TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Hapo sasa.

Watu wengi hawawezi kukuelewa unachosema hapa.

Hii serikali ni ya ujanja ujanja sana. Ina ulaghai mwingi sana. Ni watu wachache sana, kama Tundu Lissu wanaoweza kutambua ulaghai mwingi unaotumiwa na watu hawa..

Hata Mbowe bila shaka bado kanasa kwenye kokolo la hawa walaghai wakubwa!

Kila jambo, wao ni ujanja ujanja tu, hakuna wanachokwambia cha ukweli moja kwa moja!.
Royal Tour hadi leo ni kitendawili. Wamasai wanahamishwa kule ili wapishe mawindo ya wenye pesa;. hakuna anayejua pesa za ujenzi wa zile nyumba Handeni zilitoka wapi!

Hii ni serikali inayouza wananchi wake utumwani wao wakichekelea kwa kudai wamewapa wananchi ajira!
Hii ni balaa!
 
Yajayo yanafurahisha. Kwanza tunapigwa na MATOZO YA KUFA MTU. TUNAKOPA KAMA TUNAKUFA KESHO. TUNAWAPA MIKATABA HAO WALIOWAFANYA WATUMWA BABU NA BIBI ZETU.
TWAULIZA VIONGOZI WETU NI WATANZANIA AU WAGENI??!!!
😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Wachangiaji wengi humu ni wajinga. Nchi haikurupuki tu bila deep scrutiny. Bandari yetu kwa sasa inanifaisha wachache. Pia inafanya kazi chini sana ya kiwango na kwa gharama kubwa. Ni lazma awepo mwekezaji kama huyo ili kuweka tija. Sioni anaeshauri nini kifanyike mbali ya KUHARISHA NGONJERA TUPU. Hovyo kabisa
 
Serikali imechukua mkopo kuboresha Bandari ya DSM ikiwemo kuongeza kina ili meli kubwa zaidi ziweze kutua. Baada ya maboresho hayo kabla taifa halijafaidi matunda yake anakodishwa mwarabu. Kwa hiyo serikali ilienda kukopa ili imfaidishe muarabu ama??!!
 
Hivi wananchi watatoaje mawazo yao bila kuweka mkataba wazi. Wanatoa mawazo ya nini hasa? Yaani wananchi wakubali tu bila kujua tunanufaika vipi na mkataba ni wa muda gani? Badala ya kujibu waweke mkataba hapa
 
Mambo watakaofanya hao waarabu ni mepesi sana hata sisi tunaweza kufanya
 
Mpaka sasa hakuna kiongozi wa upinzani kaongea lolote sijui vijana ccm akili zenu zipo matakoni
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Mh...!!
 
Kwa hiyo walichosema TPA ni uongo?.
 
Vipi mkuu, siku hizi sikuoni kijiwe cha kahawa Uhuru Kariakoo.
 
Inasikitisha sana kwa yanayoendelea nchini.

Safari za Dubai zisizoisha nilizitilia shaka sana zingetuzalishia bomu.
Alikuwa akitafuta wawekezaji, au unahisi hapa kajichomeka yeye kiaina.
 
Hoja zetu watanzania hapa mtandaoni ni nzuri na zenye mashiko , zingepata nguvu kama zingesindikizwa na maandamano kadhaa walao ingeonyesha tupo sirious kidogo.
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Uko sahihi kabisa. TPA jambo hili haliwahusu wao ni robot tu hawana capacity ya kulisemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…