Kashishi yetu
JF-Expert Member
- Mar 22, 2014
- 3,509
- 3,741
Kama ni ya kutembelea wewe mwenyewe hapo inakuwaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii tunazungumzia kodi ni sababu tosha na ni wajibu,hao wanaoshindwa kutoa buku 3 kwa mpesa wapigwe viboko au wawekwe ndaniHiyo hela ni kubwa sana hasa kwa bodaboda!
Kuna watu wanafunga mwaka hawana hata akiba ya 10000 na wamefanya kazi mwaka mzima.
Kuna sehemu tuliambiwa tulipe 3000 kwa mwezi huku uswahilini na bado watu hawapati hiyo hela, ambapo ni wastani wa shilingi 100 kwa siku.
Kuitoa 3000 kwa pamoja bila sababu zinazoeleweka ni ngumu sana kwa watu wa uchumi fulani.
Na watoto wote wanaozaliwa salama katika hospitali za serikali watalipiwa kodiWanafunzi nao waanze kulipa kodi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi waanze kulipa kodi.
Nchi yoyote inayotegemea KODI na TOZO kwaajili ya maendeleo ni nchi ILIYOKUFAHiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.
Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.
Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
walipe tu....serikali iliwapa jina la maafisa usafirishajiBodaboda mmesikia hii? Sasa rasmi mtaanza kulipa Kodi. Hapa Serikali mmechemka na mnawaonea Bodaboda, maana kupata 20,000 kwa siku ni kazi kubwa ila Nchi itajengwa na Watanzania wote.
----
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mabadiliko ya Sheria za kodi mwaka 2023, serikali imeweka kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki zenye magurudumu mawili (Bodaboda) ambapo watatakiwa kulipa kiasi cha Sh. 65,000 kwa Mwaka.
Hayo yamesemwa jana na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hamad Mterry, wakati akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu.
Mterry amesema kuwa hiyo ni moja ya sheria ya kodi ambayo ni mpya na imewagusa Bodaboda, ambapo watatakiwa kuichagia serikali kiasi cha Sh. 65,000 kwa mwaka, kuanzia mwaka huu wa fedha ambao tayari umeanza tangu Julai Mosi, 2023.
Afisa Mawasiliano na elimu kwa umma kutoka (TRA) Mkoa wa Simiyu, Benjamin John amesema kuwa Bodaboda anaweza kulipa kodi hiyo kwa awamu nne ndani ya mwaka, ambapo kila awamu atatakiwa kulipa Sh. 16,250.
Hata hivyo wafanyabiashara za kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) wanaona kodi hiyo inakwenda kuongeza ugumu wa maisha kwao, kutokana na kipato chao cha kila siku kuwa kidogo sana.
“ Ukizingatia kwa sasa kupata Sh. 10,000 kwa siku ni ngumu sana, lakini mafuta yamepanda bei, tunalipa LATRA, tunalipa Bima, bado familia inakutegemea, leo tumeletewa TRA, ukweli kodi hii inakwenda kutuumiza sana,” amesema Ntoni Deus.
My Take
Naunga mkono,Pia pombe na Sigara ziongezewe Kodi.View attachment 2714625
Siyo kweli kwamba hakuna anayependa kulipa kodi.Iko hivi, mifumo yao hauwezi kuilinganisha na huku, usipolipa kodi ulaya maisha yako yatasimama na hauwezi kuishi, lkn kwetu haulipi kodi na unaishi vizuri tu.Hakuna apendaye kulipa kodi duniani kote.Mfumo unawalazimisha wala sio hiali yao, mfano kwa sasa tunalipa kodi ya majengo lkn ulishasikia mtz anagombana na serikali kuhusu hiyo kodi? Kama hautaki kuilipa hiyo kodi basi usiweke umeme nyumbani kwako, je utakuwa na maisha ya namna gani? Sasa ulaya mifumo ya hivyo ni mingi huna pakuchomokea unabanwa kila kona na kodi utailipa tu, Gas, maji, umeme huduma za benki, kadi za usafiri, bima nk utalipa tu upende usipende. Huku watu wanaishi kama mang'ombe halafu unawafuata polini eti unataka maziwa ndoo 5 kwa kila ng'ombe.
