TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Inabidi na wazururaji tulipe kodi, tumesahauliwa, na Riverside walipe kodi, wachoma mahindi na mihogo walipe kodi
 
Bodaboda mmesikia hii? Sasa rasmi mtaanza kulipa Kodi. Hapa Serikali mmechemka na mnawaonea Bodaboda, maana kupata 20,000 kwa siku ni kazi kubwa ila Nchi itajengwa na Watanzania wote.

----
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mabadiliko ya Sheria za kodi mwaka 2023, serikali imeweka kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki zenye magurudumu mawili (Bodaboda) ambapo watatakiwa kulipa kiasi cha Sh. 65,000 kwa Mwaka.

Hayo yamesemwa jana na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hamad Mterry, wakati akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu.

Mterry amesema kuwa hiyo ni moja ya sheria ya kodi ambayo ni mpya na imewagusa Bodaboda, ambapo watatakiwa kuichagia serikali kiasi cha Sh. 65,000 kwa mwaka, kuanzia mwaka huu wa fedha ambao tayari umeanza tangu Julai Mosi, 2023.

Afisa Mawasiliano na elimu kwa umma kutoka (TRA) Mkoa wa Simiyu, Benjamin John amesema kuwa Bodaboda anaweza kulipa kodi hiyo kwa awamu nne ndani ya mwaka, ambapo kila awamu atatakiwa kulipa Sh. 16,250.

Hata hivyo wafanyabiashara za kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) wanaona kodi hiyo inakwenda kuongeza ugumu wa maisha kwao, kutokana na kipato chao cha kila siku kuwa kidogo sana.

“ Ukizingatia kwa sasa kupata Sh. 10,000 kwa siku ni ngumu sana, lakini mafuta yamepanda bei, tunalipa LATRA, tunalipa Bima, bado familia inakutegemea, leo tumeletewa TRA, ukweli kodi hii inakwenda kutuumiza sana,” amesema Ntoni Deus.

My Take
Naunga mkono,Pia pombe na Sigara ziongezewe Kodi.View attachment 2714625
Vyombo vyote vya moto lazima vilipe kodi, huu si uonezi. Bodaboda hukusanya pesa nyingi kwa mwaka ndiyo sababu mtu mmoja anaweza kununua bodaboda za ziada.
 
Mafundi ujenzi wanatumia barabara za kurekebishwa, umekosa hoja acha chuki kwa wajenzi wavuja jasho wanakula kwa nguvu zao.
Nani anapata hela bila kuvuja jasho? Serikali hakikisheni Kila fundi ujenzi ana leseni ,walipe Kodi na wachangie mapato
 
Rais Samia futa hili pendekezo linakuletea shida zisizo na sababu na bodaboda japo Huwa hawapigi kura.

Nawasaidia afadhari mafundi ujenzi wote wawe na leseni za ujenzi ndio walipe 100,000 Kwa mwaka.

Wacha walipe tu wewe unadhani V8 new model tutawezaje kununua? Na kwny msafara hazitakiwi kupungua 10
 
Nani anapata hela bila kuvuja jasho? Serikali hakikisheni Kila fundi ujenzi ana leseni ,walipe Kodi na wachangie mapato
Wakandarasi nao si wajenzi kwani hawalipi Kodi, washazungumzia bodaboda ya wajenzi ya kwako, barabara zinarekebishwa, walipie si chombo Cha Moto.
 
Wakandarasi nao si wajenzi kwani hawalipi Kodi, washazungumzia bodaboda ya wajenzi ya kwako, barabara zinarekebishwa, walipie si chombo Cha Moto.
Kama mkandarasi analipa,mama ntilie analipa,boda analipa Kwa nini wewe fundi usilipe?
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.

Kulipa kodi ni jambo la muhimu LAKINI kodi inapotumika kufsnyia anasa watawala wakati walipaji wanashindwa kupata hata mahitaji ya lazima, uhalali wa kulipa kodi unapotea.
 
Back
Top Bottom