DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mzalendo huyo huyo anatumia gari mln 500,mzalendo huyo huyo anawaminya wengine lkn yeye anaishi
Kibepari

Ova

Ukikuta wanavotoa macho utahisi hawa ni watu, mtu anaenda ziara kijiji hakina vyoo vya shule wala maji huku akiwa ndani ya gari la milioni 550 halafu anatoa ahadi ya mifuko 20 ya cement na mifuko yenyewe watu hawatoiona ni sound tu, mtu huyo huyo halipi chochote yaani kula hadi kunya yake na kuhonga kwake wanamlipia wananchi maskini, anavimbewa anafyatuka tu hamieni burundi utahisi nchi ni mali yake yaani unamwangalia unaona huyu basi tu
 
Wakibanwa issue za kodi wanajificha kwenye blah blah za ooohhh ni sheria bunge linetunga utahisi hilo bunge lilipotunga sheria lilitoweka duniani likaenda mbinguni hivo halipo tena
 
Bahati mbaya taasisi zetu nyingi zimeoza zinanuka rushwa na kila aina ya ufedhuli huu ndio msingi unakalia rasilimali kibao bado miaka na miaka unakwenda kuzungusha bakuli nje upewe misaada, anasimama kiongozi anasema nimezunguka huko duniani kutafuta pesa au vijipesa wakati zile pesa ni mikopo ambayo wewe mwanakijiji wa maswa huko shishiyu au chemba utalipa yeye kamwe hahusiki na hilo maana pamoja na kuiba bado atalishwa hadi anazikwa bila kuumizwa na malipo
 
Mkuu umeongea point tupu lkn kwenye swala barabara nafikiri km kungekua na system nzuri ya ukasanyaji Kodi na Kodi iwe ya Hali sio hii ya kukomoana barabara zingejengwa vzr mbona jiwe alionyesha kuwa kuna uwezekano.TRA kwa kweli Kodi ni pasua kichwa kabisa
Kuna point nimeongea Kama jiwe angeipokea from kwa nyerere halafu akae madarakani for almost 50yrs Mana angeifanya hii nchi iwe Kama Libya ya Muammar Gaddafi
 
75m mpaka 85m maana kodi yake imeongezeka hizo fusso zenyewe ni tani 4
Hoyaa hii Ni Kodi tu ama hela ya kununulia.
Sasa nikuibie Siri Kuna watanzania kibao wanamiliki gari sema wanazisajilia nchi nyingine. Kama hapa Kuna baadhi ndugu zangu Wana gari Zina plate ya Kenya Mana na Kuna Ama maisha yake huko so anapiga kazi,zinaleta mzigo tz Halafu zinarudi huko.

Kama vipi Hana nchi.


Am sure for incoming 5yrs I won't be in Africa. Napigania nipate hela ninunue apartment ya three/two bedrooms Australia or Canada nisepe dua zenu Wana jamii forum wenzangu. Unalipa Kodi halafu mazingira magumu like shule,roads, hospital,umeme unakatwa ovyo. Watu ama viongozi Wana njaa mno yaani mtu anatafuta uongozi kwenda kuiba Ina Mana kupata hela just by his/her brain powers Hana huo ubavu.
Ila bado najaribu kucheki nchi za kuzamia yaani wanangu waje wawe blacks wa huko mbele,jiulize why wale blacks wa mambele hawajawahi tamani Rudi afrika.


.sema jamani kitu umasikini kitu kibaya mno yaani mno ujue. Masikini anamchukia mtu bila ya sababu ukipata ajali na gari lako anashukuru Mungu wake kuwa naye akamuonapo Mana huyu alikuwa anaringa mno na gari lake.

Mara ngoja tuone atafika wapi na haka kakazi,kanyumba ama kaelimu Mana walikuwepo akina nyerere Sasa wapo wapi.

Sasa hapo Ni kuwa anajifariji kwa kukosa kwake ili aifanye subconscious mind iseto isimpe maumivu.



Magari na majumba na Mali Ni vya kupita kwani Nani akakuambia vitadumu na huku sie wenyewe tunapita. Jitahidi Basi na wewe Basi vipitie kwako japo na wewe umiliki gari ama bilioni hata Mia benki Ile u feel iyo feelings yake jamani
 
Hii nchi yetu vitu vingi unaweza kudhani vinafanyika kwa lengo la kutukomoa kabisa

Yaani kuingiza gari hapa kwetu ni kama kufanya anasa kabisa na sio usafiri

Ukiandaa 10M kuagiza kigali basi uandae 10M ya kodi, kama vile hatuna bandari yetu

Tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe
Kuna wakati nilimsikia jamaa mmoja mfanyabiashara wa Mbeya akilalamika kwa JPM kwenye kikao cha wafanyabiashara na rais Ikulu kwamba TRA wsnatoza kodi kubwa utadhani nao wamechangia mtaji wa biashara, mpaka Magufuli aliangua kicheko. Hivi inawezekanaje nchi ambayo haitengenezi hata baiskeli kodi ya kuingiza gari iwe sawa na gharama za kununua kodi?? How?? Sometimes tunamlaumu Mwigulu but unaweza kukuta hawa ma think tanks wa TRA ndiyo wanampa huu ushauri. Hivi haiwezekani kukodisha a well known and reputable tax consultant kutoka kokote duniani atusaidie wajameni?!!
 
Inasikitisha sana ukiona waganda, wazambia, wacongoman, wanyarwanda, vyuma wanavyosukuma uje ulinganishe na matajiri wenye bandari utacheka tu na kusikitika
Hiki unachosema yule mnyalukolo wa makanikia (Chris Lukosi) ameshasema mara nyingi mpaka akatuma video clip Facebook kwamba kule Uingereza alipo kwenye yard ya magari ya kuja East Africa magari makali huenda Kenya [emoji1139] na nchi nyingine, yale kuukuu ndiyo huja Bongo..
 
Narudia kuandika tena,
Ifikie hatua muwe waelewa huwezi kujifanya una calculator ya kodi kwenye magari ambapo kodi yenyewe unatoza asilimia 80% hadi 100% ya manunuzi hii sio sawa.

Kwa mikodi yenu mikubwa ndio maana hamuwezi mkawa na walipa kodi wengi.

Mkumbuke kodi kubwa inawafanya kuathiri biashara ya mafuta kwa ujumla, biashara ya vipuri.

Hakuna sababu ya kodi asilimia 80 hadi 100 wakati ndani ya nchi hatuna uzalishaji wa magari au viwanda vya magari hakuna na kodi inakua ya kuumiza sio sawa.

Kweli mtanzania anunue gari dola 5000 kodi apigwe dola 4000 hadi 5000 halafu mtakuja na formular zenu za ajabu ajabu aibu sana hii.

Uchumi hauwezi ukakua kwa mtindo huo muelewe magari ni kifaa au chombo kinachorahisisha kuinua uchumi kwa namna moja au nyingine.
* Bandari Kuwepo Tanzania haimsaidii nafuu ya maisha mtanzania, kila bidhaa iko juu viongozi sio wabunifu wapo wapo tu.
Mkuu kwahili ifike mda tubadilike Ina kera mnoo Kuna kamsemo wanasema ukinunua treni Jenga na reli yako"unaweza jiuliza yote haha Yana tokana nann? kunawatu Wana uwezo wa kufanya vitu vikubwa Ila Wana hofia t.r.a NI SEME MKOLONI MWEUPE BADO YUPO KWA SURA YA MKOLONI MWEUSI AU MZALIWA
 
Back
Top Bottom