Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Salamu wakuu,
Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina), kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.
Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro) ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.
Pia soma: TRA fanyeni kazi zenu ipasavyo, Wahindi na Wachina wanalichezea taifa hili
Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa, nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.
Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD, huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.