DOKEZO TRA mulikeni hawa Wachina, wanahujumu uchumi wetu. Hawalipi kodi ipasavyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Salamu wakuu:
Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina).... kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.

Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro).... ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.

Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa.... nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.

Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD.... huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.
Mkuu wakale wapi?
 
Mkuu hii picha umecrop TIN haionekani, TIN ikionekana tu mchina kesho atakuwa kambani

Nimefanya kuhifadhi kwanza, hili likiwafikia wahusika nitatoa ushahidi.... ila nilivyoshambuliwa najiona nipo hatiani.
 
umetaka bei ya kiwandani ila unataka kununua godoro 1 (kweli?)

vitu vingine unakausha unapita hivi baba,hizo tarumbeta unazopiga

Kuna viumbe watakuja kupiga hela vibaya mno na serikali ndio haipat hata 10

Ki ufupi ulichofanya ni kuwashtua wapigaji (oyaaaa nendeni kule kuna dili)

Taarifa yako haijakaa kutokomeza tatizo bali imekaaa kuwasanua wapigaji waende kula huko

Siku nyingine ukitaka okoa au wasaidia TRA weka taarifa za mpk location,aliyekuhudumia,piga picha wote

Weka full details then mwaga mchele hadharani

Ila kwa taarifa hiyo Hamna kitachofanyika wataamini ni unoko tu na kuchongeana

Wabongo tunaongoza kwa roho mbaya,na tumeshatambuana so Taaarifa bila ushahidi

Ni sawa na story kijiweni
 
Soma vizuri mkuu wangu, nilitishiwa kuwa nikileta ujuaji bora niache kununua nikanunue dukani.... nikawaza kuhusu punguzo na nimechapa mwendo hadi kiwandani nikaamua kuihujumu serikali.
Iweke hiyo EFD receipt hewani mamlaka husika ilifanyie kazi naamini wapo humu
 
umetaka bei ya kiwandani ila unataka kununua godoro 1 kweli..?

Wabongo tunaongoza kwa roho mbaya,na tumeshatambuana so Taaarifa bila ushahidi

Ni sawa na story kijiweni

Ushahidi gani unataka, nilichofanya ni kumfunga paka kengere tu naamini kwa wahusika wamenielewa.... akitokea mhitaji wa uthibitisho ninaweza kusaidia kwa vile vielelelezo ninavyo sijaweka tu kwa kuwa nabezwa na wengi hapa.
 
Salamu wakuu:
Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina).... kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.

Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro).... ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.

Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa.... nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.

Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD.... huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.
Mkuu pellangyo.! Hili suala humu mimi binafsi nililipigia kelele Tangu mwaka Jana au Juzi lakini TRA wamefunga masikio na macho hawaoni.!
Kariakoo nzima huu ndio mchezo wao hasa kwenye maduka ya jumla ambayo wateja wake wanajulikana na mbaya zaidi watu hawa wanakuwa na risiti feki za EFD yaani ama zimetumika na duka jingine au alikata jana yake kisha zikarudishwa na wanunuzi ukisha nunua bidhaa anakupa hiyo risiti au wanatoa nyingine lakini kwa bei ya Chini isiyoendana na thamani ya Mzigo ulio nunua.!
Sbbu ni Mchezo unaochezwa na maduka mengi ukikataa kuchukua hiyo risiti unaweza usiuziwe mzigo unao utaka na ukienda duka jingine pia utakutana na mchezo huo huo.! Ajabu ni kuwa wahindi hawafanyi huu mchezo tatizo ni kwa waswahili wazawa na hao wachina sasa hivi
 
Naomba jina la kiwanda na sehemu kilipo PM pls
 
Kuna kamchezo kameingia, risiti zinazotoka sheli baada ya kununua mafuta kuna baadhi ya watu huwa wanaziacha.... Juzi kati Kuna boda boda nilipanda akaniambia hizo huwa watu wa sheli wanaziuza kwa wafanyabiashara.....
Sijajua kama kuna ukweli katika hilo.
 
Asante sana mkuu, waswahili ndio wanaotumika kurahisisha kwa njaa zetu na kujipendekeza kwa mwajiri... Wahindi waoga nadhani hawajasahau alichowafanya Mzee Nchonga.
 
Kuna kamchezo kameingia, risiti zinazotoka sheli baada ya kununua mafuta kuna baadhi ya watu huwa wanaziacha.... Juzi kati Kuna boda boda nilipanda akaniambia hizo huwa watu wa sheli wanaziuza kwa wafanyabiashara.....
Sijajua kama kuna ukweli katika hilo.

Duuh, risiti used..!! [emoji15]
 
Back
Top Bottom