Mheshimiwa Tundu Lissu alivyokuwa Mbeya aliituhumu TRA kwa kufanya unyang'ani wa kutumia silaha, aliueleza umma kuwa kuna wafanyabiashara walishikiwa bastola ili wawape hela kutoka kwenye account zao. Siamini haya yanaweza fanyika katika uongozi wa Dr Mhede huku ni kumchafua. TRA sio chama cha siasa wala jumuia ya CCM, kuanza kuishutumu hadharani sio haki. Na kama kuna shutuma dhidi yao kuna utaratibu wa kushughulikia rufaa za kodi Lissu kama wakili alipaswa kuzifuata na haki ikatendeka
Lissu hajawa mgombea Urais kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wala kampeni hazijaanza kwa mujibu wa sheria, anapozungumza anazungumza kama raia wakawaida na anapaswa kuwajibika yeye kama yeye kwa matamshi yake mwenyewe. Anaposema mtu akiinyima hela CCM TRA wanaitwa kumfirisi hizi ni tuhuma nzito dhidi ya TRA na hazipaswi kufumbiwa macho.
Kama ni utendaji kazi wa TRA kwa awamu hii ya Dkt. Mhede wamekuwa waungwana na watenda haki, wafanyabiashara wako huru kujieleza na maamuzi yanafanyika kwa haki, hakuna tena habari ya kufungiana maduka wala kusaka wafanyabiashara na mgambo wa jiji, sasa hizi tuhuma anazotoa amepata kutoka wapi? Lissu hakuwepo nchini wakati Dr Mhede akikabidhiwa TRA ni vyema akachukua muda wa kufuatilia utendaji wake.