TRA Kuanza Kuzitoza Kodi, Facebook, Instagram na Whatsapp
Watafanya hao watu wafunge huduma zao bongo sijui kama watakubali hahah
 
TRA leo wamafanya mazungumzo na wawakikishi wa Mitandao hiyo ya kijamii kuona namna Mitandao hiyo inaweza kulipa kodi kutokana na hiduma wanazotumia wananchi...
Hongera mother unaupiga mwingi sana. Kazi iendelee, kodi tutalipa tutake tusitake... Au tukazikwe naye?
 
TRA leo wamafanya mazungumzo na wawakikishi wa Mitandao hiyo ya kijamii kuona namna Mitandao hiyo inaweza kulipa kodi kutokana na hiduma wanazotumia wananchi...
Watasema ni magufuri,kaanzisha maana sasahivi kila baya lilianza wakati wa Magufuri
 
Wondrous country waache Ujasiria Mali huu mdogo uwe free tuumie tu kwenye bundle.

•Kumuongezea mzigo mtanzania kwa sasa waache inatosha.

N.B, ONGEZENI 200 KWENYE KILA CHUPA YA BIA,NA VILEVI HUKU MKISUKUMA FEDHA KWA WANANCHI NA KUCHOCHEA MZUNGUKO!.

"sisi walevi tutanua tu pombe hatuna jinsi na huwa hatujui kulalamika"
 
Shida ya hizi mambo wanakaa na kuamua wao kama wao haijalishi we Mwananchi utaipokea vipi na mwisho wa siku inapitishwa taka usitake.

Ila ngoja tuendelee kuona.
 
TRA leo wamafanya mazungumzo na wawakikishi wa Mitandao hiyo ya kijamii kuona namna Mitandao hiyo inaweza kulipa kodi kutokana na hiduma wanazotumia wananchi...
bado kodi ya kutumia barabara
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wake wa huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa ufafanuzi baada ya TRA kukutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini.

"Mkutano kati ya TRA na kampuni ya META ulikuwa ni mkutano wa awali wao kuweza kuelewa mazingira ya sheria za kodi za Tanzania na pia kuweza kutupitisha katika jinsi wanavyofanya biashara yao na wanavyotozwa kodi katika Nchi nyingine.

"Lengo ni kufikia mahali huko mbeleni ili kampuni hiyo ichangie kodi kwa pesa inayopata kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao, Wananchi hawatakiwi kuwa na hofu yoyote kwasababu hii inahusu biashara inayofanyika na kampuni hiyo katika Nchi mbalimbali.

"Na hili sio jambo geni lipo dunia nzima, tumesikia Kenya tayari hilo lipo, Benin, Cameroon na Nchi za Ulaya ambako kampuni hizo kubwa za mitandao duniani zinachangia kodi kwa kufuata sheria za nchi husika na taratibu za kimataifa," - Kayombo
 
Round hii hawa achi kitu [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom