Mburia
JF-Expert Member
- Jul 15, 2022
- 2,369
- 3,488
Pumba tuuu, nimenunua gari limetembea 150,000 km 7 years ago na mpaka leo sijawahi kugusa engine.. Sana sana nabadili engine oil, filter, brake shoes, matairi etc... Juzi juzi jamaa gari yake ilipiga short na kuwaka moto na yote kuteketea... Yaani ndani ya masaa 2 yote imeuzwa scraper na hakuna kilichobaki... Narudia uwezo wa kubuni kodi mbadala hawana na wameshindwa... Tukete tax consultant kutoka hukooo kwa wenzetu waliofanikiwa...Umeanza vizuri umemaliza vibaya,
Nikukumbushe tu tozo alianza kutuwekea magufuli sh 100 kwa kila lita 1 ya mafuta ya taa, disel na petrol na na baadae ikawa 200, unanunua mafuta ya taa kwa ajili ya kujimulikia na familia yako lkn unamlipia na kodi mwenye gari, hii ndio ilitakiwa kukemea vikali sana lkn kwa kua kuna watu waliamini magu hua hakosei na hana baya ikitokea kakosea au kafanya baya unarudi kwenye kanuni ileile kua magu hua hakosei ndio maana hamkupiga kelele kuhusu hii tozo, wenye magari halipii tena kodi gari yake ila wamemuwekea kwenye mafuta ila tunasahau mafuta sio kwa ajili ya magari tu....
Kwa kua hamkuona baya kwa magu nami naungana na mama kua anaendelea alipoishia magu na kudumisha alivyovianzisha na kuviboresha ikiwa na pamoja na tozo. Ila tuwe wapole tu
Kuhusu kodi za magari wengi humu hawana uelewa, mtu unaagiza gari ya mwaka 2013 now tupo 2022 na ilishatumika ina km laki na ushee huko yaani tunaleta skrepa huku kwetu afu watuwekee kodi ndogo? Hata watoto wetu wa o level wangeenda shule kila mmoja na gari yake, ile kodi ya uchakavu ndio hua ni kubwa nenda kaagize gari mpya kabisaaa uone kodi zake zipoje ndio urudi hapa kuja kuilaumu serikali.
Hivi mshajiuliza gari umeitumia miaka 10 na ushee afu unamuuzia mtu hiyo itakua gari au skrepa?