KERO TRA Temeke ni changamoto sana kwenye ufanyaji wao wa kazi

KERO TRA Temeke ni changamoto sana kwenye ufanyaji wao wa kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

sued's

Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
13
Reaction score
13
Wakuu nimekuja kwenu, ofisi za TRA Temeke zina fikirisha sanaa katika uwajibikaji wao

Nili-register TRA TIN Number mwaka 2020 branch ya Mbagala sasa nataka nihamishe ile TIN number location isome Ilala hapo ndo kimbembe aisee

Hawa jamaa nimefanya process zotee online barua nimeandika na nilianza ofisi zao kuu za Kanda ya Temeke nilijibiwa na kupangiwa mtu wa kumaliza hii process aisee pale ofisi za Kanda ya Temeke kuna kijana mmoja walio wahi pita pale wanaweza kumfahamu ni ana kaumaarufu kidogo

Yulee jamaa alinizungusha na kunipangia ratiba kila uchao miezi miwili imepita anakuja kuniambia kuwa niende brach ya Mbagala niliyo fungulia

Nikaenda na nilipo enda huko Mbagala nikaandika barua upya na kujaza fomu na kumaliza yote yanayo takiwa daahh ila ni yale yale tu huku sasa kuna mwana dada aisee ni kama yulee kijana wa kule banda la ngozi sasa nakata kwezi wa tatu huu sijafanikiwa mpaka leo kuchange location ya tin number yangu kutoka temeke kwenda ilala.
 
Nenda mkoani onana na meneja, achana na hao vijana, onana na meneja, wambie kama hawataki hautalipa kodi.
 
Mkuu,

Tunapoandika barua, tukipigwa siasa na afisa aliyepangiwa kufanyia kazi barua zetu tujifunze kuandika barua nyingine ukicc barua iliyopita. Kwa uzoefu wangu, barua ya pili ikirejea kutokufanyiwa kazi kwa barua ya kwanza huwa inashtua maafisa.

Siasa za mdomoni hazina ushahidi ndo maana hawaogopi kukupiga siasa hata miezi. Baadae akiulizwa atasema tu hukufata maelekezo au hukuonekana tena ulipoambiwa rudi kesho yake.

Ukiona jambo haliishi halafu ukataka kujua maelekezo unayopewa kama ni siasa we muulize huyo afisa unaweza nijibu hichi unachonielekeza kwa maandishi rasmi? Ukiona anaruka ruka jua ni siasa au anatengeneza mazingira ya rushwa.
Hapo wewe andika barua nyingine usipoteze muda au muone meneja mwambie unakwamishwa kuendelea na shughuli zinazosaidia wewe kulipa kodi.
 
Nimekuelewaa sanaa sanaa ndugu yangu nashukuru mno🙏🏻
 
Wanataka ya maji ila ndo vile mteja hujiongezi
 
Nenda mkoani onana na meneja, achana na hao vijana, onana na meneja, wambie kama hawataki hautalipa kodi.

Kuna wakati najiuliza hawa wengine wamepataje kazi kwenye ofisi za umma. Mbona kama wamekaa kimisheni town?
 
Kuna huyu wa TEGETA TRA nilikuwa nafatilia withholding anielkze tuu ntafanya akishanielkza naambiwa kaenda kula toka saa nane mpk kumi afu karudi yupo busy na simu sikioni mara afate maji!!

Nilibd nivumilie tuu nikajua namna ya kuomba control number!
 
Back
Top Bottom