DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kodi ni moja ya tools zitumiwazo na walamba asali kuwafanya wananchi wawe masikini japo kwa macho ya kawaida uact wanapambana kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Hii depreciation according to age ni wizi mtupu eti una discourage dumping hii principal ilikuwa na maana kipindi kile Hakuna mambo ya recycling chuma chakavu
 
Watanzania wanaenda kununua magari waliyotumia wazambia na Malawi kwa sababu yaliingia kwa kodi ndogo hata wakiuza yatauzwa kwa bei nafuu na yeye anaagiza lingine anakuachia chakavu ambalo Tanzania litaonekana ni jipya ndio maana tupo busy na Fusso sijui Tandamu ni kwa sababu ya kodi gari tani 4 ila linabeba mzigo mpaka tani 15 harafu tunasema yana matatizo ya breki...wenzetu wapo na International na aina zingine za Truck na kwa ukubwa wake zinatunza vizuri bara bara sisi tumejikita na pick up na kuziita truck kisa kodi kubwa..imefikia Watanzania eti ukimwambia chukua Scania anasita anataka Fusso wakati ni vitu viwili tofauti kabisa..
Sasa ataweza kulipa ushuru wa Scania? Zambia taxing system yao iko very friendly ndiyo maana mafuta ya magari ambayo hushukia bandarini kwetu bado kwao bei ni ya chini. Pale Tunduma sukari from Zambia kilo moja (well packaged) ni sh 2000 tuu, vitenge pia bei poa sanaa..
 
Kama una uwezo basi usilalamike. Ila hatuwez kuruhusu Kila mtu kumiliki magari Kumi lazima yawe machache wengine watumie usafiri wa umma.
'Huwezi ruhusu' kama nani?

Nyie ndo mnapanga uhai wa mtu?

Kodi zenu ni za kipumbavu, mnaishia kuwalazimisha watu walete magari yaliyochoka badala ya kuleta magari mazuri.

Huo usafiri wa umma unaouongelea utadhani ni kama Switzerland, kumbe ni nchi masikini wanakimbizana na DCM zinazokaribia kufa.

Huna efficient public transport mpaka watu wauone ni mzuri, ni bora liende watu wakatafute mkate wa kila siku.

Ukiwa na viongozi wenye chimbuko la umasikini na kukosa exposure hayo ndo matokeo.

Wewe ni mfano wa aina ya viongozi tanzania wapo. Wabunge wenyewe hawana utofauti na waliopewa degree kwa kuvuliwa chupi. Hopeless kabisa.
 
Kwani hapa kuna ligi ya wavijijini na wa mjini...? Here we are discussing kuhusu kodi za kuingiza gari nchini. Ili tupate unafuu. Na waliomo humu sio kwamba ni wa mjini tu boss
Kuna hoja kwamba bila kuweka kodi ya juu eti magari yatakuwa meengiii kuzidi uwezo wa barabara... Ndiyo nikasema watanzania siyo mijini tuuu bali hata huko vijijini ambako ndiyo waliko wengi...
 
Nenda kaulize Kenya [emoji1139] kodi yake alafu urudi hapa!
Ndio maana Kenya hamna magari ya kifahari mengi!
Siyo kweli, kuna clip ya Chris Lukosi kule Facebook akionyesha kwamba kwa nchi za East Africa Kenya ndio wanaongoza kwa kununua gari kalii na za bei mbaya..
 
Wangeruhusu tu magari yaingie free tungepata pesa nyingi Sana kuliko kutukamua kwenye Tozo, mbona vyanzo ni vingi tu.
Ukiondoa import duty utapata makusanyo mengi sana kwa mda wa miaka 20 kupitia mafuta, parking, spare parts, fine, bima, nk ni suala tu la hesabu.
 
Kwa mabilion yanayochezewa wangejikakamua wakajenga express ways hata 4 za inter regions watu wangepita kwa kulipia tolls, mfano DSM-Tunduma ambayo inachukua gari private na baadhi za biashara kama mabasi. Ukiweka 30,000 kwa basi kubwa 20,000 kwa coaster na 10,000 kwa rest of the cars za binafsi kwa siku wangekuwa wanakusanya hela nyingi sana.

