TPA: Serikali haijaipa DP World Kandarasi ya undeshaji Bandari ya Dar es Salaam kwa Miaka 100
Maria Sarungi, Kenya na kampeni ya upotoshaji dhidi ya DP World na Tanzania

* DP World akija Tanzania, Bandari ya Dar es Salaam itaongeza idadi ya shehena na itaendelea kuipiku Bandari ya Mombasa kwa ufanisi. Muathirika Mkuu wa ujio wa DP World nchini Tanzania na uimarishaji wa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ni uchumi wa KENYA ✅

* Maria Sarungi ambaye anasimamia mijadala ya Twitter Spaces kufanya kampeni ya upotoshaji dhidi wa ujio wa DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam anaishi na kufanya kazi zake nchini KENYA 🤔

* Wazungumzaji vinara kwenye Twitter Spaces ya Maria ambao wanakosoa na kupinga vikali ujio wa DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambao Maria anawatumia kama "wataalamu" wa kuchambua mkataba wa DP World na Tanzania ni Nyanje wa Nyanje na Mwaura Robert, ambao ni raia wa KENYA 🤷

Somo la leo:

1. Akili za mbayuwayu changanya na zako 🚶

2. Connect the dots (1+1=....)
 
Maria Sarungi, Kenya na kampeni ya upotoshaji dhidi ya DP World na Tanzania

* DP World akija Tanzania, Bandari ya Dar es Salaam itaongeza idadi ya shehena na itaendelea kuipiku Bandari ya Mombasa kwa ufanisi. Muathirika Mkuu wa ujio wa DP World nchini Tanzania na uimarishaji wa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ni uchumi wa KENYA...

Kumbe Shangazi anaishi Kenya siku hizi?

Hii connection ni kali
 
Maria Sarungi, Kenya na kampeni ya upotoshaji dhidi ya DP World na Tanzania

* DP World akija Tanzania, Bandari ya Dar es Salaam itaongeza idadi ya shehena na itaendelea kuipiku Bandari ya Mombasa kwa ufanisi. Muathirika Mkuu wa ujio wa DP World nchini Tanzania na uimarishaji wa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ni uchumi wa KENYA...

Kwenye miradi mikubwa ya kuleta mageuzi ya uchumi na maendeleo ya Tanzania, JPM alikuwa very ruthless kuhakikisha kuwa wasaliti wanashughulikiwa

Hawa vibaraka wakiachiwa wanaweza kuvuruga nchi kwa manufaa ya mataifa ya nje

Hii ni vita ya uchumi
 
Maria Sarungi, Kenya na kampeni ya upotoshaji dhidi ya DP World na Tanzania

* DP World akija Tanzania, Bandari ya Dar es Salaam itaongeza idadi ya shehena na itaendelea kuipiku Bandari ya Mombasa kwa ufanisi. Muathirika Mkuu wa ujio wa DP World nchini Tanzania na uimarishaji wa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ni uchumi wa KENYA...
Serikali ijifunze kufanya maamuzi Kwa kuzingatia Tija badala ya maslahi ya wanaofaidika na inefficiency ya miaka na miaka hapo bandarini..

Kwani Serikali inashindwa kutoka hadharani kuelezea Umma kwamba tutaibinafsisha Kwa sababu a,na na c?

Na huu ubinafsishaji italeta faida d,e na f?

Kama.Nchi zote Duniani zimebinafsisha na Mbarawa alitolea mfano ya Bandari kibao tuu hapa Africa shida Iko wapi Kwa Tanzania?

Kenya lazima.wafanye hivyo Kwa sababu ni washindani Wetu hiyo Haina ubishi.
 
Manake bandarini naskia hata ukipata kazi ya ufagiaji tu..umeula. nchi ina matobo mengi sana..watanzania wengi wana mentality ya wizi..na hii nadhani wanaiga kutoka kwa viongozi.

Baada ya kubifsisha bandari inabidi tuhamie kwenye mamlaka zingine kama TRA, TANAPA, TANESCO, nk. Pengine ufanisi na mapato yataonekana.

Haiwezekani kwa mfano mtu anaajiriwa TRA baada ya mwaka ana gari Kali, nyumba na demu mkali..ukiangalia mishahara ya kawaida..kumbe wizi na rushwa ndio vinawatambisha.
 
Serikali ijifunze kufanya maamuzi Kwa kuzingatia Tija badala ya maslahi ya wanaofaidika na inefficiency ya miaka na miaka hapo bandarini....
Bahati mbaya sana nchi yetu wananchi wake wanamihemkoo sana wataongea kwa mihemko na sio kwa facts..

Elimu na exposure ni muhimu sana.
 
Manake bandarini naskia hata ukipata kazi ya ufagiaji tu..umeula. nchi ina matobo mengi sana..watanzania wengi wana mentality ya wizi..na hii nadhani wanaiga kutoka kwa viongozi.

Baada ya kubifsisha bandari inabidi tuhamie kwenye mamlaka zingine kama TRA, TANAPA, TANESCO, nk. Pengine ufanisi na mapato yataonekana.

