Mtemi mpambalioto
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,436
- 7,955
ujanja ujanjaTigo Postpaid Bando za bei nafuu sana kwa Tsh 15 unapata Gb 15 mwezi mzima , karibu Dm kwa maelezo zaidi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ujanja ujanjaTigo Postpaid Bando za bei nafuu sana kwa Tsh 15 unapata Gb 15 mwezi mzima , karibu Dm kwa maelezo zaidi.
Kuna upotoshwaji mkubwa sana unafanywa juu ya mkataba unaotaka kusainiwa kati ya serikali na kampuni ya DP World na wanasiasa wa upinzani na watu wasio na taarifa sahihi kuhusu jambo hili.
Watu wetu wamezoea kutokusoma mambo na kuokota mambo mitandaoni na kutafanya kuwa ndiyo rasmi. Nimesoma
Uelewa wako mdogo katika masuala nyeti. Wewe fanya kazi ya kuleta mada za Mbowe na umbea mwingine kuhusu CHADEMA.TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .
Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Unawaamini?Nikataka kushangaa How uipe kampuni sehemu ya kimakakati kama bandari miaka mia moja
Haina ukweli wowote hii habari.View attachment 2648505
Bunge la Tanzania linaalika umma kutoa maoni juu ya azimio lake kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai juu ya uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari nchini Tanzania.
Kuna tuhuma nzito katika mitandao ya kijamii kuwa Serikali inataka kuikodisha Bandari kwa taifa Hilo la Uarabuni kwa muda wa miaka 100. Tuhuma hizo zinazidi kutatanisha zaidi hasa pale zinapotaja kuhusu Wabunge 'kuwekwa sawa' ili wapitishe hoja hiyo. Kama tuhuma hizo zina ukweli basi tutakuwa tumefikishwa mahali pabaya sana kama taifa.
Kukodisha Bandari kwa miaka 100 ni sawa na kuuza Bandari kwani kati ya wote tuliopo sasa na watakaozaliwa kesho, hakuna atakayefikia miaka 100 akiwa na nguvu. Uamuzi wa aina hiyo unatakiwa ufikiwe kwa uwazi na uelewa wa hali ya juu. Haiwezekani Wabunge ambao waliingia Bungeni kwa nguvu ya Dola lakini pia waliokosa ridhaa ya wananchi walio wengi ndio wapewe jukumu la kuamua kuhusu hatima ya jambo kubwa kama hilo.
Sisi Askofu Mwamakula tunapenda kutoa wito kwa Serikali yetu kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi tuhuma hizo kabla ya kuendelea na jambo hilo. Lakini pia, tunatoa wito kwa umma wa Watanzania kuungana kwa maslahi mapana ya taifa na vizazi vijavyo kuitaka Serikali uwazi kuhusu mikataba hiyo. Kadharika, tunatoa wito kwa Bunge na Serikali kutofanya haraka katika kuingia mikataba ambayo umma haijaielewa.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Dar es Salaam, 6 Juni 2023.
Uafrika hasa utanzania ni LAANAHivi kweli imefika sehemu Sisi Watanzania tumeshindwa kujisimamia wenyewe, yaani baada ya miaka zaidi ya 60 tangu tupate uhuru bado hatuwezi kusimamia rasilimali zetu?
Hili jambo linasikitisha sana, hata kama eneo hilo linahitaji uwekezaji, kwa nini isiwe ni wawekezaji wa ndani? Hivi hawa Waarabu ndiyo wakuwapa eneo muhimu kama hilo?
Babu zetu walishindwa kutawaliwa na hawa Waarabu mpaka wakafanya Mapinduzi licha ya hali duni ya kimaisha waliokuwa nayo kipindi hicho, leo hii kizazi hiki cha wasomi wanataka kumrudisha Mwarabu kututawala tena kwa kuwaita kama wawekezaji!
Hili jambo halifai na hata kwa akili ya kawaida lilitakiwa likataliwe na Viongozi bila hata Sisi Wananchi kujua, vitu kama hivi kutuhusisha Wananchi wa kawaida ni kuonesha kuwa Nchi yetu sasa ina ombwe la Viongozi.
TPA ni sawa tu na kiranja wa zamu yeye kazi yake ni kutekeleza na kusimamia kinachoamuliwa pale bungeni na bunge la ccm, na wakikaa vibaya utasikia wametumbuliwaTarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.
Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya undeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".
Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa a Kimataifa na Umma kwa jumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika boreshaji na endelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.
