DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Narudia kuandika tena,

Ifikie hatua muwe waelewa huwezi kujifanya una calculator ya kodi kwenye magari ambapo kodi yenyewe unatoza asilimia 80% hadi 100% ya manunuzi hii sio sawa.

Kwa mikodi yenu mikubwa ndio maana hamuwezi mkawa na walipa kodi wengi.

Mkumbuke kodi kubwa inawafanya kuathiri biashara ya mafuta kwa ujumla, biashara ya vipuri.

Hakuna sababu ya kodi asilimia 80 hadi 100 wakati ndani ya nchi hatuna uzalishaji wa magari au viwanda vya magari hakuna na kodi inakua ya kuumiza sio sawa.

Kweli mtanzania anunue gari dola 5000 kodi apigwe dola 4000 hadi 5000 halafu mtakuja na formular zenu za ajabu ajabu aibu sana hii.

Uchumi hauwezi ukakua kwa mtindo huo muelewe magari ni kifaa au chombo kinachorahisisha kuinua uchumi kwa namna moja au nyingine.

* Bandari Kuwepo Tanzania haimsaidii nafuu ya maisha mtanzania, kila bidhaa iko juu viongozi sio wabunifu wapo wapo tu.
Ukiongea sana utaambiwa kama hutaki kanunue baiskeli
 
Inasikitisha SANA. Watanzania tunaishi kama mashetani yani...Ukiwa Tunduma unashuhudia lundo la gari nzuri nzuri za aina tofauti tofauti na hizi yebo yebo zetu tulizozizoea kuziona hapa bongo zikivuka boda kwenda nchi jirani.
Hiv mkuu ukiwa nchi jirani ukanunua gari ukiwa huko hv kulileta hapa kwetu Kuna usumbufu tena ama huwa inakuwaje?
 
Ndo maana nchi yetu ina magari used na machakavu kila kona...na ajali haziishi...
Kwa sababu watu hawawezi kuingiza magari mapya
Harafu Polisi ikitokea ajali wao wanakimbilia kusema chanzo ilikua mwendo kasi kumbe magari ni chakavu tuu haya na hili hawawezi kulisema kwa kuwa wao ndio chanzo...na hawawezi kushauri kwa zile gari za nje hao trafiki watakagua nini kila saa si itakua salamu tu na wao wanapenda raia wakiendesha gari chakavu ili wapate utumbo..
 
Tushushe kodi halafu tupige ban kuagiza gari juu ya miaka 5. Ila tukishusha kodi halafu tukaacha kama jinsi ilivyo, miundombinu hautamudu kuhimili wingi wa magari.
Sasa miundo mbinu si ndo jukumu la serikali kujenga na kutengeneza sasa fikiria kama sasa hivi kodi za magari zipo juu na hio miundo mbinu ni mibovu yani huwezi hata kufurahia gari iliochini
 
Sasa miundo mbinu si ndo jukumu la serikali kujenga na kutengeneza sasa fikiria kama sasa hivi kodi za magari zipo juu na hio miundo mbinu ni mibovu yani huwezi hata kufurahia gari iliochini
Hili ni tatizo sugu boss.
 
Mie naweza nikaongea lugha nyingine ya kitalaamu kuwa why Kodi kubwa. Inawezakana serikali Ina discourage private ownership ya vehicles ,why Ina discourage?

Sababu ya barabara aka level of services like A,B,C,D,E and F. Sasa uwezo wa serikali kujenga road Kama ya kiwango Cha LoS A Ni gharama mno yaani mno kwanza hatuna uwezo.

Wakiweks ushuru chini gari zitajazana road mno itapelekea tutakuwa na LoS E or F ambayo utakuwa unasafiri hata km 200 kwa saa nne badala ya mbili ama tatu.

Kuna namna ya watu husika ama mamlaka ku discourage kila nzi kumiliki gari like kuanzisha toll roads, high parking fees, muda huo huo inatakiwa public transportation iwe nzuri kinyama ndicho inachojitahidi kwa DART sema Naona wanashindwa Mana bado Ni karaha kwa wwsafiri.
Hebu waza gari moja inabeba watu mbili na je hao Mia mbili kila mmoja angekuwa na gari lake huko road kungekuwaje.

Nchi yetu ama zetu unapoambiwa Ni masikini Ni ukweli Mana ukitaka ushuru uwe chini mno hata 20% ya Bei uliyonunulia.

Inatakiwa tuwe mpaka na njia nane ama multi lanes roads, hii road unajua inaweza jengwa kwa Bei gani tutajiuza mpaka sie utumwani ndipo tujenge hii roads Mana madini Kuna watu wanakula perse mpaka vizazi vyao. Labda magufuli angeipokea nchi tokea kwa nyerere akomae na mwendo ule ule nchi iwe na hela na akae madarakani mpaka muda huu yaani zaidi ya miaka 50 ndipo tungeweza Ila kwa Hali hii bwawa linacheleweshwa ili watu wauze gesi zao Mana Wana hisa sio leo tusubirie kwanza.

Na tumeambiwa kuwa kuni na mkaa unaleta mapafu homa sijui Nini tutumie gesi ili kuwanenepesha akaunti zao,yaani we are like fodders to feed their bank accounts for their incoming generation.

Wakati miaka takribani Bilioni na mabilioni binadamu amekuwa alitumia kuni na mkaa.

Ila Sasa huyu kisa kiongozi anajua kuwa tunamuona Kama Mungu ana akili Sana kuliko yeyote. Kuna muda tajiri anawaza kuwa masikini Hana akili kabisa kisa ya yeye kumiliki pesa Ila sio wote lakini yaani Kuna watu wale wenye dharau.

