TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Hii tunazungumzia kodi ni sababu tosha na ni wajibu,hao wanaoshindwa kutoa buku 3 kwa mpesa wapigwe viboko au wawekwe ndani
 
Wanafunzi nao waanze kulipa kodi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi waanze kulipa kodi.
Na watoto wote wanaozaliwa salama katika hospitali za serikali watalipiwa kodi

Hili hailitawagusa watoto njiti
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Nchi yoyote inayotegemea KODI na TOZO kwaajili ya maendeleo ni nchi ILIYOKUFA

Serikali imara inategemea uzalishaji wa malighafi, Elimu na Teknolojia ili kupata mapato kupitia exportation of products or services
 
walipe tu....serikali iliwapa jina la maafisa usafirishaji
 
Siyo kweli kwamba hakuna anayependa kulipa kodi.

Hapa ninapoishi Marekani kodi za nyumba ndiyo zinaendesha shule za msingi na sekondari.

Na zinaendesha shule vizuri tu.

Lakini kuna wazazi wengi huchangia mifuko mbalimbali ya kuboresha mambo ya elimu, bila kushurutishwa kufanya hivyo, kwa kueleea umuhimu wa elimu.

Ukitaka kuelewa habari hizi kwa upananzaidi soma kitabu cha Robert D. Putnam "Our Kids: The American Dream in Crisis" kaongelea sana jambo hili.

Hivyo, habari yako kwamba hakuna mtu anapendankulipa kodi si kweli.

Huku tulipo kuna watu wanalipa kodi mpaka nyingine za kujiwekea wenyewe juu ya kodi za serikali.
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Kulipa kodi watu hajakataa ila hiyo kodi inaenda kufanya nini ndio changamoto kwa serikali zetu za kiafrika
 
Wanafunzi nao waanze kulipa kodi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi waanze kulipa kodi.
Nilijua tu baada ya bandari kuuziwa mwaarabu, hakuna kitega uchumi kwasasa.
Usifurahie sana, kuna kodi nyingine inakuja
 
Shida siyo kulipa kodi. Shida ni vipato vya wananchi.
Ugali dagaa 1500 watu wanalalamika bei kubwa.
Marekani kuna vyanzo vya pesa vingi sana, unaweza kutengeneza application na ukawa una watoza watu kwa USD 1 sawa na 2300 ya kitanzania na ukapokea pesa kutoka mataifa yote duniani. Kwa Tanzania kupokea pesa shilingi 2300 kutoka Ghana, ukiweza kujibeba utaweza kupokea hiyo hela.
Tanzania ni masikini sana.
 
Kulipa kodi watu hajakataa ila hiyo kodi inaenda kufanya nini ndio changamoto kwa serikali zetu za kiafrika
Hakuna chanzo cha hela. Bandari imeuzwa kwahiyo kitega uchumi ni watu.
Wauze na ziwa viktoria ili tuheshimiane
 
Exactly.

Ndiyo point niliyoitaja hapo juu. Kukiwa na kazi nzuri, nyingi, halafu kodi zinatumika vizuri kwenye mipango ya jamii, watu wengi watalipa kodi bila kinyongo.

Tatizo kazi hakuna, watu wanajiongeza wenyewe, wanapigana, serikali inakuja tu kukusanya kodi, na kodi yenyewe hatuoni inafanya nini.

Lazima watu wasipende kulipa kodi.
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Na maendeleo hayo lazima yaonekane dhahili kwa macho ya nyama
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Hiyo 200 unaiona ndogo kwa kuwa upo kwenye mzunguko wa pesa.
Kuna nyumba sh 1000 inaweza tafutwa wiki .
 
Rais Samia futa hili pendekezo linakuletea shida zisizo na sababu na bodaboda japo Huwa hawapigi kura.

Nawasaidia afadhari mafundi ujenzi wote wawe na leseni za ujenzi ndio walipe 100,000 Kwa mwaka.
Mafundi atotoi ata Mia Yani tuwajengee majumba yao alafu tulipe Kodi bodaboda hawapandi ndomana wanawaonelea
 
Mafundi atotoi ata Mia Yani tuwajengee majumba yao alafu tulipe Kodi bodaboda hawapandi ndomana wanawaonelea
Unawajengea Bure? Lazima.kufanya kazi kwa.leseni kama huna huruhusiwi kufanya kazi za ujenzi
 
Kama kipindi kile. Samia anatoa hela kuwapa simba na yanga kwa kila goli. Siyo mbaya
Ila ni pale unafamilia nyumbani umeicha hakuna unga halafu unaenda kuwanunulia marafiki bia. Tuna shule hazina choo, vitabu na madawati.
Katika nchi hii, kuna watu wanapokea mshahara wa 30,000 kwa mwezi (beki), wengine kwa siku wanalipwa 3,000 kwa mwezi 90,000 na wengine 120,000 kwa mwezi, na wengine ni 150,000 kwa mwezi.
Watu hawa ni wengi sana Tanzania ndiyo wananchi.
Sasa unamtoza kodi unafikiri atakuelewa?
Kama Tanzania inataka kodi iboreshe maisha ya watu kiuchumi kama
1. Kupunguza kodi / tozo kwenye biashara
2. Kuweka fursa za wananchi kupata ajira kama baadhi ya sekta kuziendesha zenyewe mfano kuchimba dhahabu, almasi, bandari, gesi n.k hii itafanya hela ibaki hapa hapa Tanzania
3. Kilimo
4. Kuboresha mifumo ya upokeaji hela kutoka nje ya nchi kama kuruhusu kupokea pesa kutoka payapal. Hii itasaidia watu kufanya biashara nje ya nchi na kupokea pesa kutoka kwenye zote duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…