TRA 2025: Tupeane Mbinu za kufaulu Usaili (Interview) Za TRA

TRA 2025: Tupeane Mbinu za kufaulu Usaili (Interview) Za TRA

Acha waendelee kupeana moyo kwenye hamna wajinga hawa, wanafikiri hii Tanzania ni meritocratic country na wakati nchi inanuka corruption na nepotism kila mahali, na ndio maana ukienda maofisini huko wamejaa wamejaa vilaza watupu na waledi hamna kabisa ila ndio wana enjoy maisha na madharau kibao.
Watu wabishi hawapendi kusikia ukweli, mfano mzuri bungeni, wabunge wamepitishwa bila kupingwa halafu vilaza..!! Na wenye elimu nao wameungana na vilaza limekuwa bunge la kusifu na mapambio.!!

Wanachokifanya hakuna ni kupiga porojo, hata kuwasemea wananchi kero zao hamna.
Wanakula kodi zetu bure na bado wanapitisha miswaada ya hovyo ya kuuza rasilimali za nchi..!!
 
Habarini Wakuu!!!!!!

Kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii. Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania wametoa fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

Fursa ni nyingi kweli na wamegusa fani nyingi tu. Jumla ya nafasi walizotangaza ni 1596.

Kwa hiyo Wakuu kama kuna mtu ana link ya Group ambao wana solve maswali kwa ajili ya kujiandaa na Interview hii naomba uweke link hapo chini ili watu tujumuike wote.

Ushirikiano ni muhimu watu wote watoboe. Cha muhimu kufika kwenye Oral.

Na kama una hints au topic au maswali unajua yataulizwa, tusaidie kuweka chini hapo kwenye comment ili wengi wafaidike.

Shukran.
Unataka maswali ya Interview mbona Bado tunaaapply. Au Interview nilini ili niache kuapply
 
Naomba msaada kila nikijaribu kuji register inaleta huu ujumbe, nimetumia computer na simu vyote sijafanikiwa. Msaada tafadhali.
20250208_152618.jpg
 
1. Fanya Utafiti wa Kina Kuhusu TRA
- Jifunze kuhusu historia, dhamira, malengo, na sera za TRA. Fahamu majukumu ya idara unayofanyiwa usaili na jinsi shirika linavyofanya kazi.
- Tambua mabadiliko yoyote ya hivi karibuni au sera mpya, hasa yale yanayohusiana na TRA 2025, ili uweze kuzungumzia mambo ya sasa.

2. Elewa Nafasi Unayoiomba
- Soma maelezo ya kazi kwa uangalifu ili kuelewa mahitaji, ujuzi na sifa wanazotafuta.
- Jiandae kuelezea jinsi uzoefu wako, elimu yako, na ujuzi wako unavyolingana na mahitaji ya nafasi hiyo.

3. Andaa Majibu kwa Maswali ya Kawaida ya Usaili
- Tafakari maswali kama “Ni nini unajua kuhusu TRA?”, “Kwa nini unataka kufanya kazi hapa?”, “Ni changamoto gani unazoweza kukabiliana nazo katika nafasi hii?” na “Umeweza vipi kukabiliana na changamoto katika kazi zako za awali?”
- Tumia mifano halisi ya mafanikio yako na jinsi ulivyoweza kushughulikia matatizo kazini.

4. Ongeza Ujuzi wa Msingi wa Kitaalamu
- Kama nafasi unayoiomba inahusisha elimu ya sheria za ushuru, hesabu au usimamizi wa rasilimali, hakikisha umejifunza misingi ya mada husika.
- Angalia kama kuna vipimo vya kitaaluma au mafunzo maalum yanayoweza kukusaidia kujitayarisha kwa majukumu ya nafasi hiyo.

5. Mazoezi ya Usaili
- Fanya mazoezi ya kujibu maswali ya usaili na rafiki, mwajiri wa awali, au kupitia video ili kuongeza kujiamini.
- Jifunze kutumia lugha ya mwili inayoonyesha utulivu na kujiamini, kama vile kuangalia jambo kwa undani, tabasamu la kujali, na kuweka msimamo mzuri.

6. Mavazi na Matarajio ya Kitaalamu
- Hakikisha unavaa mavazi yanayofaa kwa usaili. Mavazi safi, ya kisasa na ya kitaalamu huonyesha uzito wa tukio hilo.
- Jiandae kufika kwa wakati na kuwa na nakala za wasifu (CV), barua ya ombi, na hati nyingine muhimu.

