DOKEZO TRA mulikeni hawa Wachina, wanahujumu uchumi wetu. Hawalipi kodi ipasavyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni NUSU kwa NUSU.[emoji1484]
cc: MWANAKA
 
Attachments

  • IMG_0096.JPG
    IMG_0096.JPG
    218 KB · Views: 5
Ukwepaji kodi na rushwa vipo Dunia nzima. Itakuchukua muda mrefu kuendelea endapo unataka halali.

Binafsi nipo tayari kuchukua risiti ya nusu bei, ili hela inayobaki nifanyie mambo mengine.

Si kila kinachozungumzwa duniani ndicho kinachotendeka. Wanatuhubiri kuwa wazalendo lakini wao wanapiga.
 
Sio unakataa kitu bila kua na hona za msingi we ungewaambia tu nyie niandikie risiti halisi maana risiti nikiipeleka ofisini naenda kurudishiwa hela yangu..ila kama hujawahi fanya biashara huwezi elewa umuhimu wa wanachokifanya hao wachina..pia hata ukinunua mzigo i.e china invoice hua haiandikwi bei halisi uliotoa

hiyo ipo hata ulaya na america.. biashara ili isife lazima ujanja uwepo..

hujui hata makampuni makubwa kama voda, tbl, pwc, tigo, total zinaajiri wataalamu wa kodi ambao wanapewa bonus na mishahara mikubwa wakisaidia kukwepa kodi
 
Salamu wakuu:
Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina).... kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.

Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro).... ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.

Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa.... nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.

Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD.... huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.
Wako wapi aisee nina shida ya godoro
 
Ndo uwe unaenda kununua dukani... Unapunguziwa being halafu unaleta unaaa..

Sijapunguziwa bei, ni ‘bei ya kiwandani’ tena ni fixed.... wenyewe wanaita ‘wholesale price’.
 
Salamu wakuu:
Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina).... kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.

Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro).... ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.

Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa.... nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.

Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD.... huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.
Kariakoo maduka ya wahindi ya machine na spares huko nako balaa! Nusu bei kitu cha kila siku.
 
we mleta mada yaelekea hujawahi hata kuuza pipi ndo maana umeleta habari kama hii..otherwise ungejua jinsi mazingira ya biashara yalivyo magumu nchi hii usingeandika huu upupu.

Uko sahihi.
 
hiyo ipo hata ulaya na america.. biashara ili isife lazima ujanja uwepo..

hujui hata makampuni makubwa kama voda, tbl, pwc, tigo, total zinaajiri wataalamu wa kodi ambao wanapewa bonus na mishahara mikubwa wakisaidia kukwepa kodi

Kwahiyo haramu ikifanywa na wengi inageuka halali..? [emoji848]
 
Mleta mada ni Muongo sana! We utakua sio mzalendo bali ni mnaa na mnoko tu! Kwanini hukuelekea TRA siku hyo hyo kuripoti na ushahidi ulikuwa nao? Na bado zaidi unakuja kuleta habari nusu humu jamvini!? Nenda Police au TRA.
 
Nimeamua kutumia jukwaa hili kutoa dukuduku nikiamini TRA pia wako humu, uongo na unoko wangu uko wapi ndugu nimeweka sehemu ya risiti hapo.... huko police wala sikuwa na lengo la kukukamatisha endelea kuhujumu tu.
 
Back
Top Bottom