TANZIA TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024

TANZIA TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024

View attachment 3170823
=============

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inasikitika na kutoa pole kwa familia na ndugu na jamaa kutokana na kifo cha mtumishi wetu wa TRA, Bw. AMANI Kamguna Simbayao kilichotokea leo mchana wa tarehe 06 Desemba 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa baada ya tukio la shambolic akiwa katika majikumu yake ya kikazi kwa maslahi ya Taifa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar Es Salaam. Tunatarajia wahusika wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Dah so sad
 
Waliofanya huo uhuni ndo watajua huwa ni Polisi kweli au Policcm. Watasakwa kila kona na kufikishwa mahakamani. Na wakileta ubishi tutasikia "Marehemu alikuwa akikataa amri halali ya polisi ikabidi zitumike risasi za moto"...
PoliCCM hao hapo poneaponea uwe na kadi ya Chama A uwe nayo ndio unaachwa
 
wao hawakupaswa kumvizia mt kwa stail ya watekaji, watz wangeamin vp kam n TRA? wakt mtaan kunamatukio ya kikatili yanaendlea? polen familia ila nadhan watz tmeanz kuamka sasa
Wewe una uhakika gani kama ni TRA kweli, can't you read between lines?
These dudes are spin masters, the whole shit is just being twisted.
Ni walewale 'wasiojulikana'.
 
I see, namfahamu huyu kijana ..alipita SUA Morogoro..baadae nikawa namuona na magari ya maji ya Kilimanjaro..nadhani alikuwa upande wa Sales.tukapotezana kipindi..dah alikuwa mtu mstaarabu na mpiganaji.. Lala salama Simbayaooo! ..tutaonana asubuhi iliyo njema
Dah kumbe msuaso.R.I.P bro maana kuingia TRA ni kazi
 
Hii ni kusudi tu

Watekaji wanajulikana ila wakija kila mtu anaufyata mfano yule Bonge alipiga kelele hakuna aliyejitokeza, kwa kibao hakuna aliejitokeza

Kwa Nondo tena kweupe kabisa hakuna aliethubutu hata kufungua mdomo

Leo hii mnajua kabisa hawa ni tra mnaamua kuwakomesha

Sasa rungu liwafikie wote waliohusika

Maana wanaokuja na bangili mkiwaona mnakaa kimya, hawa tofauti mnajifanya vifua mbele

Shenz type

I couldn't said it any better. Wanaua wanaowaweza tu shenzi.
 
Nchi zenye halafu ya ujamaa hizi zina mambo mengi, usikute hata sio TRA ni haohao wasiojulikana - taasisi imeamshiwa zigo.
Anyway..vijana muwe na uelevu..someni alama za nyakati - mtakufa nafasi zenu wataajiriwa wengine na ndani ya siku 2 - the state will forget about you - your children, parents, ndugu watabaki na majonzi milele - wengine watakusahau the moment umefukiwa.
Msijitafutie ushujaa wa kijinga - waachieni police wafanye kazi zao za ukamataji - wewe kalale na mkeo na watoto wako.
Halafu kwa hali ya sasa - na taharuki ya utekaji unapata wapi ujasiri wa kufanya vile - tena kwa haya magari yenye sifa ya kuteka , katika eneo ambalo juzijuzi tu mtu katekwa na kuuawa - Mzee Kibao. Dont be stupid
 
Hao wakwepa kodi ni wajinga na wapuuzi, wanataka kufanya biashara bila kulipa kodi, itakuwa sasa wanakimbiakimbia kujificha kutokana na tukio lao la kishenzi. Nchi hii ina wafanyabiashara wengi wasiokuwa na elimu na matokeo yake ndio haya
 
Kwanza kuzuwia na kushambulia wafanyakazi wa taasisi za serikali ili wasifanye kazi zao ni makosa makubwa sana. Waliotenda kosa hilo mpaka wakasababisha kifo cha mfanyakazi huyo wasakwe popote walipo na wafikishwe mahakamani kujibu mashitaka ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo
 
Hawa TRA kuna mda mwingine wanajisahau kuna kipindi walikuja ofisin kwangu saa sita usiku na bukta za kulalia et ni TRA wanataka kunikagua washukuru mungu nilikuwa na ustaarabu flan lakn kwa mazingira ya kawaida unaeza wakataa na Kuwaitia wez
 
Kwanza kuzuwia na kushambulia wafanyakazi wa taasisi za serikali ili wasifanye kazi zao ni makosa makubwa sana. Waliotenda kosa hilo mpaka wakasababisha kifo cha mfanyakazi huyo wasakwe popote walipo na wafikishwe mahakamani kujibu mashitaka ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo
Usilolijua kaka kama ucku wa giza unaeza kuta walifos walitaka ela jamaa akaamua kuwatia kiberit
 
Usilolijua kaka kama ucku wa giza unaeza kuta walifos walitaka ela jamaa akaamua kuwatia kiberit
purukushani na hao wafanyakazi wa taasisi za umma kama polisi, takukuru na tra bila kuawaacha wale wa maliasili, usipoelewana nao vema vurugu hutokea. All in all hao wafanyakazi ni wa kuogopwa hata kama wanafanya corrupt, huwezi kushindana nao kibabe, wale ni kuwaripoti kwa mamlaka za juu yao kama wanafanya corrupt
 
Back
Top Bottom