TRA Wakanusha taarifa zilizoandikwa JamiiForums kwamba Mtandao wao Unasumbua, Waziita uzushi

TRA Wakanusha taarifa zilizoandikwa JamiiForums kwamba Mtandao wao Unasumbua, Waziita uzushi

Kuna Taarifa Kutoka TRA wakikanusha Uzushi Ulioletwa Hapa Jamii Forum Kuhusu Mtandao Wa TRA kutofanya Kazi Nchi Nzima. View attachment 1800217

Kuna hili hapa linawahusu na hamjajitokeza kulitolea taarifa kwa umma, je mnalizungumziaje?
 
Najua tarehe tajwa tin ilishindikana kuibadili kutoka ya biashara kuwa ya mtu binafsi kutokana na matatizo ya mtandao. Sasa wafanyakazi wao wanatudanganya wateja, au wakanushaji wajitekenya na kujicheka wenyewe, wanajua linaloendelea? Hiyo ilikuwa Ta, mikoa mingine sijui.
Haya mambo hutokea sana, mtandao huwa unasingiziwa kama wakizidiwa na kazi
 
TRA uongo ni jadi yao ndiyo sababu hawaoni tatizo kuwabambikia Wafanyabishara kodi FAKE au wapewe rushwa ili wapunguze assessment yao FAKE.
Najua tarehe tajwa tin ilishindikana kuibadili kutoka ya biashara kuwa ya mtu binafsi kutokana na matatizo ya mtandao. Sasa wafanyakazi wao wanatudanganya wateja, au wakanushaji wajitekenya na kujicheka wenyewe, wanajua linaloendelea? Hiyo ilikuwa Ta, mikoa mingine sijui.
 
TRA uongo ni jadi yao ndiyo sababu hawaoni tatizo kuwabambikia Wafanyabishara kodi FAKE au wapewe rushwa ili wapunguze assessment yao FAKE.
Ww Huku Ukuwezi, twende Kwenye basketball Mkuu
 
Kesho sijui taasisi gani itasemwa mimi hapa nipo na tax consultant yangu naona mifumo yao TRa ipo sawa na mpaka VAT niliweza kufile ,sasa na hii ya lawson tena kesho tutasikia na lingine.Hebu tuache kidogo kupotosha
Mifumo kusumbua au kufanyiwa marekebisho hilo sio swala la ajabu kijana umeongea na afisa utumishi yeyote aliyeko karibu nawe amekupa jibu gani kuhusiana na lawson?
 
Sio kukanusha tu, rais aingilie kati ajulikane muongo nani kati ya mleta mada na TRA
TRA Wamekanusha Taarifa zilizoandikwa JamiiForums zilizodai Mtandao wao kusumbua.

Wamesema ni taarifa ya Uongo na Uzushi. Kwani imelenga kupotosha na kuleta taharuki miongoni mwa Walipa Kodi pamoja na kuidhalilisha taasisi na Watumishi wake.

Katika kipindi cha mwezi mzima, TRA haikuwa na Hitilafu yoyote.

TRA imewataka Waipa Kodi kuendelea kulipa kodi.

Zaidi, soma; Rais Samia ingilia kati, TRA watatukwamisha

View attachment 1800218

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Kulinda heshima ya JF, huyo aliyeleta taarifa za uzushi bila ya ushahidi wowote asiachwe bila kuwajibishwa kwa njia inayofaa watakayoona inafaa.

JF isifanywe kuwa kituo cha majungu na habari zisizokuwa na ukweli wowote.
 
Iliyoandikwa katika mtandao wa JamiiForums.

Taarifa haijakosewa, wewe ndio umeielewa tofauti
Asante kwa kunisahihisha na Naomba Msamaha kwa mwandishi kwa kuwakosoa pasipo na kosa...
 
Asante kwa kunisahihisha na Naomba Msamaha kwa mwandishi kwa kuwakosoa pasipo na kosa...
Unajua kwa nini tunasema haya mambo huku mitandaoni?

Ni kutokanna na ukiritimba uliojengwa na hizi taasisi, huenda mleta malalamiko alipata changamto kadhaa yeye binafsi akazani tatizo lipo kwa ujumla akaamua kulisema hapa.

Endapo hizi taasisi zingekuwa zinapokea simu kupitia namba zao wanazotuelekeza kuwa ni za dharura, huyu mdau angewapigia na kuwauliza. Kwa kuwa huwa hawapokei hata kama simu ipo hewani(sijui tatizo ni nini) ndio maana inasababisha tuulizie kupitia mitandaoni
 
Back
Top Bottom