wapi vile? Na hao TRA mbona Chenge hawakumfungulia kesi!!!? Hahahahahaha Tanzania yetu nchi inayofananishwa na kichwa cha mwendawazimu kila kinyozi kutaka kujifunza kunyoa nywele kupitia kichwa cha mwendawazimu.

Mpaka wanahisi tumeficha hela kwenye Nyumba Zetu za nyasi
 
Upinzani uliposema wakaonekana wanawatetea wakwepa kodi, jamaa akasema asiyetaka na asije, jamaa akatuaminisha watz kuwa anaweza kushindana na njaa na akashinda watz tukamuachia uwanja yetu macho tunasubiri nani atainuka kidedea lakini juzi Kati mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka watu wameficha noti kwenye makabati
sKushindana na njaa!!! Hahaaa
 
Labda washauri wanaogopa kumwambia ukweli mfalme....

Tatizo TRA wenyewe wanatoza kodi kwa kuwakomoa wafanyabiashara.

Imefika wakati kufanya biashara Tanzania ni kama dhambi.!
Hivi kiongozi ukiwa unaogopa kumshauri boss wako kuna umuhimu gani wa kufanya kazi kama mshauri na je unakuwa na mapenzi mema na nchi yako maana Rais siyo mungu anakosea na anatakiwa aelekezwe.
 
Kuna factors nyingi, mojawapo ni kuwa kipindi cha JK kulikuwa na Memorundum ya kuipa unafuu fulani mizigo kutoka china, lengo likiwa ni kustimulate biashara kati ya Wafanyabiashara wa Kitanzania, wanaochukua mzigo china na Wazalishaji wa China, sasa baada ya awamu hii kuingia madarakani, wameondoa hiyo kitu, matokeo yake Watanzania wanaokwenda China kufunga mzigo wamepungua.
 
Hapo bado kwenye biashara na viwanda...maana uuzaji bidhaa umepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na fedha kuwa ngumu lakini pia watu kukamuliwa sana kodi.Haiprndezi katika nchi yetu hii ambayo mfumo wa kodi bado haujawa mzuri kung'ang'ania mgawane faida ya nusu kwa nusu kati ya mfanyabiashara na serikali.Hotel kadhaa zimefungwa na Bar kadhaa zimefungwa...watu kuanzisha biashara mpya wanaogopa usalama wa mitaji yao.
 
Maskini! aliogopa kusema kweli kwa kuhofia kuitwa mchochezi na hivyo uteuzi wake kutenguliwa almaarufu kutumbuliwa sasa kaamua kusema ukweli baada ya kutembelewa na Wabunge!

Kamati ya bunge leo imeshangaa baada ya kufika bandari ya dar na kukuta hali ya bandari ikiwa kavu haina mizigo.. Wakati huo mkurugenzi wa TPA alikiri wazi kwamba kwa sasa hali ya bandari sio nzuri

Kamati hiyo imeiwatupia lawama washauri wa rais kwa kushindwa kumshauri vizuri rais kuhusu kupungua mizigo bandarini


Pia kamati hiyo imetaka tra waseme wazi Pesa zinazoongezeka kila mwezi zinatoka wapi waki hali ya bandari ni mbaya

Pia kamati imeomba mjadara wa haraka kunusuru hali ya bandari ya dar es salaam

Chanzo: ITV habari
 
Sasa unataka waseme kweli afukuzwe kazi. Hata kama me natoa tu takwimu kama bwana mkubwa anavyotaka. Bandari inaingiza ngapi trilioni mbili...😵😵
Sasa unadanganya ili iweje? Unakuwa una mapenzi mema na nchi yako kweli? Hivi somo la uzalendo/uraia linakuwa na maana gani kama hutimizi katika kuwasaidia wananchi na na Taifa kwa ujumla
 
Kweli hii Awamu haina rafiki Na raia, kila mtu anajuuuuutrraaaaaa, Na hali ya Maisha
 
Sasa itakuwaje tena, uchumi utakuwaje, naomba mchukue hatua haraka sana kuokoa hali hii
 
Mbwembwe zote zimeishia kwenye aibu hii.

Ni wazi mapato ya mwezi tunayosomewa ni madeni ya nyuma sasa njia ya muongo ni fupi uchumi umekwama nadhani Leo ndiyo ccm watasadiki kuwa demokrasia na uchumi ni pande mbili za sarafu moja ukisigina kimoja umesigina vyote.
 
Hawa jamaa mwanzoni walifikiri ni business es usual huku wakitumia zaidi ya 95% ya muda wao kuwapiga vijembe ukawa badala ya kujua kilichokuwa mbele yao. Sasa leo ndio wanajidai 'kugundua' eti na VAT kwenye miamala ya simu. Muda sio mrefu hata wale wanaodhani Mbowe ni mkwepa kodi za NHC pale Mkwepu wataelewa inamaanisha nini!
Kuna Mh Mbunge mmoja kwa habari ya ITV usiku kauliza swali hilo.
Si ndo 'uchochezi' wenyewe huo?
 
Back
Top Bottom