Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Madini wachaji kodi 4% alafu urithi 15% akili za kiafrika bwana!
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
kodi sawa kwa maendeleo ya nchi, lakini ni ngumu kutengeneza wananchi wazalendo kwa kuwakata kodi 15%, hii lazima itakuwa kero. Hakuna maneno yoyote mazuri utakayompa mtu unayemkata 15% akakakuelewa. Hapa lazima nguvu itatumika kupata kodi hiyo. Hakutakuwa na uhiari wa kutoa kwa sababu 15% ni kubwa sana. Serikali kupitia mamlaka zake itujengee moyo wa kupenda kutoa kodi kwa hiari, furaha na moyo wa kupenda, na hii inahitaji pamoja na kauli nzuri za kutia moyo toka kwa watendaji wa serikali, itozwe kodi kiasi ambacho hakitamuumiza mlipaji. Let say kodi ni 1%, haitahitaji nguvu nyingi kuipata, wahusika watahitaji kukumbushwa tu na wengi watatoa. Naamini itapatikana pesa nyingi kuliko hiyo 15% ambayo kuipata mpaka mtu aingie kwenye 18 za serikali.
 
Kuna nchi yoyote inayokusanya kodi kama hizo?
Pamoja na wingi wa kodi lakini pia wabuni namna ya kumfanya mtu alipe kodi kwa hiari. Mojawapo ya njia hizo ni tax credit zinazotoa upendeleo kwa walipa kodi kwenye baadhi ya huduma na kuwapunguzia privilege wasiolipa kwa maksudi.
Ndio ndugu yangu. Mfano mmoja wa nchi hizo ni Uingereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeniacha !! Kwani mshahara si unakatwa kodi ? Sasa iweje nilichokusanya kwa miaka yote hiyo bado pia wachukue kodi ?? Kweli tumeishiwa mawazo, rasilimali kibao hatujui zitumia sasa tunaanza kunyonya mile kidogo tulichobarikiwa..!! Mi nafikiri wajielekeze sana kwenye hizi rasilimali za nchi maana ndio zenye fungu kubwa la mapato !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Waliweka matumaini makubwa kwenye chenji ya makinikia sasa tumaini hilo halipo tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adui wa maskini ni maskini mwenzie hasa pale akipewa mamlaka ya kumtawala.

Task Force12
 
Hivi huyu jamaa ana nini na familia yake maana sijawahi sikia mke wake au watoto wake wakihusishwa na kashfa zake zaidi ya watoto wa ndugu zake. hata ile nafasi ya yule bint kuingia UDOM ki utata utata inaonyesha ilikua initiative na strugle za mama au bint mwenyewe au haikubali kuwa ni familia yake
Mkuu lile jiziiii lina roho mbaya mpaka kwa familia yake
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Inheritance ni income pia....it should be taxed....
Wazungu wanayo kitambo tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi kama hizi zipo sana kwenye baadhi ya nchi huko ughaibuni.
Nchi zenye maendeleo zina kodi nyingi sana. Maendeleo yana kuja kama kila mtu yupo tayari kulipa kodi kwa shughuli yoyote [emoji562]
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Hawa wahongaji wa Bongo Movie mbona hawapo siku hizi,hujamsikia Sepetunga juzi akilalamika kuwa maisha yamekuwa magumu sana inabidi wabuni mbinu mbadala za kujiingizia mapato...
 
Hii kodi ipo. Na ina maana sana. Kikubwa watoe elimu. Kuna nchi nilisoma mwalimu wangu akanisimulia kuwa kurithi siyo deal sababu kodi yake lazima ukae chini. Ni muda and was not interested hivyo sikumbuki saana maelezo alotoa. Ila ni kama aim ya nchi yao ni usawa. Wazazi kama ni mambo safi na weww kijana tafuta zako. Kitu kama hicho. Especially wana ukali wa mtu kurithi land. Maybe sababu wana upungufu wa ardhi.
 
Je hiyo zwadi inakuwa haijalipiwa kodi. Mfano gari inanunuliwa mtu anapewa zawadi wakati wa ununuzi kodi hailipiwi.
Pili urithi unadai kodi si laana hizi jamani. Kabla ya kurithi zilikuwa wapi. Hii ni njaa sio ubunifu
 
Sijui vigezo gani vitakavyotumika hapa, lakini hili la urithi linaweza kuleta mateso fulani hivi hasa kwa familia ambazo zitajikuta hazina chanzo chochote cha mapato zaidi ya hiyo/hizo property za kurithi.

kuna uwezekano tukashuhudia mali zikipigwa minada kufidia kodi hiyo na familia husika kujikuta kwenye umaskini zaidi. labda kama kutakuwa na categories kama walivyofanya kwenye kodi ya majengo.

Ushauri wangu ni kwamba zipo njia ambazo ni very effective kwenye ukusanyaji wa kodi ambazo hazijatumika bado na zinaweza kusaidia kuongeza mapato na kuziba mianya ya ukwepaji kodi.

kwa mfano kupiga marufuku kulipa cash kwenye baadhi ya huduma na badala yake huduma hizi zilipiwe kwa kutumia kadi au Mpesa/Tigopesa/Airtel money n.k. mfano hotel zote kubwa, mafuta ya petrol/diesel, ticket za ndege/meli, Super market kubwa, maduka makubwa, hospitali zote (siyo zahanati) na huduma/malipo ambayo hayawaathiri watu wa chini na wanaoishi vijijini ambako huduma za mpesa/tigopesa/airtel money hazipatikani kwa urahisi sana.

Binafsi siamini sana kwenye EFD kwa sababu bado kuna ukwepaji mkubwa wa kodi kwa kutumia machine hizo.
 
Back
Top Bottom