DOKEZO TRA mulikeni hawa Wachina, wanahujumu uchumi wetu. Hawalipi kodi ipasavyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Salamu wakuu,

Hili nimekutana nalo jana, japo imekuwa sio ngeni ila hii niliipokea kwa uchungu mkubwa sana (sijui kwa vile ni Wachina), kama mzalendo ikabidi ‘nipachimbe’ sana.

Wanauza bidhaa kwa kile wanachoita ‘bei ya kiwandani’ hivyo mteja unategemea unafuu wa bei, na kwa kuzingatia hilo nilifika hadi kiwandani kupata ofa hii (godoro) ila masharti niliyopewa ni kwamba stakabadhi (risiti) itaandikwa NUSU ya kiasi ninayolipia mzigo.

Pia soma: TRA fanyeni kazi zenu ipasavyo, Wahindi na Wachina wanalichezea taifa hili

Nilipoonesha kutoafiki kwanza ‘wahudumu’ wakanishangaa kwamba mi wa wapi sijui utaratibu huo ni wa siku zote, na kauli za vitisho kuwa wataacha kuuzia ‘watumiaji’ ili kuepusha usumbufu na ujuaji badala yake wauzie wafanyabiashara tu ambao wao wanaelewa, nami kwa vile sikutaka kukosa kilichonipeleka ikabidi kukubaliana na masharti nishiriki kwenye hujuma.

Mamlaka zina mkono mrefu, mnajua yanayoendelea kukwepa VAT za EFD, huu ni mfano tu ila picha ni kubwa sana TRA kuweni macho.
 
Sio unakataa kitu bila kua na hona za msingi we ungewaambia tu nyie niandikie risiti halisi maana risiti nikiipeleka ofisini naenda kurudishiwa hela yangu..ila kama hujawahi fanya biashara huwezi elewa umuhimu wa wanachokifanya hao wachina..pia hata ukinunua mzigo i.e china invoice hua haiandikwi bei halisi uliotoa
 
Kama kweli una nia thabiti ya kukomesha tabia hiyo, ungeweka wazi hilo duka liko wapi, au kiwanda kiko eneo lipi na ikiwezekana hata hiyo Stakabadhi ya nusu bei ibandike humu jamvini ili mamlaka husika zichukue hatua. Au ukishindwa weka kwenda email ya TRA huduma kwa wateja.
Vinginevyo hongera kwa kuonyesha njia Mkuu.
 
Binafsi sizipendi hizi mashine kabisa,Nashauri hali ya ukadiriaji irudishwe kama awali,
Duka lipo kariakoo kwa mwaka milioni 10,utalipa kwa awamu 4,full stop,daka lako linapewa namba maalumu,pamoja a/c ya kulipia.then Tra wanakuwa wanamonitor tu kwa Gps.,hili liambatane na adhabu kali kupitiliza ikiwa ni pamoja na kufilisi.
 
Sasa kwanini usingewaambia wa kuandikie bei halisi uwe mzalendo
 

Je, nahitaji niwe na sababu ya msingi kupata risiti halali..?
 
Sasa kwanini usingewaambia wa kuandikie bei halisi uwe mzalendo

Soma vizuri mkuu wangu, nilitishiwa kuwa nikileta ujuaji bora niache kununua nikanunue dukani.... nikawaza kuhusu punguzo na nimechapa mwendo hadi kiwandani nikaamua kuihujumu serikali.
 
Nonsense , nchi hii hamna faida ya kulipa kodi , it doesn't make any difference . Mijitu inakwapua trillions haiwajibishwi halafu inapambana kupata Mia mbili Mia mbili za wachina . ****

Come to your senses, uzalendo kwanza.
 
Weka hapa hiyo efd receipt tuifanyie kazi pole mkuu na hongera kwa uzalendo wa kutoa taarifa
 

Nikiweka stakabadhi hapa haina details kuonesha tofauti ya bei halisi na kisio, imetaja tu kiasi na aina ya bidhaa (godoro) ambalo wewe hujui bei yake so huwezi kulinganisha.... nashukuru umenielewa Hata kama uwasilishaji wangu haujatimia ila ujumbe ni ule ule.
 
Ila linapokuja suala la ushindani Wazalendo (wa Tanzania ) hupenda faida kubwa sana wa china huweka faida ndogo hili hupelelea kutokuweza kushindana na kirahisi!!
Hapa kuna kaharufu ka conflicts of interest!
 
Kilichoniumiza zaidi ni pale ninayejadili naye ni Mswahili, yeye anakazia kuwa hayo ni maelekezo ya kiofisi na ndio utaratibu wao.... kwamba nikionekana ameshindwa ‘kunimudu’ ni bora tuache biashara kwa maana likimfikia Boss wake ‘Mchina’ nitahatarisha kibarua chake.

Kwa kuzingatia hali ilivyo mtaani, nikaguswa na chozi la huyu raia.... njaa zetu zinatumika vibaya kujiibia wenyewe.
 
Haya ni mambo ya kawaida sana kwenye biashara hapa bongo,njia za ukwepaji kodi ni nyingi sana tofauti na hiyo .
.
.
Hivi ukilipa kodi halali ndo maisha yako na ya yule mwana wa nchi kule kijijini yanapata nafuu?

Kila mtu ni mkwepa kodi nchi hii,hata hao wanaokwambia kuwa wao ni wazalendo i.e manunuzi makubwa ya serikali na miradi ya uwekezaji,

NB:Rejea Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…