Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Naomba elimu kuhusu kodi ya urithi.....mfano...baba amafariki ameacha nyumba mbili ambazo amekuwa akilioia kodi miaka yote.Baada ya mimi kurithi hizo nyumba,nitahitajika tena kulipia kodi nyumna hizo.??
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
maoni yangu tutakutana 2020 basi
 
Nchi iko vibaya. Pamoja na kuongeza vyanzo vya kodi na kubana kila mahali bado hali ni tete na mambo ni magumu. Hawa watu wanapaswa kuondoa soni na kumfuata Mzee wa Msoga wamuulize alikuwa anapata wapi fedha. Ninachoona watatoza kodi kila wanachokiona lakini bado hawatatoka.
 
Wa
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Waje tu hata na "marriage tax" yaani ukifunga ndoa unalipa kodi, au "birth tax" ambayo unalipa pale unapozaa mtoto! Vyanzo vya mapato ni vingi
 
Sawa tu, alimradi kodi irudi tena kwetu kwa njia za miundo mbinu, elimu, afya, ustawi wa jamii, maji, umeme na usalama...
Hatutajali hata kidogo...
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Hii sheria mbona hipo miaka mingi tuu sana sana wahindi ndio walikuwa wanalipa kutokana na kuwa na makampuni yaliyo sajiliwa .mtoto akirithi anatozwa hiyo Kodi.hivyo tuseme Tra wameamua kuifanyia kazi kwa watanzania wote ataa kwa urithi Wa Mlalahoyi .mjane au mtoto ukirithi kibanda cha milioni 5 unadaiwa laki saba na nusu na Tra .Dduuhh Baba huyu hakika amezaliwa mlango Wa kutia hasara .hakuna rangi tutaacha kuona !!!
 
waTanzania tujiandae kisaikolojia. Tanzania ya miaka mitano au kumi ijayo... itakuwa na mabadiliko mengi sana. wanaoamini kwamba hali ya nyuma itarudi JPM akiondoka....Naweza sema ni kama ndoto za mchana. Hata hizi kodi nyingi zitaibuliwa mpaka tutajiuliza kama tuko TZ tunayoijua au vipi. Na anaweza kuondoka JPM akaja mwingine shida zaidi!
 
tukopi tukopi tunavyoviweza,
Nakuunga mkono tusipende kukopi kila kitu maana wenzetu wanazo hizo kodi lakini pia kuna child credit wana kusanya na wanazitumia. Tukifanya hivyo ni sawa. Hizo kodi kwa wenzetu hazi waathiri wako happy kulipa. Kwa mfano wewe mwenye income kubwa unakatwa kodi kubwa na kuna mtu hakatwi Bali anaongezewa kwenye income yake kuna working tax credit children tax credit kwa wenye watoto ambao income yao inaonekana haitoshi haya ndiyo matuminzi ya kodi siyo kumkomesha raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kodi ni ngumu kuitekeleza kama kuchimba mawe baharini!
Ni rahisi sana kupotoshwa kwa kodi hii kwa kupewa majina mabaya kitu ambacho kitapelekea serikali kuchukiwa na wananchi.
Serikali atakuwa mrithi wa lazima kwenye kila familia umtake usimtake utagawana nae.
Mfano:-
Tuko watoto 10 kwenye familia
Baba ameacha sh 10,000,000 benki ambayo urithi wetu.
Tukaamua kugawana sawa
Serikali 15% = 1,500,000 baki 8,500,000
Mama 15% ya fedha iliyobaki baada ya kodi
8,500,000 x 15% = 1,275,000
Baki = 7,225,000 ambayo tutaigawa watoto wote kumi
7,225,000 / 10 = 722,500/=

Kila mtoto atapata T shs 722,500/=
Mama yetu mjane T shs 1,275,000/=H
Mheshimiwa serikali T shs 1,500,000/=

SASA TAFAKARI KUANZIA HAPO.

