TPA: Serikali haijaipa DP World Kandarasi ya undeshaji Bandari ya Dar es Salaam kwa Miaka 100
Hakuna shida bandari kubinafsishwa hizi tuhuma za hii kampuni kupewa miaka 100 ni hasara sana huwezi kuongelea tu faida za huo mkataba bila kuhoji masharti ya huo mkataba
Masharti ndio hojini,kama Kuna masharti yasiyo na faida ambayo sidhani kama yapo ndio yajadiliwe..

Kuna title deed ya miaka 10,33,50 Hadi 100
 
Tangu Enzi za mangungo hadi Karen hii tunapigwa tuuuui
 
Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.

Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya undeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".

Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa a Kimataifa na Umma kwa jumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika boreshaji na endelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.

Ushirikiano wa Nchi mbili za Dubai a Tanzania una lengo la kongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dares Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda pamoja na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari za Tanzania kwenda chi za jirani ambazo zinatumia Bandari zetu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia wekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.

View attachment 2648437View attachment 2648438

Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Hata hamuaniki eti! Maana uzalendo hamna. Zaidi tu mnawaza kujilimbikizia tu mali vichwani mwenu, kupitia ufisaji na upigaji.
 
Si kawaida kwa mikataba kuvuja.

Hili swala la Bandari ya Dar na DP World kuna mzalendo kaamua kutuondolea matatizo maana kashusha Mkataba kama ulivyo na wote walioweka Saini zao

NB: Sasa lazima watafutane maana kitumbua kimeingia mchangaView attachment 2648602View attachment 2648604View attachment 2648603View attachment 2648605View attachment 2648606
View attachment 2648609
Mimi ningekuwa Samia ningeyaachia madanganyika yaendelee na maujinga Yao ya ujamaa,ya nini kujizeesha Bure na majitu yaliyoxoea umaskini na Kuendesha kama mapunda?
 
Hivi kweli imefika sehemu Sisi Watanzania tumeshindwa kujisimamia wenyewe, yaani baada ya miaka zaidi ya 60 tangu tupate uhuru bado hatuwezi kusimamia rasilimali zetu?

Hili jambo linasikitisha sana, hata kama eneo hilo linahitaji uwekezaji, kwa nini isiwe ni wawekezaji wa ndani? Hivi hawa Waarabu ndiyo wakuwapa eneo muhimu kama hilo?

Babu zetu walishindwa kutawaliwa na hawa Waarabu mpaka wakafanya Mapinduzi licha ya hali duni ya kimaisha waliokuwa nayo kipindi hicho, leo hii kizazi hiki cha wasomi wanataka kumrudisha Mwarabu kututawala tena kwa kuwaita kama wawekezaji!

Hili jambo halifai na hata kwa akili ya kawaida lilitakiwa likataliwe na Viongozi bila hata Sisi Wananchi kujua, vitu kama hivi kutuhusisha Wananchi wa kawaida ni kuonesha kuwa Nchi yetu sasa ina ombwe la Viongozi.
 
mkataba upo vizuri sana, mapato kupanda mara 3-4 zaidi ya awali, hili ni jema sana.
Nimekipenda kipengele cha ku fail kufikia malengo tarajiwa inamaanisha mkataba huu "utavunjika rasmi" kipengele hiki kimenigusa hasa kuhusu umakini wa mkataba huu.
Mkataba unasema wa miaka mingapi
Mkuu

Ova
 
Serikali imechukua mkopo kuboresha Bandari ya DSM ikiwemo kuongeza kina ili meli kubwa zaidi ziweze kutua. Baada ya maboresho hayo kabla taifa halijafaidi matunda yake anakodishwa mwarabu. Kwa hiyo serikali ilienda kukopa ili imfaidishe muarabu ama??!!
Hela zinakopwa ili zipigwe wewe shtuka. Watu wanavuna hela za kulisha hadi vizazi vya 10 huko.
 
Si kawaida kwa mikataba kuvuja.

