zwangandaba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2023
- 747
- 1,404
Humu watu wanaongelea ushabiki tu wala hwana elimu ya nini kinaendelea DRC kwa sasa.Una uhakika na ulicho andika mkuu.
Tpdf na majeshi mengine ya MALAWI , SOUTH AFRýKEEPING.
Watz wachache sana wenye uwezo wa kufatilia habari za duniani. Wengi wanapenda ushabiki na ligi.
Kuna mtu mpka leo anakanusha role ya helkopita za south Afrika kwenye kufifisha mashambulizi ya m23 mwaka 2014 na kupelekea m23 kushindwa.
Wapo watanzania mpaka leo hawui key role ya SAMIDC nchini DRC. Eti hawaruhusiwi kupigana kwa sababu wanalinda raia. Unalindaje raia ikiwa huna uwezo wa kumwangamiza adui wa hao raia? Wewe unao walinda raia unapigwa na kuteketezwa vifaa vyako na huna uwezo wa kulipiza.
Wewe unaelinda raia hunauwezo wa kujilinda.
Hakuna kiumbe anaeweza kujiuliza kwa nini SAMIDRC haijawhi kuteka hata cm 1 ya eneo kutoka kwa m23 wakati hao m23 kila kukicha wanateka maeneo kutoka mikononi mwa serikli na washirika wake.
Mara kadhaa mpaka juzi tumesikia m23 wameshambulia vikosi vya FARDC na washirika wake na kutia hasara lakini hatuoni mashambulizi ya maana dhidi ya m23 ama hasara.
Leo Wa south Africa wako kwenye mjadala wa kutaka vikosi vyao viondoke DRC kwani mpaka sasa askari wake 5 wameuwawa na majeruhi takribani askari 40. Wasauzi wanalaumu serikali kwa ukata katika jeshi ikiwamo kukosa uwezo wa kumiliki helkopita za mashambulizi kwa ajili ya kukinga vikosi vyao.
Mwanzoni mwa mwezi wa march m23 walipeleka uwanja wa vita mitambo ya kudungulia ndege aina ya SAM ambayo iliondolewa baada ya kupigiwa kelele sana na UN kuwa iondolewe.
M23 ya leo hakuna wa kuitingisha maana ni bora sana kwa sababu imeimarishwa na RDF ambao wanapigana full scale na kwa siraha za kisasa . Msauzi ambae ndie mwenye nguvu kwenye kikosi cha sadc ameshaona msala hivyo muda wowote anaondoa vikosi maana kelele nyimbani zinazidi kuongezeka.
Akili ya kwida tu jiulize hili swali. M23 ambao wana saidiwa kwa ukaribu na Rwanda wanapigana na majeshi ya serikali yanayosidiwa na Burundi, SADC, Wazakendo,FDNL na mkundi zaidi ya 5 ya wanamgambo lakini bado serikali haitoboi
Nirudie tu kuwambia huwezi kumshinda adui unae mdharau kwa kufuata historia yake ya jana.