Ushirikiano wa Nchi mbili za Dubai a Tanzania una lengo la kongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dares Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda pamoja na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari za Tanzania kwenda chi za jirani ambazo zinatumia Bandari zetu.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia wekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.
View attachment 2648437View attachment 2648438
Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Like ya pili ni ya kwangu. Watanzania tumezoea sana mipasho isiyoumiza kichwa, tuna uvivu wa kutafuta maarifa ule uvivu wa kusoma.Kuna upotoshwaji mkubwa sana unafanywa juu ya mkataba unaotaka kusainiwa kati ya serikali na kampuni ya DP World na wanasiasa wa upinzani na watu wasio na taarifa sahihi kuhusu jambo hili.
Watu wetu wamezoea kutokusoma mambo na kuokota mambo mitandaoni na kutafanya kuwa ndiyo rasmi. Nimesoma makubaliano haya kurasa zote 33 sijaona mahali palipotajwa miaka 100 imekubaliwa kukodishwa DP World bandari.
Sijajua wanaosema bandari imekodishwa miaka 100 wanatoa wapi hizi taarifa! Ni tabia ile ile ya kuzusha mambo na kupayuka bila kuwa na ushahidi. Tabia hii inaleta taharuki sana kwa watanzania bila sababu za msingi.
Wote ni mashahidi wa jinsi TICTS na akina Karamagi wamefanya kazi bandarini kwa miaka 26 na hakuna uwekezaji wamefanya mpaka wamepelekea bandari ya Dar Es Salaam pamoja na umuhimu wake kuzidiwa na bandari mpaka ya Mombasa kwa sababu huduma mbovu na TICTS hawakuwa wanawekeza kwenyw kununua vifaa kwa miaka yote 26 ya mkataba wao. Hatuwezi kuwa na bandari haina vifaa na meli zinasubiri siku 14-21 kupakua mizigo wakati jambo hilo kilitakiwa kufanywa kwa masaa 12-24 tu na hicho ndicho kiwango cha kimataifa cha ufanisi wa bandari kupakua mizigo.
Nani aliwahi kuhoji miaka 26 ya TICTS kuwa watoa huduma hapo bandarini? Nani aliwahi kuwaza na kujua TICTS wamekaa hapo bandarini kwa miaka 26? Marais wangapi wamepita na hawakuwa na uthubutu wa kuwaondoa TICTS pamoja na utapeli wao?
Awamu hii iliamua kuifanya bandari kuwa lango kuu wa uchumi na wakaamua kutafuta muwekezaji mwenye uzoefu na mwenye hela ya kufanya kazi na DP World wakawa chaguo.
Serikali imeenda mbali zaidi kufanya mambo wazi na kupeleka bungeni kujadili jambo hili, nataka watu wanaopinga DP World waje hapa watuambie lini TICTS na mikataba yao ilijadiliwa bungeni kwa uwazi huu?
Haikuwa hivyo kwa kuwa TICTS walikuwa wanagawa rushwa haswa na Karamagi ndiye alikuwa kinara na viongozi wengi wakiopita walikuwa wanufaika.
Serikali hii imekuwa jasiri kuliko zote na kuwang'oa TICTS kwa sababu walikuwa wanadharau mkataba wao na hakuna kitu cha maana wamefanya na bado walikuwa wanapewa kikataba kihovyo hovyo tu na kwa kugawa rushwa.
Upotoshaji unaofanywa kuhusu DP World ni jambo la hovyo na aibu sana. DP World wanakwenda kuifanya bandari ya Dar Es Salaam kuwa ya kisasa na yenye ufanisi sana kutokana na aina ya uwekezaji na fedha wanakwenda kuweka na kufanya mabadiliko kwenye hii bandari.
Wapiga kelele wamejaa Tanzania hii, wengi uwezo wao mdogo wa kuelewa kinachozungumzwa na pia wavivu wa kutafuta maarifa.Wachangiaji wengi humu ni wajinga. Nchi haikurupuki tu bila deep scrutiny. Bandari yetu kwa sasa inanifaisha wachache. Pia inafanya kazi chini sana ya kiwango na kwa gharama kubwa. Ni lazma awepo mwekezaji kama huyo ili kuweka tija. Sioni anaeshauri nini kifanyike mbali ya KUHARISHA NGONJERA TUPU. Hovyo kabisa
Kama TICS hawakufanya na hakuna aliyeweza kuwagusa, unauhakika gani hao DP watafanya? Kwani Tanzania si ile ile na watu ni wale wale? Why then kama uwekezaji haujaleta mafanikio mbadilishe mvinyo wakati chombo ni kile kile?Kuna upotoshwaji mkubwa sana unafanywa juu ya mkataba unaotaka kusainiwa kati ya serikali na kampuni ya DP World na wanasiasa wa upinzani na watu wasio na taarifa sahihi kuhusu jambo hili.
