TRA, hii imekaaje? Gari ya 2022 na usajili wa miaka ya 2005?

TRA, hii imekaaje? Gari ya 2022 na usajili wa miaka ya 2005?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
20221107_160554.jpg
20221108_064901.jpg

Mitaani kuna vituko vingi.

Kuna magari ya wasiyojulikana wengi tu sasa hivi, lakini hii ni kiboko. Gari T140ALF ina usajili wa karibia miaka 20 nyuma kwa gari iliyotengenezwa 2022, LC300 Landcruiser New model.

Inakuwaje hapo?
 
Ukiona hivyo usilisogelee, kaa mbali, hata traffic akiliona analiacha lipite mbali nae.

Alafu ww shida yako ni maji, umeme, hospitali upate huduma nzuri, shule, barabara nzuri, kuwe na amani na usalama unapoishi, gharama za maisha zisipande sana na huduma nyingine muhimu za jamii, sio unakuwa busy kuangalia plate numbers za magari barabarani, ushaingilia mambo ambayo hayakuhusu kabisa, hadi hapo ushaharibu, watakusaka shauri yako.

Mambo mengine ukiona yasiokuhusu achana nayo, piga kimya utaishi vizuri sana duniani.
 
Ukiona hivyo usilisogelee, kaa mbali, hata traffic akiliona analiacha lipe mbali nae.

Alafu ww shida yako ni maji, umeme, hospitali upate huduma nzuri, shule, barabara nzuri, kuwe na amani na usalama unapoishi, gharama za maisha zisipande sana na huduma nyingine muhimu za jamii, sio unakuwa busy kungalia plate numbers za magari barabarani, ushaingilia mambo ambayo hayakuhusu kabisa, hadi hapo ushaharibu, watakusaka shauri yako.

Mambo mengine ukiona yasiokuhusu achana nayo, piga kimya utaishi vizuri sana duniani.
Mkuu hili taifa letu na tusiishi kwa woga.
Na mlinzi no. 1 wa taifa hili ni mtanzania mwenyewe na kila mzalendo.
Soma ahadi za chama utanielewa.
Tukiona kitu kisicho cha kawaida mitaani lazima tuweke wazi.
Kama mnafikiri hawa ni wana usalama basi concealment na blending na public hapo ni sifuri.
Ni kama ngamia aliyezika kichwa mchangani huku mwili wote unaonekana, na watu wakajua huyu ni ngamia.
There must be a better way.
 
Angalia hiyo plate number imechomekwa tu haijafungwa.. Hayo ni magari ya usalama hayana registration maalum
Du na usalama huu ni wa nani?,wale wateule wachache wanaobugia pie yetu au wa mlala hoi?maana nchi imekua kichaka cha mafisadi na Ile tiss real imepotolea wapi?,ilikua inatuletea viongozi Safi waliokua vetted vema, hii ya sasa...ngoja ni makapukapu tu
 
ukiliona linakufwatilia we jisalimishe tuuu ama uwahi kituo cha polisi
Mkuu hata ukienda polisi haisaidii...

Hao watakufuata huko huko polisi watakuchomoa tena bila hata maelezo
Dawa ni kujisalimisha na kutii maelekezo yao..

Kipindi cha nyuma ukisikia watu ambao hawafahamiki basi jua ndio hao..
Kuna trafiki alisimamisha gari yenye plate number dizain hii kwa kosa la kuzidisha spidi zaidi ya 50 kwenye eneo flani.. Akawa anakomaa kuandika faini.. Sasa number za gari hazipo kwenye system ya TRA.. Jamaa kwa upole kabisa anamwambia trafiki andika tuu faini..
Trafiki mwenzake akamstua achana na hilo gari.. Hao ni watu wasiojulikana
 
Hahaa anapekenyua sana.kwanza yey ana shid gan na namba za magar.yey ni trafik?
Vitu vingine awe anaacha haina maana ya kuleta uzi.siwez kuelezea zaidi
Kizazi cha uoga wa mbwa koko, kipindi cha awamu ya kwanza kila raia alikua ni first line of defence wa nchi, kitu kisicho Sawa lazima unawataarifu wahusika, scout mwenzangu pale ilipokua kituo cha station, kwa mbele kulikua na petrol station, 'tourist 'alipotea njia na kumuuliza huyu rafiki yangu njia ya kwenda Kilomanjaro Hotel, rafiki yangu akamwelekeza akaulize lile jumba Jeupe lililo sambamba na kituo cha station, old school humu watalitambua lile jumba!,TISS ili EARN RESPECT kwa raia, hawajawahi kuwa tainted na mateso kwa raia, walikua very smart hawa jamaa
 
Du na usalama huu ni wa nani?,wale wateule wachache wanaobugia pie yetu au wa mlala hoi?maana nchi imekua kichaka cha mafisadi na Ile tiss real imepotolea wapi?,ilikua inatuletea viongozi Safi waliokua vetted vema, hii ya sasa...ngoja ni makapukapu tu
Asante mkuu kwa kuiona point.
TISS tunaowajua wanatakiwa kuwa smart na Intellingent, na ndio maana kuna kitu kinaitwa inteligensia.
Na wanatakiwa kuwa intelligent katika kila kinachofanyika.

Hii kujiweka wazi na kuamsha interest za hata wasiojua , that is definately not smart.
 
Back
Top Bottom