TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Hili nalo ni pigo la aibu kwa Serikali yetu
Sijui Watakuja na lipi sasa mana kila aina ya ukweli wanaupindisha uonekane ni uongo
Sasa muhimili mwingine wa Dola umetambua tatizo na kuamua kuliweka wazi, hii inamaanisha tunaongozwa na Serikali inayodangaya wananchi wake kwa kutoa taarifa zisizo sahihi
 
Hatuwezi kurudi kama zamani tena maana Msumbiji wana reli ya uhakika na usafirishaji wa reli ni rahisi kuliko barabara.
 
kamishna TRA anasema mapato ya bandari yameongezeka na wakuregenzi wa bandari wanasema mapato yamepungua kwakuwa mizigo hakuna BORA KIAMA KIJE TU KWAKUWA HAKUNA MUADIRIFU CCM
Lugha gongana
 
Toka tani 40,000 hadi tani 1000 nataka TRA watwambie kodi wanayokusanya kwa kiwango cha lami kama wanavyojinadi wanaitoa katika vyanzo vipi? Na wale waliokuwa wanapika kelele kuwa watu wanakwepa kodi wanaweza wakawasaidia kujibu pia
 
Yule waziri aliesema kuwa mazingira ni rafiki kuliko nchi jirani na tutegemee flow ya mizigo na hakuna upungufu wa mizigo kupitia tbc na itv leo imekuwajee.... Au ni serikali ya matamko na matukioo nauliza tuu
 
Tulieni Mnyooke!

Wakati wa JK mlidhani mambo yanajiendea tu ndio sababu mliimbishwa nanyi Mkaitikia kiitikio eti Kuna Ombwe la Uongozi.

Bandari ilipovamiwa kwa Mbwembwe mkashangilia mlidhani anakomolewa Jakaya. Magari yamepungua kutoka 3,500 mpaka 1,500 na bado mpaka itafika 500 kwa siku.

Sasa Chanjo kadhaa zimeanza kuadimika.

Lazima Mnyooshwe na mtanyooka Tu.
Mapumziko Mema Rais Mstaafu Kikwete kuna watu walidhani wakati wako Mambo yanajiendesha tu!
Mount Meru ipo Mnadani inauzwa kwa kukosa wateja
Zingine zinageuzwa Hostel bila ya kujua Pass mark zimeongezwa kupunguza Wanafunzi Vyuo vikuu.

Wa Vietnam wamefika Dar Jana wameenda mpaka Msoga kuchota Hekma halaf kuna Vichaa walitufundisha eti ni Rais Dhaifu.
Naupenda sana Utawala na Leadership style ya Magufuli kwa kuwa inathibitisha nilichokuwa naamini Juu ya Jakaya Kikwete.

Wale walioruhusiwa kufanya Siasa kwa uhuru walituaminIsha wanafanya hivyo kutokana na Ujasiri na uthubutu wao sio Utashi wa Rais Leo hii wote wamefyata na Mwanamume Mmoja anazunguka Nchi nzima kupiga Mikutano
 
Namba huwa haziongopi mwisho wa siku itajulikana tu
 
Labda washauri wanaogopa kumwambia ukweli mfalme....

Tatizo TRA wenyewe wanatoza kodi kwa kuwakomoa wafanyabiashara.

Imefika wakati kufanya biashara Tanzania ni kama dhambi.!
 
Upinzani uliposema wakaonekana wanawatetea wakwepa kodi, jamaa akasema asiyetaka na asije, jamaa akatuaminisha watz kuwa anaweza kushindana na njaa na akashinda watz tukamuachia uwanja yetu macho tunasubiri nani atainuka kidedea lakini juzi Kati mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka watu wameficha noti kwenye makabati
 
Makubwa haya......bwanamkubwa hajuwi hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…