TRA: Ukinunua bidhaa na usipodai risiti utapigwa faini ya kati ya Tsh. 30,000 na Tsh. 1,500,000

TRA: Ukinunua bidhaa na usipodai risiti utapigwa faini ya kati ya Tsh. 30,000 na Tsh. 1,500,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mwongozo wa kisheria kwa wananchi wote kwamba endapo utanunua bidhaa au Huduma ni lazima udai risiti.

Endapo utakamatwa umenunua bidhaa au Huduma na hauna risiti basi utapigwa faini ya kati Tsh. 30,000 na 1,500,000 kwa mujibu wa kanuni za sheria ya kodi.

Kumbuka kudai risiti kila wakati.

Maendeleo hayana vyama!

----
Tra.jpg
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), imesema kuwa wataanza msako katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwakagua na kuwatoza faini wanunuaji wanaonunua bidhaa bila kuomba risiti na wafanyabiashara wanaouza bidhaa bila kutoa risiti.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Januari 7, 2021, na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Richard Kayombo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio.

"Kama hautachukua risiti kwenye huduma ama bidhaaa yoyote uliyonunua ambayo inatakiwa kutolewa risiti, unaweza ukatozwa faini ya shilingi 30,000 au Milioni 1.5", amesema Kayombo.

Aidha akizungumzia kuhusu wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu, Kayombo amesema kuwa, "Kama umeuza bidhaa lakini hujatoa risiti adhabu yako ni kati ya Mil. 3 hadi Mil. 4.5 iwe umetoa risiti ya udanganyifu adhabu hiyo inakuhusu au unayo mashine lakini hauitumii".
 
Na bado, JK aliendesha nchi vizuri na alikuwa anakusanya bil 900 ,nyinyi mnaokusanya Trilioni 2 mnanyonya damu wananchi ,bado kodi ya "KUWEZANA" tu ndio TRA wamebakiza.
Bwashee usisahau kudai risiti kila ufanyapo manunuzi!
 
Jamaa sasa wanabuni kila njia ya kukusanya mapato ile SGR ikamilike, ile ya uhujumu uchumi na kuongea na DPP wameona inaanza kupwaya, watuhumiwa wanakaribia kwisha magerezani.
 
Jamaa sasa wanabuni kila njia ya kukusanya mapato ile SGR ikamilike, ile ya uhujumu uchumi na kuongea na DPP wameona inaanza kupwaya.
Cha muhimu usisahau kudai risiti kila wakati!
 
Warumi13​

1 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.

4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu.

5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala.

7 Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.

Qur'ani
"Enyi mlioamini Mtiini Allah, na mtiini Rasuli (Wake Muhammad) na Wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu, ......" (Qur'ani, 4:59)
 
Bwashee usisahau kudai risiti kila ufanyapo manunuzi!

Bwasheee hiyo kodi mimi hainisaidii hata kidogo maana huku napokaa umeme natumia wa solar na maji nimechimba kisima, barabara hazipitiki kipindi cha mvua, bombadia sijawahi kupanda kwahiyo kodi yenu sijawahi kuitumia, risiti kwangu ni option siwezi kudai bora kodi achikichie mfanyabiashara ataongeza mzunguko kuliko mchukue nyinyi mnaenda kuendeleza GBADOLITE ya CHATTLE.
 
Warumi13​

1 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu...
Mungu wa dunia ndio anataka mamlaka iliyopatikana kwa kura za kwenye mabegi meusi iheshimiwe.

Mungu wa kweli anatuasa tusiibe.
 
Bwasheee hiyo kodi mimi hainisaidii hata kidogo maana huku napokaa umeme natumia wa solar na maji nimechimba kisima,barabara hazipitiki kipindi cha mvua,bombadia sijawahi kupanda kwahiyo kodi yenu sijawahi kuitumia,risiti kwangu ni option siwezi kudai bora kodi achikichie mfanyabiashara ataongeza mzunguko kuliko mchukue nyinyi mnaenda kuendeleza GBADOLITE ya CHATTLE.
Omba tu risiti wakati wote ndugu yangu maana Ukipatikana utahama huko kwenye umeme wa sola uende kwenye ugali wa bure wa serikali.
 
Mungu wa dunia ndio anataka mamlaka iliyopatikana kwa kura za kwenye mabegi meusi iheshimiwe.

Mungu wa kweli anatuasa tusiibe.

Mungu hakushindwa kuzuia lolote

"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu."

"Enyi mlioamini Mtiini Allah, na mtiini Rasuli (Wake Muhammad) na Wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu, ...... (Qur'ani, 4:59)
 
Jamaa sasa wanabuni kila njia ya kukusanya mapato ile SGR ikamilike, ile ya uhujumu uchumi na kuongea na DPP wameona inaanza kupwaya, watuhumiwa wanakaribia kwisha magerezani.
Watu wataviziwa kama kuku!Hiki ni chanzo kipya cha mapato!

Mambo mengine ni ushamba,faini hiyo ilipaswa apigwe ambaye hajatoa risiti na si mteja!Sio kazi yangu kudai risiti!Ni hiari yangu kufanya hivyo!Ila kwa mtoaji risiti ndio anatakiwa alazimishwe!
 
Bwasheee hiyo kodi mimi hainisaidii hata kidogo maana huku napokaa umeme natumia wa solar na maji nimechimba kisima,barabara hazipitiki kipindi cha mvua,bombadia sijawahi kupanda kwahiyo kodi yenu sijawahi kuitumia,risiti kwangu ni option siwezi kudai bora kodi achikichie mfanyabiashara ataongeza mzunguko kuliko mchukue nyinyi mnaenda kuendeleza GBADOLITE ya CHATTLE.
Sheria itafuata mkondo wake bwashee!
 
Back
Top Bottom