Sasa wao mikopo, madarasa na vyoo, zahanati vitu ambavyo vinakuwa liability kwa asilimia 100%
Kwa barabara za kulipia tu serikali ingeweza ingiza zaidi ya bil 100 kwa mwaka...
Maana yake ndani ya miaka 10 inakuwa ishajilipa
Sioni sababu ya kutumia masaa 14 kufika Tunduma, wakati barabara zikiwa sawa, unaweza tumia masaa 10 tu.

Umeokoa mafuta
Vifo
Muda
Ajali
 
'Huwezi ruhusu' kama nani?

Nyie ndo mnapanga uhai wa mtu?

Kodi zenu ni za kipumbavu, mnaishia kuwalazimisha watu walete magari yaliyochoka badala ya kuleta magari mazuri.

Huo usafiri wa umma unaouongelea utadhani ni kama Switzerland, kumbe ni nchi masikini wanakimbizana na DCM zinazokaribia kufa.

Huna efficient public transport mpaka watu wauone ni mzuri, ni bora liende watu wakatafute mkate wa kila siku.

Ukiwa na viongozi wenye chimbuko la umasikini na kukosa exposure hayo ndo matokeo.

Wewe ni mfano wa aina ya viongozi tanzania wapo. Wabunge wenyewe hawana utofauti na waliopewa degree kwa kuvuliwa chupi. Hopeless kabisa.
Na hakuna kitu mutaweza kutufanya.
 
Ubunifu katika kukusanya kodi hakuna ndio maana kunakua na mlundikano wa kodi kwenye kitu kimoja
Hivi wanashindwa hata kufanya competition kwa wananchi kupeleka their ideas/proposals kuhusu Kodi mpya rafiki halafu anayeshinda wanamlipa??
 
Hiv mkuu ukiwa nchi jirani ukanunua gari ukiwa huko hv kulileta hapa kwetu Kuna usumbufu tena ama huwa inakuwaje?
Usumbufu ni ule ule tuu mkuu maana si lazima usajili hilo gari lako? Yaani shida iko pale pale
 
Kodi inawekwa Kubwa Ili kupunguza idadi ya waagizaji magari. Kodi Ikiwa chini Kila mtu atanunua gar na itakuwa fujo. Mfano nchi ya Vietnam usafiri wao mkubwa ni pikipiki maana gar yoyote utakayonunua Kodi yake Kwa TSH n 80M.

Hivyo wanaotumia magari ni ni kama anasa tu.

Hata watumishi wengi wa serikali huko Vietnam wanaotumia pikipiki.

TRA Wako sahihi
Fikra na akili za kimasikini

Gari si ufahari

Gari zikiwa nyingi mafuta yatatumika mwngi na serikali itapata faida
 
Kodi inawekwa Kubwa Ili kupunguza idadi ya waagizaji magari. Kodi Ikiwa chini Kila mtu atanunua gar na itakuwa fujo. Mfano nchi ya Vietnam usafiri wao mkubwa ni pikipiki maana gar yoyote utakayonunua Kodi yake Kwa TSH n 80M.

Hivyo wanaotumia magari ni ni kama anasa tu.

Hata watumishi wengi wa serikali huko Vietnam wanaotumia pikipiki.

TRA Wako sahihi
Narudia tena, hii hoja ni kindezi sana.. Watanzania milioni 60 wanaishi huko Dar au mijini?? Ukubwa wa hii nchi ni zaidi ya hekta milioni 95... Zaidi ya watanzania 90% wanaishi vijijini huko Likawage, Nanjirinji, Nakapanya, Nanyumbu, Ikubulu, Lubalisi, Lunenzi, Chabima, Mwese, Lwega na kwingineko. Je wao huko vijijini hawana haki ya kumiliki magari?? Maendeleo ni pamoja na kaya nyingi kumiliki gari kwa maendeleo yao, gari ni kitendea kazi na siyo anasa... acha ulofa jombaaa
 
Back
Top Bottom