Haiwezekani kwa mfano mtu anaajiriwa TRA baada ya mwaka ana gari Kali, nyumba na demu mkali..ukiangalia mishahara ya kawaida..kumbe wizi na rushwa ndio vinawatambisha.
Ingekuwa ni vyema tungeibinafsisha Serikali kwani ndio imeshindwa kuwasimamia watu iliyowaajiri yenyewe.
Huko kwingine ni kutapatapa tu na kuongeza matatizo
 
Bahati mbaya sana nchi yetu wananchi wake wanamihemkoo sana wataongea kwa mihemko na sio kwa facts..

Elimu na exposure ni muhimu sana.
Ni ujinga kusikiliza Kila mtu anachotaka, haiwezekani Libandari Kwa miaka zaidi ya 60 hakuna kitu Cha maana inafanya..

Yaani uache kubinafsisha ambapo utapata growth ya mapato Kwa Zaidi ya Trilioni 1 uje kusubiria watu wazembe wajinufaishe hapo bandarini..

Mwendazake licha ya kujaza wanajeshi sijui Tisa nk Kuna Cha maana kilifanyika? Kwani wao sio Watumishi hawataki.pesa?
Dawa ya kukumesha huo ujinga ni private sector full stop.
 
Tunahitaji mjadala mipana sana kabla kuamua hatma kukodisha bandari yetu jamani watu wa tiss wapo kushauri ?
 
Ingekuwa ni vyema tungeibinafsisha Serikali kwani ndio imeshindwa kuwasimamia watu iliyowaajiri yenyewe.
Huko kwingine ni kutapatapa tu na kuongeza matatizo
Huko utagusa sharubu za simba.
 
Je huo mkataba upo? Kama haupo mbona kwenye website ya bunge wameondoa notisi yao ya kuazimia kupitisha huo mkataba? Baada ya watu kuanza kupiga kelele?
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100

Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.

Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.

Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.

c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.

Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.

f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani tatizo sio uwekezaji ili kuboresha ufanisi.

Tatizo ni muda wa mkataba 100yrs / 50 yrs / 30 yrs / 20 yrs /10 yrs?

Mie ngeshauri mkataba uwe miaka 25 (mtoto kazaliwa, kaenda primary, sekondari, chuo na bado hajapata ajira)
 
Sijauona huo mkataba lakini kama ni kweli viongozi wetu wametuingiza kwenye mkataba wa miaka 100 basi kuna shida mahali sio bure. Maana yake tumedhulumu haki na wajibu wa vizazi vijavyo bila sababu za msingi kabisa. Kama sisi ni wapuuzi hatuna uwezo wa kuendesha bandari yetu tuna uhakika gani kuwa vizazi vijavyo vitakuwa wapuuzi kama sisi kiasi wao washindwe kuendesha sekta muhimu ya uchumi na usalama wa nchi kama bandari. Kwa nini tuwaingize watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe kwenye mkataba wasiouelewa? Vipi Nyerere angeamua kubinafsisha kila kitu hawa viongozi wa sasa wangekuta nini cha kubinafsisha? Viongozi wetu wa sasa walikuwa wapi na walikuwa na umri gani wakati nchi inabinafsisha ATCL na TANESCO kwa makaburu halafu wakagundua kuwa ni mikataba ya hovyo ikavunjwa?

Ningewaelewa viongozi wetu iwapo wangeingia mkataba wa kati ya miaka 10 - 20 basi ambao ungekuwa na kipengele cha kuongezwa iwapo watafanya vizuri. Kama Karamagi na TICTS yake tu kwa miaka zaidi ya 20 tuemeona hafai tukabadilisha vipi huyu wa miaka 100 akionekana hafai baada ya mwaka 1 kama nchi tunafanyaje?

Kwa jinsi bunge lilivyo sioni huo mkataba kama kweli upo ukikwama bali utapita bila kupingwa kwa asilimia mia moja na makofi juu. Akija raisi mwingine baada ya miaka kadhaa mbele akaupinga wabunge hao hao watamshangilia na kupitisha azimio la kuupinga kwa asilimia 100.

Pamoja na mapungufu yake spika wa bunge aliyepita Ndugai kuna maneno alizungumza watui tukayachukulia poa lakini kumbe yalikuwa na ukweli kiasi fulani na sasa yameanza kudhihirka wazi.

Ni mtazamo tu
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Wewe tuoneshe wapi pameandikwa miaka 100
 
Ni ujinga kusikiliza Kila mtu anachotaka, haiwezekani Libandari Kwa miaka zaidi ya 60 hakuna kitu Cha maana inafanya..

Yaani uache kubinafsisha ambapo utapata growth ya mapato Kwa Zaidi ya Trilioni 1 uje kusubiria watu wazembe wajinufaishe hapo bandarini..

Mwendazake licha ya kujaza wanajeshi sijui Tisa nk Kuna Cha maana kilifanyika? Kwani wao sio Watumishi hawataki.pesa?
Dawa ya kukumesha huo ujinga ni private sector full stop.
Hakuna shida bandari kubinafsishwa hizi tuhuma za hii kampuni kupewa miaka 100 ni hasara sana huwezi kuongelea tu faida za huo mkataba bila kuhoji masharti ya huo mkataba
 
Back
Top Bottom