Hebu pata picha hapo nini kitatokea?
Mrithi mkuu atakuwa serikali kwenye kila familia ingawa sina uhakika 15% itakatwa baada vitu gani kufanyika lakini kwa vyovyote ni shida.
Kodi za namna hii ndio huwa zinaondoa serikali madarakani kwa wenzetu kwani huwa hazizingatii utamaduni wa nchi.
Ni rahisi sana kodi hii kuitwa kodi ya msiba na hawatapata jina zuri la kuwafanya wananchi waipende.
Mbunge wangu ikiipitisha ajiandae kuondoka maana ndio kete bora kuliko zote
Kama mwenzake aliunga mkono kusogezewa huduma ya gereza na akaondoka katika hili sijui.
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Balaa hili, uingereza wanalipa kitu kama 60% kwenye inheritance tax, sisi tunaiga tu bila kuangalia hali za kiuchumi za nchi yetun hutashangaa kuja kuskia wanaintroduce wedding tax

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikitokea marehemu alikuwa na madeni. Mtoto amerithishwa madeni, TRA watabeba mzigo wa deni kwa 15%?
Wakikubali kubeba na sisi tutakubali kutoa, kodi lazima ijali usawa safi sana.
 
Hii kodi ipo. Na ina maana sana. Kikubwa watoe elimu. Kuna nchi nilisoma mwalimu wangu akanisimulia kuwa kurithi siyo deal sababu kodi yake lazima ukae chini. Ni muda and was not interested hivyo sikumbuki saana maelezo alotoa. Ila ni kama aim ya nchi yao ni usawa. Wazazi kama ni mambo safi na weww kijana tafuta zako. Kitu kama hicho. Especially wana ukali wa mtu kurithi land. Maybe sababu wana upungufu wa ardhi.
Yes lakini katika mazingira yetu kodi hiyo haina maana. Yaani ni sawa na kuwatoza 'mayatima' kodi kwa kile kidogo walicho nacho
Uelewe pia kuna nchi uzao wa watoto ni wa kiwango kidogo.
Hapa kwetu mtu kaacha 7 na nyumba sh 10M halafu unakata kodi wakati kuna ugomvi unarindima

Kodi kwa mfano ya 15% kwa 10M ni sawa na 1.5M. Kiasi hicho ni 1.5 ni pungufu ya allowance ya siku moja ya wabunge 10 kukaa katika viti vya kazi
I mean kukaa na si mshahara au mafuta n.k
Nadhani kuongeza mapato TRA wangemshauri Rais
1. Apunguze siku za Bunge
2. Au afute kodi ya kukaa kwenye kiti cha kazi
3. Kufuta chaguzi za njiani za hovyo kama za Madiwani ambazo zitagharimu 700M

Hilo ni bora kuliko kukata kodi kwa mayatima.

Kwasasa tusubiri kodi za mimba kwa akina mama.
Ultra sound ikithibitisha ni kiume ni 13% atalipa mahari mbeleni, wa kike 15%!!

Nchi hii inavituko, tuna utajiri kama utalii hatuifikirii huko tunataka short cut kila kitu
 
kazi tunayo...
  • Land rates
  • Inheritance tax
  • Tax kwenye zawadi inayozidi 5m/-
  • Property tax
  • Payee
  • Income tax
  • VAT kwenye bidhaa
  • Vehicle registration tax
  • Fuel tax
  • ...
  • ...
Twafa...🙁😡😕😳😵
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
1. Huo urithi anayeutoa (marehemu) alikuwa akilipa kodi?! Kama ndiyo.. Kuwatoza wanufaika waurithi huo haitakuwa kutoza kodi vitu vile vile kwa Mara ya pili?!

2. Kama itapitishwa ni vitu vyote vya urith vitatoza hiyo 15%? Kama jibu ni ndiyo.. Itakuwaje kwa vitu kama vibuyu na uganga utakaorithishwa.. Nguo na fimbo ya babu.. Au Mali ambazo hazikununuliwa?!

3. Kwenye zawadi pia.. Je iliponunuliwa ililipiwa kodi?! Kama ililipiwa..kwann ikatwe kodi tena?! Kwenye kuwa zawadi ni swala la matumizi.. Akiamua kuipaki.. Au kuitoa kafara kwa Mungu wake wa Kiafrika kwa kuichoma moto nani atatozwa kodi hiyo ya 15%? Mungu wake au Mtoaji wa sadaka?

Note: TRA ili wapate hiyo 15% ya mirathi wajiasili kuwa watoto wa familia zote za kitanzania. Hakuna namna.
 
Back
Top Bottom