TRA ni SHIDA: Wavamia Ofisi hapa Viwandani

Ingawa mm pia ni muumini wa ustaarab, hii taarifa haijakaa sawa. Toa details zaidi maana wabongo tunajuana.

Hakuna mtu mwehu au mjinga avamie tu, na kuondoka na laptops...
watu wanadharau demand notice na simu, huo ni ujinga, hata kama unadaiwa nenda kaongee nao, wakati mwingine tunalaumu TRA kumbe ni maudhi ya kampuni yenyewe, na si kila kodi inasubiri hadi mwaka ndo ulipe, unawakata watu paye afu hutaki kulipa
 
Hiyo ndiyo dawa ya wakwepa kodi
 
Team Jiwe kazini ! hujawahi kuuza hata mapera lakini unajifanya mjuaji !
 
Mama kasema angependa kuona tukilipa kodi halali kwa hiyari bili shurti, hajasema tukwepe Kodi au tulipe chini ya kiwango
"Maneno yangu tutekeleze hiyari kwa uaminifu mkubwa, serikali ina mamlaka ya kutumia shurti pale inapobidi"
 
Hehe wapambe wa samia wako njia panda hawajui waunge mkono au wademke
 
Huko ndio kudaiana gani? Unachukua vielelezo vya mtu na kuondoka navyo kwanini akienda mahakamani asiseme TRA has tampered with his records.

Haya ndio mambo ya ovyo TRA muda mrefu na yanayo halalisha ubambikiaji wa madai.

Watu walipe kodi na wala sio swala la kumbelezana but surely that is not how tax fraud is investigated, kama hawana hao wataalamu wa auditing si bora waazime kutoka ofisi ya CAG.

Desperate time calls for desperate measures, naona baada ya kuona maporomoko kwenye makusanyo wamegundua kodi sio swala la mzaha.

Watu wakisema waachwe waliopo TRA washaanza kupata uzoefu wa kukusanya kibabe kwa taratibu za sheria, japo kulikuwa na makosa ya hapa na pale mkurugenzi alikuwa kwenye harakati za kurekebisha uwezi badilisha culture ya shirika zima overnight.

Sasa kilichofanywa hapo kama kweli unaweza justify vipi kisheria who goes to other business and leaves with their records, that’s just crime and abuse of power.

Hii nchi ni rahisi kutabili outcome zake on what will follow maana maamuzi ya viongozi huwa hayafanyiwi risk assessment kwanza, kauli za mama kuna watu walishaona zitaleta shida mbele anatuma salamu sizo kwenye jamii na walipa kodi.
 
Tulia sindano iwaingie! kuna watu hawawezi ustaarabu!! Wanachukulia ustaarabu wa mama kuwa ni unyonge! Ghafla unakuta watu wanaanza kujivuta kulipa kodi, wamezoea kulazimishwa! Mama alishasema toka mapema, timiza wajibu wako, ukinizingua tunazinguana!! Hao jamaa itakuwa wamezingua na sasa ni mwendo wa kuzinguana tu! Wanataka wasilipe kodi stahiki, halafu kesho na keshokutwa hao hao watasema mbona kasi ya maendeleo imepungua? Safi sana TRA chini ya uongozi wa mama.
 
TRA wangekuwa wanafanya random sampling za Z Report kuangalia kama kuna discrepancies/variation significant halafu wa take to task hao walipa kodi. Huhitaji kufanya physical verification initially . Tumia technology vizuri.
 
Hiyo ni kazi yao na wanaijua vizuri. Msihukumu kwa haraka, mpaka TRA wamechukua hatua hiyo lazima huyu mlipa kodi atakuwa na ujeuri fulani. Nchi hii kuna udanganyifu mkubwa sana wa kodi! na kazi ya TRA ni ngumu sana! Kuna watu hawawezi kabisa ustaarabu, watu wa namna hiyo ndio wale mama alisema ukinizingua tunazinguana!! Sasa ukiandaa mazingira ya kuzinguana, usije hapa na kuanza kulia lia!!
 
Asante kiongozi kwa kutoa elimu.......tatizo kubwa la nchi yetu ni wanasiasa....

Wanasiasa wetu wanapigania maslahi yao ya kisiasa hata kama itagharimu damu ya mtu..........

Tunatakiwa kama taifa ili tusonge mbele lazima tujue ni wakati gani wa kutenganisha siasa na mambo ya kitaaluma na weledi......tuna wanasiasa waropokaji......na sio wajenga hoja za msingi za kuliinua taifa...
 
watu wanadharau demand notice na simu, huo ni ujinga, hata kama unadaiwa nenda kaongee nao, wakati mwingine tunalaumu TRA kumbe ni maudhi ya kampuni yenyewe, na si kila kodi inasubiri hadi mwaka ndo ulipe, unawakata watu paye afu hutaki kulipa
Umesema vizuri sana! Siamini kuwa TRA wamekuja tu from nowhere na kuvamia na kuchukua vielelezo. Lazima wamekutana na usumbufu na ukorofi usio wa kawaida!
 
Na wakwepa kodi wakubwa ndiohao hao wafanya biashara wakubwa wenye fursa ya kumuona na kupeleka malalamiko yao kwake.
 
Nafikiri kama ungejua sababu mada ingekuwa nzuri. Sababu kwa upande wa wafanyabiashara pia kuna tatizo, kwani ni mara ngap TRA wamefanya unyama huo?

Sina uelewa sana kuhusu utaratibu wa namna wanavyomshika mtu au vurugu za namna hyo.

Kwa upande wangu, mzee wangu alishawahi kupata shida kama hiyo ila nikajaribu kufuatilia kiini ikaonekana mzee hakujibu barua za TRA ambazo zilimtaka kukamilisha madeni yake.
 
Mama kasema angependa kuona tukilipa kodi halali kwa hiyari bili shurti, hajasema tukwepe Kodi au tulipe chini ya kiwango
"Maneno yangu tutekeleze hiyari kwa uaminifu mkubwa, serikali ina mamlaka ya kutumia shurti pale inapobidi"
Hakuna wa kulipa Kodi bila shuruti
 
Lipeni kodi acha majungu mbwiga we!
 
Hawa watu ni Tatizo ktk hii nchi, Raisi aweke wakurugenzi kutoka nje kama Majirani zetu ambao wana weledi wa namna ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya wafanya biashara na Serekali, kuweka mifumo ya kieletronic ili walipa kodi wasionane na hwa watu, na waondolewe kinga ya kutokushitakiwa wanapobambikia watu kodi na wakivamia maofisi ya watu washitakiwe kama wao na si Serikali
 
sasa hivi hata petrol station hazitoi risiti tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…