DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwahiyo maendeleo ya watu hupimwa Kwa Wing wa magari?

Kodi ya magari ni sehemu ya kodi za kipumbavu za bidhaa zilivo kubwa ambazo hupachikwa na viongozi wajinga wenye mawazo ya kipumbavu ambao hawamsaidia mtanzania bali kumdidimiza kila wakati
 
Ukipita mitaa ya Livingstone na Lindi Kariakoo utaumia jinsi wa Kongo wanavyopaki benz za kibabe zenye usajili wa kongo

Wale acha wale maisha unajua kuna wakati viongozi wanajisifu na blah blah za amani na utulivu wakati walitakiwa kuwasifu watanzania kwa kua mazuzu na wapole maana kuna vitu mtanzania anafanyiwa na kuonewa bila sababu yoyote
 
BANDARI IKO TANZANIA BIDHAA ZOTE BEI JUU SABABU YA KODI KUBWA, WANAONUFAIKA NA BANDARI NI MAJIRANI ZETU NA SIO WATANZANIA HUU NI UKWELI MCHUNGU.
 
Watanzania walirithi kila kitu madini aina karibu zote, bandari, ardhi yenye rutba, kiswahili, mbuga za wanyama, fukwe za maziwa na bahari, mito mikubwa, lakini watanzania wanaishi maisha magumu kupita maelezo, miaka 61 ya uhuru hadi leo Tanzania haijapata kiongozi wa mageuzi ya kiuchumi
 
Kodi ya magari ni sehemu ya kodi za kipumbavu za bidhaa zilivo kubwa ambazo hupachikwa na viongozi wajinga wenye mawazo ya kipumbavu ambao hawamsaidia mtanzania bali kumdidimiza kila wakati
Kujenga nchi lazima upate maumivu makali
 
Bandari mali yetu, nchi iko kwenye geografia nzuri lakini hatunufaiki na kwa kifupi hadi majirani hutushangaa kwa nini hatuko mbele yao kiuchumi wakati tuna kila kitu,
Kabisa,wazambia wanatumia magari mazuri kuliko sisi

Ova
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Angeona la kwangu la mwaka 2000 ndo angezimia...
Yaani hilo langu la 2002 huko Lusaka si nitaonekana kituko mimi, hivi nyie TRA mbona hivyo lakini, gari ni kitendea kazi cha kuinua uchumi wa taifa letu, sio anasa!!
 
Ubunifu zero wa viongozi, maisha yanatakiwa kua rahisi na sio kufanya ugumu wa maisha
Hawajui kwamba gari zikiwa nyingi them ile multiplier effect ya kutumia mafuta mengi zaidi, shughuli nyingi zaidi za kiuchumi nk. nk zitawawezeshabkukusanya kodi kubwa zaidi ya hiyo wanayoitaka na kukuza uchumi kwa kasi zaidi, hivyo wataweza kuongeza idadi na ubora wa barabara zilizopo, ni akili ndogo tu
 
Sikupinga kwa kua nna uwezo wa kununua jipya, nna gari ya mwaka 2001 nna miaka 12 hadi sasa hivi nipo nayo na sijabadili injini pia, lkn ukweli unabaki tunanunua gari zilizotumika sanaaa, km 150000 sio mchezo mkuu.
 
Serikali isiojali muda
 

Hawajui hayo na ma phd yao ya kubumba! Mindset ni tozo driven!
 
Nikiwa Nairobi nilikaza macho sana sikuona Noah ist carina sijui Masienta porte sijui midude gani michakavu ni ndinga za maana tu ziko barabarani kama hujaenda nchi za jirani congo drc hasa lubumbashi Lusaka Nairobi huwezi jua kinachoendelea kifupi bongo ukiacha maviete ya govt gari nyingine ni mikweche tu kwa hili usiniambie sina uzalendo unaendesha gari ya 2002 kweli huzuni sana
 
Kuagiza magari machakavu yanatesa sana kilasiku kwa fundi unapoteza pesa kwenye spea in fact nchi inageuka kijiwe cha wahunzi inaleta shida sana hebu hili nalo wabunge waliangalie tumechoka kuwa wahunzi wajameni .
 
Mtu anawaza Tanzania kwa jicho la Dar wakati kuna watanzania wako maji moto, wana uwezo wa kununua magari kodi ikiwa himilivu na magari hayo yakawasaidia kukuza uchumi wao
Exactly [emoji1666] [emoji1666] mkuuu
 
Kama ndio hivyo, wengi tunatia huruma hapa bongo
 
Nunua gari mpya ufurahie unafuu wa kodi
 
Bandari Kuwepo Tanzania haimsaidii nafuu ya maisha mtanzania, kila bidhaa iko juu viongozi sio wabunifu wapo wapo tu.
wajanja wanavusha hadi Zambia kabla haijawa registered inarudi tena Dar like imetumika Zambia. u save kama 50-100% ya ushuru ambao ungelipa hapa kwa TRA. hii yote kwa sababu wanaamini kodi kubwa ndo suruhu ili hali kodi kubwa ndo inaleta mianya ya kukwepa kodi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…