TRA ni SHIDA: Wavamia Ofisi hapa Viwandani

Ndugu huu utakuwa wivu sasa. Mtawaonea sana viongozi wa tra , tulipe kodi ndugu zangu tunazostahili sidhani kama kutakuwa na mgogoro au malalamiko yoyote. Tujiulize ITV hapo kuna viwanda vingapi kwanini awe huyo tu?
Hakuna anayekataa kulipa kod ila iwe halali na wao waelewe kama kipindi hiki cha korona biashara zimeyumba, wengine wanafilisika, na kiwanda sio cha kuvamia ni kumuita mwenye kiwanda wakae mezani waongee, Kuvamia ni kujenga picture mbaya kwa nchi
 
Huu wimbo wa kulipa kodi bila shuruti hauna mwitikiaji. Waulize wanaolipa kodi wakuambie kama kinachowasukjm0
Asiyelipa kodi ni jambazi! Tusimung'unye maneno katjka hili! Anafanya serikali ishindwe kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia watanzania!! Kwa hiyo akivamiwa ka a jambazi ni sahihi kabisa!
 
Hakuna anayekataa kulipa kod ila iwe halali na wao waelewe kama kipindi hiki cha korona biashara zimeyumba, wengine wanafilisika, na kiwanda sio cha kuvamia ni kumuita mwenye kiwanda wakae mezani waongee, Kuvamia ni kujenga picture mbaya kwa nchi
Mtu akivamiwa ujuwe njia zote za kistaarabu zimegonga mwamba!! Kwani wafanyabiashara wote wanavamiwa?
 
Hivi hata kodi ikiwa ndogo watu watakwepa kulipa kodi?

Kwa sababu kuna mtu alisema Mtanzania hayupo tayari kulipa kodi. Kama ndiyo hivyo, basi tuanze kuwafundisha umuhimu wa kodi wanafunzi tangu wakiwa chekechea, labda itasaidia!
 
Waache waendelee kupiga makofi na vigelegele, kuvuna mabua ni suala la wakati tu.
 

Umesema sawa lkn shida ni nidhamu ya pesa za umma wao wana nidhamu nasi hatuna kwa ubinafsi wetu na ndo maana hata usimamiaji wa rasilimali za nchi sie tupo nyuma na mfano nchi za Asia na mashariki ya kati nyingi baada ya uhuru tulikuwa tupo sawa au tunakaribiana lkn ona gap walio tuacha na hapa ni kusimamia vizuri rasilimali zao, mafuta nk

Tumeiga/ku copy demokarasia lkn je ktk hali halisi je tunaishi na kutenda kama inavyotakiwa hata kwa zile haki tu za msingi kama ( kuchagua, kutoa maoni, kuandamana ) kwahiyo ku copy suala moja kuishi kulingana na unacho copy ni suala jingine
 
Hiyo kauli inakera sana, siku moja nilimuuliza mfanyabiashara hiyo sheria ya kuwa ukiuza bei ya jumla hautoi risti uliitoa wapi? jamaa akaangalia chini.
 

Huko unakosema kwa wenzetu; kodi inatumika kwa maendeleo ya watu wenyewe yaani walipa kodi, lakini hapa kwetu kodi haitumiki hivyo bali hutumika kuwanenepesha wabunge na wakubwa serikalini!!! Si umeona jinsi Viongozi wa hazina walivyojichotea mahela kama vile ni za Bahati nasibu!! Sasa namna hiyo motisha ya kulipa kodi itatoka wapi?

Matumizi mabaya ya fedha na seriklia ndio yanafanya watu wakwepe kulipa kodi. Leo hii serikali kabla ya kufanya mabadiliko yaliyopendekezwa na CAG inakwenda pitisha matumizi ya kununua ndege mpya kwa ATCL; shirika ambalo CAG amelieonesha kuwa linatia hasara nchi!!! Je serikali inategemea kupata matokeo tofauti iwapo waliohusika kulitia hasara shirika wataendelea kuliongoza? Serikali lazima ijitathmini inaisichukulie kuwa wananchi ni watu wa kupuuzwa.

Hata kama serikali itachukua madeni yote ya ATCL, ijulikane wazi kuwa bila kulifanyia mabadiliko ya msingi kiuongozi hilo shirika hakuna faida itakayopatikana kwa miongo mingi ijayo!!!
 
Wakwepa kodi ni mafioso
 
Mkuu Nyani Ngabu, ebu tusaidie kuelewa TRA ya huko unyamwezini (IRS) inafanyaje kazi? Kwa kusikia kwangu ni kwamba hao jamaa ni moto wa kuotea masafa.
 
Acha porojo. Kodi inalipwa kwa mujibu wa sheria siyo kwa mujibu wa matumizi. Ingekuwa hivyo basi marekani wangeshaacha kulipa kodi kwa sababu matumizi ya majeshi ya marekani hakuna anayejua na idara ya ulinzi haikaguliwi!
 
Mwenye akili nyingi mbona alishindwa kuzuia mdororo wa uchumi hata "mkaanza kubariki uporaji kwenye akaunti za watu..." jifunzeni KRA na URA wanafanyaje kazi hapo sio mbali.
Ikiwa watafuta kazi na wanaotafutiwa na vigogo wote wanataka kila mmoja aajiriwe TRA basi kuna jambo hapo...
 
Elimu ya kodi na umuhimu wa kodi vilipaswa kutolewa tangu elimu ya awali (watoto wanapofunzwa uzalendo wajue umuhimu wa kodi kwa taifa lao) sasa hii taabu ya kumfunza mbwa mzee kuwinda inatugharimu....
 

Hawa tiaraei saa zingine ni wa kupiga tu
 
Acha porojo. Kodi inalipwa kwa mujibu wa sheria siyo kwa mujibu wa matumizi. Ingekuwa hivyo basi marekani wangeshaacha kulipa kodi kwa sababu matumizi ya majeshi ya marekani hakuna anayejua na idara ya ulinzi haikaguliwi!

Kwani ATCL ni Jeshi mbona unajitoa ufahamu!!! Nani kauliza matumizi ya TPDF? Je wewe unategemea matokeo tofauti kwa kuwatumia watu wale wale waliolifikisha hilo shirika hapo lilipo? Usilinganishe mambo ya marekani na huku ambako mpaka leo shule zenu hazina mashimo ya vyoo!!!!
 
Inaelekea wewe fasihi ulifeli kabisa. Unajadilije mfano unaacha point yenyewe? Kweli chadema kazi wanayo. Nimesema kodi inalipwa kwa mujibu wa sheria siyo kwa mujibu wa matumizi. Watu wengine wagumu kuelewa!
 
Nimesema kodi inalipwa kwa mujibu wa sheria siyo kwa mujibu wa matumizi

Unajua kuna watu wanakwepa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria!!! Have you ever heard of TAX AVOIDANCE? Find out why people avoid paying taxes!!!
 
Hujui hiyo nguo kabla ya kufika hapo dukani imelipiwa kodi ngapi. Mfumo wa kodi Tanzania ni very complicated. Kama hujawahi kufanya biashara utamuona huyo dada ni mwizi.
 
Kuhus ATCL wewe unaangalia faida kwa namba zilizomo ndani ya vitabu vya mahesabu ya ATCL, lakini huangalaii strategic advantages kwa nchi. Ukitaka shirika la ndege ambalo vitabu vyake vinaonyesha faida, basi hutakuwa na shirika lolote la ndege za abiria afrika, mashariki ya kati na asia isipokuwa Ethiopan na Emirates tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…