Hili swala la Bandari ya Dar na DP World kuna mzalendo kaamua kutuondolea matatizo maana kashusha Mkataba kama ulivyo na wote walioweka Saini zao

NB: Sasa lazima watafutane maana kitumbua kimeingia mchangaView attachment 2648602View attachment 2648604View attachment 2648603View attachment 2648605View attachment 2648606
View attachment 2648609
Haya bado ni matunda ya ule uchaguzi wa mwaka 2015. Bado tunaendelea tu kuyafaidi. Maana hakuna namna nyingine.
 
Maria Sarungi, Kenya na kampeni ya upotoshaji dhidi ya DP World na Tanzania

* DP World akija Tanzania, Bandari ya Dar es Salaam itaongeza idadi ya shehena na itaendelea kuipiku Bandari ya Mombasa kwa ufanisi. Muathirika Mkuu wa ujio wa DP World nchini Tanzania na uimarishaji wa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ni uchumi wa KENYA [emoji736]

* Maria Sarungi ambaye anasimamia mijadala ya Twitter Spaces kufanya kampeni ya upotoshaji dhidi wa ujio wa DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam anaishi na kufanya kazi zake nchini KENYA [emoji848]

* Wazungumzaji vinara kwenye Twitter Spaces ya Maria ambao wanakosoa na kupinga vikali ujio wa DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambao Maria anawatumia kama "wataalamu" wa kuchambua mkataba wa DP World na Tanzania ni Nyanje wa Nyanje na Mwaura Robert, ambao ni raia wa KENYA [emoji1745]

Somo la leo:

1. Akili za mbayuwayu changanya na zako [emoji124]

2. Connect the dots (1+1=....)
Mbona wanauza vya Tanganyika tu huko kwao hawana cha kuuza ?
 
Na bado mkishauza bandari ya Daslama muingie tena mkenge kumpa mchina ile ya Bagamoyo, kimsingi nchi ilishauzwa kitambooooo, nilipoona bandari wameanza kutoa watu wenye akili na kuweka wale waburushi wa kizimkazi nikajua ohoooo kazi imekwisha, kwakweli Kagame apewe maua yake kabnisaaa, maana aliongea kama utani kwamba apewe bandari kwa miezi kadhaa tu na atafanya wonders, tukamuona mwendawazimu. HANGAYA OYEEEEEE>
 
Kwamba nyie Watanganyika million 61 huko mmeshindwa kuiendesha bandari yenu mpaka muamue kuikodisha.!!??
 
Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.

Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Serikali iwe inatoa taarifa sahihi mapema kila wakati ili wananchi wasipotoshwe.
Hii kukaa kimya mpaka mambo ya kisiasa na kiuchumi yanaharibika, ni kama kutegeshea bomu halafu unakaa mbali kusikilizia linalipukaje.
 
Hivi kweli imefika sehemu Sisi Watanzania tumeshindwa kujisimamia wenyewe, yaani baada ya miaka zaidi ya 60 tangu tupate uhuru bado hatuwezi kusimamia rasilimali zetu?

Hili jambo linasikitisha sana, hata kama eneo hilo linahitaji uwekezaji, kwa nini isiwe ni wawekezaji wa ndani? Hivi hawa Waarabu ndiyo wakuwapa eneo muhimu kama hilo?

Babu zetu walishindwa kutawaliwa na hawa Waarabu mpaka wakafanya Mapinduzi licha ya hali duni ya kimaisha waliokuwa nayo kipindi hicho, leo hii kizazi hiki cha wasomi wanataka kumrudisha Mwarabu kututawala tena kwa kuwaita kama wawekezaji!

Hili jambo halifai na hata kwa akili ya kawaida lilitakiwa likataliwe na Viongozi bila hata Sisi Wananchi kujua, vitu kama hivi kutuhusisha Wananchi wa kawaida ni kuonesha kuwa Nchi yetu sasa ina ombwe la Viongozi.
"Black people are not complete human beings because they don't have a good brain to govern the society as white people are. They are still under the process of becoming the complete human beings". Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Back
Top Bottom