TPA: Tutajenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa Mpira wa Michezo hapa Kizimkazi

TPA: Tutajenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa Mpira wa Michezo hapa Kizimkazi

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Bandari Tanzania Bara (TPA) ameahidi kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa michezo katika eneo la Kizimkazi, Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA ameyasema hayo leo katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hakika maendeleo hayana mahali.
Weka taarifa sawa, jana nimefuatilia tukio hilo, na ni wadau wa maendeleo kwa umoja wao ndio watakaojenga uwanja huo wa kisasa, ambao pamoja na vingi utakuwa na viwanja vitatu vya mpira, jengo la mazoezi, viwanja vya mpira wapete, mkono, mabwawa ya kuogelea etc

Na wadau hao ni benki zaidi ya tano nmb, crdb,azania,nbc,Equity na mashirika kama Tanroads, Tanesco, TPA huku wakiahidi kuwa wadau wengine wataungana nao baadae

Ukisema TPA peke yake unamislead watu for no reason!, Anaehitaji taarifa zaidi na uwanja ulivyo afuatilie streaming ya live ya jana ya Ikulu kule Youtube, imeelezea kwa kina na ilisomwa na Nsekela wa CRDB mbele ya Rais Samia
 
TPA inajiingizaje Zanzibar ili Hali Wana mamlaka Yao ya bandari hao wazanzibar
 
TPA ndio wanaoahidi kujenga uwanja mkubwa wa kisasa Kizimkazi? Kwa nini mamlaka ya bandari Zanzibar isichuke tenda hiyo?
Au zile pesa za wajomba kuhusu bandari za Tanganyika ndio mkondo 😲

Kwa sababu tipiei itatoa mpunga wa dipii weldi...
 
Kwani TPA wana kampuni ya ujenzi mpaka waseme watajenga?
 
Hivi wewe mkurugenzi mziam kweli?
Hizo pesa unazochezea hyko si ukanunue Crane japo moja?
Hilo halina tija kabisa ndugu huko!
 
Ukiwa na furaha sana au huzuni sana usitoe ahadi yoyote.

Hao TPA kabla ya kujenga uwanja Zanzibar, inabidi warekebishe eneo lao Kurasini la Harbours Club. Wangeboresha eneo lao lenye uwanja mzuri wa Basketball,Football na Handball pia wangejenga sehemu ya michezo mbalimbali maana eneo ni kubwa lingetosha kuweka swimming na sehemu za michezo ya watoto.

Wangeweka hata nyasi bandia wanazobaki nazo baada ya watu kushindwa kulipa storage charges. Kiwanja chao kingekodishwa na timu kwenye michezo mbalimbali.
 
Nchi hii bhana ina mambo ya ajabu sana nadhani ndio kiwango cha Elimu yetu hiyo...
 
Huyo alietoa hio ahadi labda hajui kuhusu katiba yake au anamuona raisi kama mjinga fulani wa kudanganywa kwa ahadi zisizoweza tekelezeka. Kuna mawili kutojua au kumuona mwenzake mjinga ila boss wa tpa azingatiwe anawezakuwa na hoja
 
Eeeh MUNGU fanya jambo.
Tulifurahi sana 2021 Mwezi wa 3, tarehe hatuijui ila wewe na wahusika wanaijua.

Mungu fanya jambo, jioneshe tena watu wafurahie, ila kamwe tusirudi kama zamani.
Fanya jambo Baba
 
Huyo ni speaker tu, angalia sauti inapotoka 🏃🏃🏃
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Bandari Tanzania Bara (TPA) ameahidi kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa michezo katika eneo la Kizimkazi, Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA ameyasema hayo leo katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hakika maendeleo hayana mahali.
tpa haina uwezo wa kujenga ywanja wa kisasa pesa hiyo hawana..labda kama utajengwa kwa miaka 10 sawa..
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Bandari Tanzania Bara (TPA) ameahidi kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa michezo katika eneo la Kizimkazi, Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA ameyasema hayo leo katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hakika maendeleo hayana mahali.

Naona hata aibu kusikia.
 
Tungepata kiambatanisho kama clip
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Bandari Tanzania Bara (TPA) ameahidi kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa michezo katika eneo la Kizimkazi, Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA ameyasema hayo leo katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hakika maendeleo hayana mahali.
hivi ingekuwa unyama sana maana inafikirisha cos Bandari ni mambo ya muungano ila wamevuruga cos Zanzibar wana sheria yao ya bandari na wana mkurugenzi wao wa bandari. sasa Mkurugenzi wa TPA tena kusema ataenda kujenga uwanja zanzibar inatafakarisha.
 
Hii tabia ilianza Awamu ya tano

Butiama, Lupaso,Mkuranga na hata Msoga kulikuwa maarufu kwa historia yake sio miradi yake wakati wa tawala za waungwana hao
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Bandari Tanzania Bara (TPA)

Core functions za bandari hazihitaji kujiingiza katika shughuli za kujenga viwanja vya burudani, wajikite kuongeza ufanisi wa kupakua na kupakia mizigo katika bandari.

Bila kutoa tahadhari na angalizo unaweza kusikia pia TPA wameamua kujenga jengo la makao makuu ya bandari Dodoma na kuhamishia watendaji wote Dodoma.

Sheria ya Bandari : The Ports Act No. 17 of 2004 (the Ports Act) is the foundation of the regulation, development, and management of ports in Tanzania. Under this Act, the Tanzania Ports Authority (the TPA) was established as the principal body responsible for managing and delivering services at all ports in the country. The key elements of the Ports Act include: source : Overview
 
Sahihi umedadavua vizuri mno kisomi na kwa lugha rahisi ya hadi mtu wa kawaida kuelewa

Uko sahihi
 
Back
Top Bottom