Samahani kwa kuwachanganyia maada jamani tozo zimetuvuruga kinyama yaani huyu maza inabidi nimtumie maza alfu kumi kwa Basi Mana kwa tozo atapokea Kama alfu tano ya kutuma na kutolea.

Mana mchumia tumbo degree 12 Hana uwezo wa kuzalisha vyanzo vya uchumi ama uwekezeji ili akusanye Kodi Bali anacheki Ni wapi pa kukwapua huyu asiwe nacho kabisa.

Kama sio kuwa wanatengeneza tatizo halafu wanalitatua ili watt wamkubali baba na mama kuwa wako nondo I don't know.
Kama walivyoua reli ya Arusha wakaja wakaifufua wakajisifu kwa wananchi kuwa Ni wajanja nipeni mrija nizidi kuwannyonya damu mbakie skeletons...

I am lost
Hili niliwahi lisema kupitia huu uzi:

Narudia kuandika tena,

Ifikie hatua muwe waelewa huwezi kujifanya una calculator ya kodi kwenye magari ambapo kodi yenyewe unatoza asilimia 80% hadi 100% ya manunuzi hii sio sawa.

Kwa mikodi yenu mikubwa ndio maana hamuwezi mkawa na walipa kodi wengi.

Mkumbuke kodi kubwa inawafanya kuathiri biashara ya mafuta kwa ujumla, biashara ya vipuri.

Hakuna sababu ya kodi asilimia 80 hadi 100 wakati ndani ya nchi hatuna uzalishaji wa magari au viwanda vya magari hakuna na kodi inakua ya kuumiza sio sawa.

Kweli mtanzania anunue gari dola 5000 kodi apigwe dola 4000 hadi 5000 halafu mtakuja na formular zenu za ajabu ajabu aibu sana hii.

Uchumi hauwezi ukakua kwa mtindo huo muelewe magari ni kifaa au chombo kinachorahisisha kuinua uchumi kwa namna moja au nyingine.

* Bandari Kuwepo Tanzania haimsaidii nafuu ya maisha mtanzania, kila bidhaa iko juu viongozi sio wabunifu wapo wapo tu.

Mkuu hongera sana sana kwa mada nzuri kabisa, umeona mbali sana.

Mkuu Maxence Melo, tafadhali hii mada msiiondoe, iwepo online muda wote, ikiwezekana na wewe mkuu Maxence utusaidie ujumbe huu uwafikie walengwa kwa namna yoyote, na sio kujali matumbo yao huku tusio na uwezo tunaumia.
 
Mfumo wa elimu umeleta aina ya viongozi waliokuwepo.

Akili ya kuwaza nje ya boksi hawana. Wanatafuta kitu ambacho ni obvious kwao then wanakirundika mikodi kibao.

Angalia petrol na diesel zinavyorundikwa makodi mara mbili ya thamani ya hayo mafuta.
 
Ubunifu katika kukusanya kodi hakuna ndio maana kunakua na mlundikano wa kodi kwenye kitu kimoja
Ndo akili zao zilipoishia ndio maana huwezi ona jipya lolote.

Telecom sector imepigwa kodi mpaka imeyumba, Petrol na Diesel zimesharundikwa mikodi kibao.

Uber na Bolt wameona wanapata faida sana, wamewapiga mikodi mpaka wameondoka.

Viongozi wanaowaza kijamaa ni nuksi sana kwa ustawi wa uchumi.
 
Yaani wanakamua kodi sawa na bei ya gari, aisee bongo bahati mbaya....

Ni hatari mno mkuu, kwanzia nyerere mpaka awamu ya 6 limekaliwa kimya suala la ushuru,sijui kwanini aise wanatufanyia hivyo!!

Ndugu zangu tupazeni sauti, tusikate tamaa na hilo, tunaumia tunaumia, magari dubai, Japan n.k bei ya kutupa, linunue sasa na ulilete huku aise kodi utakayolipizwa ni heri ukanunulia huku hata kama limechoka sawa tu.
 
Kodi inawekwa Kubwa Ili kupunguza idadi ya waagizaji magari. Kodi Ikiwa chini Kila mtu atanunua gar na itakuwa fujo. Mfano nchi ya Vietnam usafiri wao mkubwa ni pikipiki maana gar yoyote utakayonunua Kodi yake Kwa TSH n 80M.

Hivyo wanaotumia magari ni ni kama anasa tu.

Hata watumishi wengi wa serikali huko Vietnam wanaotumia pikipiki.

TRA Wako sahihi
 
Yaani wanakamua kodi sawa na bei ya gari, aisee bongo bahati mbaya....

Fikiria mzalishaji anakuuzia bei rahisi wao wanadandia kodi mara mbili hadi tatu ya bei ya manunuzi kesho wanaanza kulialia mapato hayatoshi wanashindwa kukumbuka mzunguko wa kiuchumi wameufunga wao wenyewe.
 
Harafu Polisi ikitokea ajali wao wanakimbilia kusema chanzo ilikua mwendo kasi kumbe magari ni chakavu tuu haya na hili hawawezi kulisema kwa kuwa wao ndio chanzo...na hawawezi kushauri kwa zile gari za nje hao trafiki watakagua nini kila saa si itakua salamu tu na wao wanapenda raia wakiendesha gari chakavu ili wapate utumbo..

Gari chakavu lazima watu watakufa kila siku na wataleta visababu kibao kumbe kodi inachangia hadi basi la abiria mtu anabembeleza used za miaka kibao kumbe kodi himilivu watu wataleta vyuma vipya, magari imara huokoa pia uhai wa watu
 
Back
Top Bottom