Watu wetu wamezoea kutokusoma mambo na kuokota mambo mitandaoni na kutafanya kuwa ndiyo rasmi. Nimesoma makubaliano haya kurasa zote 33 sijaona mahali palipotajwa miaka 100 imekubaliwa kukodishwa DP World bandari.
Sijajua wanaosema bandari imekodishwa miaka 100 wanatoa wapi hizi taarifa! Ni tabia ile ile ya kuzusha mambo na kupayuka bila kuwa na ushahidi. Tabia hii inaleta taharuki sana kwa watanzania bila sababu za msingi.
Wote ni mashahidi wa jinsi TICTS na akina Karamagi wamefanya kazi bandarini kwa miaka 26 na hakuna uwekezaji wamefanya mpaka wamepelekea bandari ya Dar Es Salaam pamoja na umuhimu wake kuzidiwa na bandari mpaka ya Mombasa kwa sababu huduma mbovu na TICTS hawakuwa wanawekeza kwenyw kununua vifaa kwa miaka yote 26 ya mkataba wao. Hatuwezi kuwa na bandari haina vifaa na meli zinasubiri siku 14-21 kupakua mizigo wakati jambo hilo kilitakiwa kufanywa kwa masaa 12-24 tu na hicho ndicho kiwango cha kimataifa cha ufanisi wa bandari kupakua mizigo.
Nani aliwahi kuhoji miaka 26 ya TICTS kuwa watoa huduma hapo bandarini? Nani aliwahi kuwaza na kujua TICTS wamekaa hapo bandarini kwa miaka 26? Marais wangapi wamepita na hawakuwa na uthubutu wa kuwaondoa TICTS pamoja na utapeli wao?
Awamu hii iliamua kuifanya bandari kuwa lango kuu wa uchumi na wakaamua kutafuta muwekezaji mwenye uzoefu na mwenye hela ya kufanya kazi na DP World wakawa chaguo.
Serikali imeenda mbali zaidi kufanya mambo wazi na kupeleka bungeni kujadili jambo hili, nataka watu wanaopinga DP World waje hapa watuambie lini TICTS na mikataba yao ilijadiliwa bungeni kwa uwazi huu?
Haikuwa hivyo kwa kuwa TICTS walikuwa wanagawa rushwa haswa na Karamagi ndiye alikuwa kinara na viongozi wengi wakiopita walikuwa wanufaika.
Serikali hii imekuwa jasiri kuliko zote na kuwang'oa TICTS kwa sababu walikuwa wanadharau mkataba wao na hakuna kitu cha maana wamefanya na bado walikuwa wanapewa kikataba kihovyo hovyo tu na kwa kugawa rushwa.
Upotoshaji unaofanywa kuhusu DP World ni jambo la hovyo na aibu sana. DP World wanakwenda kuifanya bandari ya Dar Es Salaam kuwa ya kisasa na yenye ufanisi sana kutokana na aina ya uwekezaji na fedha wanakwenda kuweka na kufanya mabadiliko kwenye hii bandari.
Ukiamini wasemacho ndo kuingia mkenge.Kama kweli hamjabinafisha barikiweni
Sio bandari ya dar tu, ni bandari zoteNa bado mkishauza bandari ya Daslama muingie tena mkenge kumpa mchina ile ya Bagamoyo, kimsingi nchi ilishauzwa kitambooooo, nilipoona bandari wameanza kutoa watu wenye akili na kuweka wale waburushi wa kizimkazi nikajua ohoooo kazi imekwisha, kwakweli Kagame apewe maua yake kabnisaaa, maana aliongea kama utani kwamba apewe bandari kwa miezi kadhaa tu na atafanya wonders, tukamuona mwendawazimu. HANGAYA OYEEEEEE>
Huu ndo ukweli.watu wanajitoa tu ufahamu kwa maelezo mengi ambayo hayana maana.Ingekuwa ni vyema tungeibinafsisha Serikali kwani ndio imeshindwa kuwasimamia watu iliyowaajiri yenyewe.
Huko kwingine ni kutapatapa tu na kuongeza matatizo
Sijaelewa na sitoelewa na siko tayari kuelewa na sina nia ya kuelewa hadi mafisadi wote wa bandari (wa leo na wa zamani) wawajibishwe na kufilisiwa hata kama wako makaburini.Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.