Halafu kuna watu wakiambiwa ukweli utasikia ooh wanakwepa kodi akili zingine za kijinga toka tani elfu 40 mpaka tani 1000 si hatari hiyo..kisha TRA wanakuja na mbwembwe za kukusanya kodi kwa 98.9% sijui kama wana mapenzi mema na nchi hii au ni kumfurahisha boss wao
Mpaka wanahisi tumeficha hela kwenye Nyumba Zetu za nyasi
Sasa TRA wanavunja rekodi kila mwezi ya makusanyo kivipi?
sKushindana na njaa!!! HahaaaUpinzani uliposema wakaonekana wanawatetea wakwepa kodi, jamaa akasema asiyetaka na asije, jamaa akatuaminisha watz kuwa anaweza kushindana na njaa na akashinda watz tukamuachia uwanja yetu macho tunasubiri nani atainuka kidedea lakini juzi Kati mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka watu wameficha noti kwenye makabati
Sasa TRA wanavunja rekodi kila mwezi ya makusanyo kivipi?
Hivi kiongozi ukiwa unaogopa kumshauri boss wako kuna umuhimu gani wa kufanya kazi kama mshauri na je unakuwa na mapenzi mema na nchi yako maana Rais siyo mungu anakosea na anatakiwa aelekezwe.Labda washauri wanaogopa kumwambia ukweli mfalme....
Tatizo TRA wenyewe wanatoza kodi kwa kuwakomoa wafanyabiashara.
Imefika wakati kufanya biashara Tanzania ni kama dhambi.!
Kamati ya bunge leo imeshangaa baada ya kufika bandari ya dar na kukuta hali ya bandari ikiwa kavu haina mizigo.. Wakati huo mkurugenzi wa TPA alikiri wazi kwamba kwa sasa hali ya bandari sio nzuri
Kamati hiyo imeiwatupia lawama washauri wa rais kwa kushindwa kumshauri vizuri rais kuhusu kupungua mizigo bandarini
Pia kamati hiyo imetaka tra waseme wazi Pesa zinazoongezeka kila mwezi zinatoka wapi waki hali ya bandari ni mbaya
Pia kamati imeomba mjadara wa haraka kunusuru hali ya bandari ya dar es salaam
Chanzo: ITV habari
Sasa unadanganya ili iweje? Unakuwa una mapenzi mema na nchi yako kweli? Hivi somo la uzalendo/uraia linakuwa na maana gani kama hutimizi katika kuwasaidia wananchi na na Taifa kwa ujumlaSasa unataka waseme kweli afukuzwe kazi. Hata kama me natoa tu takwimu kama bwana mkubwa anavyotaka. Bandari inaingiza ngapi trilioni mbili...😵😵
Kuna Mh Mbunge mmoja kwa habari ya ITV usiku kauliza swali hilo.
Si ndo 'uchochezi' wenyewe huo?