7. Kujiandaa Kujulisha Maswali
- Kuwa na maswali yako mwenyewe kuhusu utamaduni wa kazi, maendeleo ya shirika, fursa za mafunzo na maendeleo ya taaluma ndani ya TRA.
- Maswali haya yanaonyesha kuwa umefanya utafiti na una nia ya kweli ya kujifunza zaidi kuhusu shirika.

8. Dhibiti Hisia na Wasiwasi
- Fanya mazoezi ya kupumua kwa kina na tafakari kabla ya kuingia kwenye usaili ili kupunguza wasiwasi.
- Kumbuka kuwa usaili ni mazungumzo; lengo ni kuonyesha uwezo wako na kujifunza kuhusu nafasi hiyo pia.

9. Fuata Miongozo ya Mawasiliano
- Jifunze kusikiliza maswali kwa makini kabla ya kujibu. Usikimbilie, bali toa majibu yenye muundo, na hakikisha unaelezea wazi malengo yako na jinsi utakavyosaidia TRA kufikia malengo yake.

Kwa kufuata vidokezo hivi, utakuwa umejiandaa vizuri na kuongeza nafasi yako ya kufanikiwa katika usaili wa TRA 2025. Kumbuka, mazoezi na utafiti wa kina ni ufunguo wa kujiamini na kuonyesha ufanisi wako.

Ova
Asante mkuu kwa hizi hints, naamini zitatusaidia huko mbeleni.
 
Mkuu hapoo n MAOMBIII tyu

MWAKA Jana nilikuwa na shemejio WA Uganda pale sinzaa hotel Moja

Wakati nakula lunch jamaa MMOJA PEMBEN anaelekezwa jinsi ya kujibu hayo maswali ya tra na interview keshoyake na hadi calculations.,naamini jamaa Yuko kazini kwa sasa...ningejua ningechukia namba yake ingawa jamaa alikuwa kama anauwoga pemben nani baadae WAKAHAMIA mezan ya mbali
Pepa zote hata za utumishi watu lazima wawe na maswali na majibu, kuwapata au kuwajua ndo changamoto hiyo.
 
Naomba msaada kila nikijaribu kuji register inaleta huu ujumbe, nimetumia computer na simu vyote sijafanikiwa. Msaada tafadhali. View attachment 3229165
Hatua za Kuchukua
  • Jaribu tena baada ya muda.
  • Hakikisha unaunganishwa kwa mtandao wa kasi.
  • Tumia browser tofauti.
  • Futa cache na cookies kwenye browser yako.
  • Angalia kama kuna taarifa rasmi kutoka kwa TRA kuhusu matatizo ya mfumo.
Ikiwa shida inaendelea, wasiliana na msaada wa kiufundi wa TRA kwa msaada zaidi. Unaweza kufikia msaada wao kupitia:
  • Barua pepe: support@tra.go.tz
  • Namba ya simu: +255 22 219 9200
  • Mitandao ya kijamii: Angalia kurasa zao rasmi za Facebook au Twitter kwa maelekezo zaidi.
Natumai hii itakusaidia kutatua tatizo lako

Ova
 
Asiwakatishe mtu tamaa wewe nenda fanya mtihani muombe Mungu utapata wapo watu kibao wamepata hawana ndugu wala cha connection tena wameingia ile ya majuzi hapo,jifue kweli kweli kapige paper then piga oral unatusua tuu.
 
Hatua za Kuchukua
  • Jaribu tena baada ya muda.
  • Hakikisha unaunganishwa kwa mtandao wa kasi.
  • Tumia browser tofauti.
  • Futa cache na cookies kwenye browser yako.
  • Angalia kama kuna taarifa rasmi kutoka kwa TRA kuhusu matatizo ya mfumo.
Ikiwa shida inaendelea, wasiliana na msaada wa kiufundi wa TRA kwa msaada zaidi. Unaweza kufikia msaada wao kupitia:
  • Barua pepe: support@tra.go.tz
  • Namba ya simu: +255 22 219 9200
  • Mitandao ya kijamii: Angalia kurasa zao rasmi za Facebook au Twitter kwa maelekezo zaidi.
Natumai hii itakusaidia kutatua tatizo lako

Ova
Asante kwa maelekezo, nimejaribu njia zote mpaka kubadili browser lakini sijafanikiwa. Mpaka nikasema nijaribu usiku mwingi pengine itakua watu wamepungua shida ni hiyo hiyo.

Nadhani msaada wa mwisho ni kuwasiliana nao kama ulivyoshauri.
 
Back
Top Bottom