TPRB yawaonya wanaofanya shughuli za mipangomiji bila kuzingatia sheria

TPRB yawaonya wanaofanya shughuli za mipangomiji bila kuzingatia sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imewataka wananchi, wadau na wataalam wa mipangomiji nchini kuhakikisha kuwa utekelezaji wa shughuli zote za mipangomiji unazingatia kikamilifu sheria, kanuni na miongozo.
8b57c3b3-05be-42e7-a008-e769ded3a617.jpeg

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB), TP. Martha J. Mkupasi Januari 29, 2026 kupitia taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa kazi za mipangomiji zinazoendelea kutekelezwa nchini.

Kupitia taarifa hiyo, TP. Mkupasi amebainisha kuwa uzingatiaji wa sheria na kanuni unasaidia kuepusha migogoro mbalimbali katika jamii hivyo amewasihi wananchi kuwa makini wanapohitaji huduma za mipangomiji kwa kuhakikisha wanazitafuta kutoka kwa wataalam na kampuni zilizosajiliwa au kupitia mamlaka halali za upangaji, ili kuepuka migogoro ya ardhi na changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye.
97854fe1-dfa0-4122-8cd2-b03323436e35.jpeg

“Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inapenda kuujulisha umma kuwa, shughuli za mipangomiji zinapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya sheria, kanuni na miongozo. Kifungu cha 22, 23, 24 na 25A cha Sheria ya Usajili wa wataalam wa Mipangomiji Sura 426 vinazuia mtu au kampuni isiyosajiliwa na Bodi kujihusisha na kazi za mipangomiji;

“Bodi inawakumbusha wataalamu wa mipangomiji na Kampuni zilizosajiliwa, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ili kutoa huduma bora za mipangomiji kwa Umma” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
2082ea3c-cbc5-44bf-b084-8379c0c34c30.jpeg

Bodi imewataka wananchi na wadau wa mipangomiji kuhakikisha wanapata huduma za mipangomiji kutoka kwa kampuni za mipangomiji na wataalamu waliosajiliwa au mamlaka za upangaji ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi inaendelea kufuatilia kwa karibu kazi zote za mipangomiji zinazotekelezwa nchini, ikiwa ni sehemu ya jukumu lake la kisheria la kusimamia na kudhibiti taaluma ya mipangomiji.

Kaimu Msajili huyo amewataka wote wanaokiuka sheria za mipangomiji kuacha mara moja vitendo hivyo, akisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kutekeleza kazi za mipangomiji kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.
 
Mambo ni mengi hawa wanatokea wapi tena....si wangewasiliana na maofisa mipango miji wa.manispaa,jiji,wilaya yaani kila Kona watu kibao
 
Back
Top Bottom