Nirudi kwenye hoja ya msingi, acheni watu wa vijijini, ambao ni wakulima, wanunue magari yao kama pick up, Fuso, trekta, guta nk kwa bei nafuu ili waweze kuzalisha mazao mengi na kuwaletea huko mjini kwa bei poa. Hayo magari ya wakulima hayahitaji lami wala nini, na kama mimi ningekuwa kwenye maamuzi basi ningepitisha sheria kwamba magari na mashine kama trekta, pick up, Fuso na nyinginezo ambazo zinachangia uzalishaji shambani vingelipiwa kodi less than 15% ya gharama ya hiyo mashine ili kila mkulima amiliki trekta, powertiler, lori/Fuso, guta, water pump, harrow, planter, spray mashine