TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Namtaka rais wa bodaboda aje atoe tamko, pumbavu kabisa wamekula kitu kizito na ushabiki wao kwa CCM wa kijinga
 
Sawa na TSh.193 kwa siku,TSh.1,350 kwa wiki,TSh.5,400 kwa mwezi na TSh.65,000 kwa mwaka...
 
Hiyo Kodi Ni ndogo Sana Hawa vijana ndio walio andamana kuunga mkono bandari kuuzaa kwa dp world SAS nasema mm nikija kuwa mtendaji mkuu wa mamlaka hyo nitawap akiwango Cha laki tatu kwa mwaka Hadi warudi mashambani wakalime
 
Mama anaupiga mwingi
 
Serikali iliwapamba na sifa lukuki kumbe ilikuwa inawalia timing iwapige na kitu kizito[emoji3]
 
Kwa nini jamaa huyo alizungumzie hili Simiyu?
 
Umeshawahi kuwa dereva bodaboda mpaka useme hicho kiwango ni kidogo?
Mikataba ya pikipiki.gn miezi 12_14.boxer ndio balaa miezi 17 ..sumatra.bima .bado haitoshi imekuja 65000 nishida tupu kwa bodaboda hata huruma hamna.usalama wake mdogo akiwa barabarani kweli kujiajiri sijui ina maana gani...
 
Your browser is not able to display this video.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mabadiliko ya Sheria za kodi mwaka 2023, serikali imeweka kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki zenye magurudumu mawili (Bodaboda) ambapo watatakiwa kulipa kiasi cha Sh. 65,000 kwa Mwaka.

Hayo yamesemwa Agosti 10, 2023 na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hamad Mterry, wakati akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu.

Mterry amesema kuwa hiyo ni moja ya sheria ya kodi ambayo ni mpya na imewagusa Bodaboda, ambapo watatakiwa kuichagia serikali kiasi cha Sh. 65,000 kwa mwaka, kuanzia mwaka huu wa fedha ambao tayari umeanza tangu Julai Mosi, 2023.
Afisa Mawasiliano na elimu kwa umma kutoka (TRA) Mkoa wa Simiyu, Benjamin John amesema kuwa Bodaboda anaweza kulipa kodi hiyo kwa awamu nne ndani ya mwaka, ambapo kila awamu atatakiwa kulipa Sh. 16,250.

Hata hivyo wafanyabiashara za kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) wanaona kodi hiyo inakwenda kuongeza ugumu wa maisha kwao, kutokana na kipato chao cha kila siku kuwa kidogo sana.

“ Ukizingatia kwa sasa kupata Sh. 10,000 kwa siku ni ngumu sana, lakini mafuta yamepanda bei, tunalipa LATRA, tunalipa Bima, bado familia inakutegemea, leo tumeletewa TRA, ukweli kodi hii inakwenda kutuumiza sana,” amesema Ntoni Deus.

Source: Global TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…