Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Madini wachaji kodi 4% alafu urithi 15% akili za kiafrika bwana!
 
kodi sawa kwa maendeleo ya nchi, lakini ni ngumu kutengeneza wananchi wazalendo kwa kuwakata kodi 15%, hii lazima itakuwa kero. Hakuna maneno yoyote mazuri utakayompa mtu unayemkata 15% akakakuelewa. Hapa lazima nguvu itatumika kupata kodi hiyo. Hakutakuwa na uhiari wa kutoa kwa sababu 15% ni kubwa sana. Serikali kupitia mamlaka zake itujengee moyo wa kupenda kutoa kodi kwa hiari, furaha na moyo wa kupenda, na hii inahitaji pamoja na kauli nzuri za kutia moyo toka kwa watendaji wa serikali, itozwe kodi kiasi ambacho hakitamuumiza mlipaji. Let say kodi ni 1%, haitahitaji nguvu nyingi kuipata, wahusika watahitaji kukumbushwa tu na wengi watatoa. Naamini itapatikana pesa nyingi kuliko hiyo 15% ambayo kuipata mpaka mtu aingie kwenye 18 za serikali.
 
Ndio ndugu yangu. Mfano mmoja wa nchi hizo ni Uingereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliweka matumaini makubwa kwenye chenji ya makinikia sasa tumaini hilo halipo tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adui wa maskini ni maskini mwenzie hasa pale akipewa mamlaka ya kumtawala.

Task Force12
 
Mkuu lile jiziiii lina roho mbaya mpaka kwa familia yake
 
Wengine wanaingia humu kama vile malaika halafu wanamwaga tumba za ubuyu tu na kuwaita wenzao vilaza...DEVIL'S SHIT

Ubinaadam kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inheritance ni income pia....it should be taxed....
Wazungu wanayo kitambo tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi kama hizi zipo sana kwenye baadhi ya nchi huko ughaibuni.
Nchi zenye maendeleo zina kodi nyingi sana. Maendeleo yana kuja kama kila mtu yupo tayari kulipa kodi kwa shughuli yoyote [emoji562]
 
Hawa wahongaji wa Bongo Movie mbona hawapo siku hizi,hujamsikia Sepetunga juzi akilalamika kuwa maisha yamekuwa magumu sana inabidi wabuni mbinu mbadala za kujiingizia mapato...
 
Hii kodi ipo. Na ina maana sana. Kikubwa watoe elimu. Kuna nchi nilisoma mwalimu wangu akanisimulia kuwa kurithi siyo deal sababu kodi yake lazima ukae chini. Ni muda and was not interested hivyo sikumbuki saana maelezo alotoa. Ila ni kama aim ya nchi yao ni usawa. Wazazi kama ni mambo safi na weww kijana tafuta zako. Kitu kama hicho. Especially wana ukali wa mtu kurithi land. Maybe sababu wana upungufu wa ardhi.
 
Je hiyo zwadi inakuwa haijalipiwa kodi. Mfano gari inanunuliwa mtu anapewa zawadi wakati wa ununuzi kodi hailipiwi.
Pili urithi unadai kodi si laana hizi jamani. Kabla ya kurithi zilikuwa wapi. Hii ni njaa sio ubunifu
 
Sijui vigezo gani vitakavyotumika hapa, lakini hili la urithi linaweza kuleta mateso fulani hivi hasa kwa familia ambazo zitajikuta hazina chanzo chochote cha mapato zaidi ya hiyo/hizo property za kurithi.

kuna uwezekano tukashuhudia mali zikipigwa minada kufidia kodi hiyo na familia husika kujikuta kwenye umaskini zaidi. labda kama kutakuwa na categories kama walivyofanya kwenye kodi ya majengo.

Ushauri wangu ni kwamba zipo njia ambazo ni very effective kwenye ukusanyaji wa kodi ambazo hazijatumika bado na zinaweza kusaidia kuongeza mapato na kuziba mianya ya ukwepaji kodi.

kwa mfano kupiga marufuku kulipa cash kwenye baadhi ya huduma na badala yake huduma hizi zilipiwe kwa kutumia kadi au Mpesa/Tigopesa/Airtel money n.k. mfano hotel zote kubwa, mafuta ya petrol/diesel, ticket za ndege/meli, Super market kubwa, maduka makubwa, hospitali zote (siyo zahanati) na huduma/malipo ambayo hayawaathiri watu wa chini na wanaoishi vijijini ambako huduma za mpesa/tigopesa/airtel money hazipatikani kwa urahisi sana.

Binafsi siamini sana kwenye EFD kwa sababu bado kuna ukwepaji mkubwa wa kodi kwa kutumia machine hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…