Kulipa kodi watu hajakataa ila hiyo kodi inaenda kufanya nini ndio changamoto kwa serikali zetu za kiafrikaHiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.
Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.
Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Nilijua tu baada ya bandari kuuziwa mwaarabu, hakuna kitega uchumi kwasasa.Wanafunzi nao waanze kulipa kodi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi waanze kulipa kodi.
Shida siyo kulipa kodi. Shida ni vipato vya wananchi.Siyo kweli kwamba hakuna anayependa kulipa kodi.
Hapa ninapoishi Marekani kodi za nyumba ndiyo zinaendesha shule za msingi na sekondari.
Na zinaendesha shule vizuri tu.
Lakini kuna wazazi wengi huchangia mifuko mbalimbali ya kuboresha mambo ya elimu, bila kushurutishwa kufanya hivyo, kwa kueleea umuhimu wa elimu.
Ukitaka kuelewa habari hizi kwa upananzaidi soma kitabu cha Robert D. Putnam "Our Kids: The American Dream in Crisis" kaongelea sana jambo hili.
Hivyo, habari yako kwamba hakuna mtu anapendankulipa kodi si kweli.
Huku tulipo kuna watu wanalipa kodi mpaka nyingine za kujiwekea wenyewe juu ya kodi za serikali.
Hakuna chanzo cha hela. Bandari imeuzwa kwahiyo kitega uchumi ni watu.Kulipa kodi watu hajakataa ila hiyo kodi inaenda kufanya nini ndio changamoto kwa serikali zetu za kiafrika
Exactly.Shida siyo kulipa kodi. Shida ni vipato vya wananchi.
Ugali dagaa 1500 watu wanalalamika bei kubwa.
Marekani kuna vyanzo vya pesa vingi sana, unaweza kutengeneza application na ukawa una watoza watu kwa USD 1 sawa na 2300 ya kitanzania na ukapokea pesa kutoka mataifa yote duniani. Kwa Tanzania kupokea pesa shilingi 2300 kutoka Ghana, ukiweza kujibeba utaweza kupokea hiyo hela.
Tanzania ni masikini sana.
Na maendeleo hayo lazima yaonekane dhahili kwa macho ya nyamaHiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.
Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.
Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Hiyo 200 unaiona ndogo kwa kuwa upo kwenye mzunguko wa pesa.Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.
Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.
Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Mafundi atotoi ata Mia Yani tuwajengee majumba yao alafu tulipe Kodi bodaboda hawapandi ndomana wanawaoneleaRais Samia futa hili pendekezo linakuletea shida zisizo na sababu na bodaboda japo Huwa hawapigi kura.
Nawasaidia afadhari mafundi ujenzi wote wawe na leseni za ujenzi ndio walipe 100,000 Kwa mwaka.
Unawajengea Bure? Lazima.kufanya kazi kwa.leseni kama huna huruhusiwi kufanya kazi za ujenziMafundi atotoi ata Mia Yani tuwajengee majumba yao alafu tulipe Kodi bodaboda hawapandi ndomana wanawaonelea
Fundi atufanyi kazi kila siku kwa mwezi unafanya kazi wiki mbili alafu ulipe KodiUnawajengea Bure? Lazima.kufanya kazi kwa.leseni kama huna huruhusiwi kufanya kazi za ujenzi
Kama kipindi kile. Samia anatoa hela kuwapa simba na yanga kwa kila goli. Siyo mbayaExactly.
Ndiyo point niliyoitaja hapo juu. Kukiwa na kazi nzuri, nyingi, halafu kodi zinatumika vizuri kwenye mipango ya jamii, watu wengi watalipa kodi bila kinyongo.
Tatizo kazi hakuna, watu wanajiongeza wenyewe, wanapigana, serikali inakuja tu kukusanya kodi, na kodi yenyewe hatuoni inafanya nini.
Lazima watu wasipende kulipa kodi.
Chumba 30,000 kwa mwezi. Ni sawa na shiling 1000 lakn ikifika mwezi watu hawana hela.Hiyo 200 unaiona ndogo kwa kuwa upo kwenye mzunguko wa pesa.
Kuna nyumba sh 1000 inaweza tafutwa wiki .