TRA wana jambo lao, Sio kwa watu maarufu tu, ndugu yangu alieanza biashara 2015 kwa mara ya kwanza kapigwa faini nzito ya kukwepa kodi,

TRA wana jambo lao, Sio kwa watu maarufu tu, ndugu yangu alieanza biashara 2015 kwa mara ya kwanza kapigwa faini nzito ya kukwepa kodi,

Mkuu,
Achana na uchumi wa makaratasi,
Twende kwenye vitu vyenye uhalisia.

Ndo maana nmekuuliza hivi unajua

1. cement mfuko mmoja unauzwaje nawe unapaswa ukauzeje?

2. Soda/bia kreti moja Inauzwa sh. Ngapi na Ina faida sh ngapi?

3. Sukari kiroba kimoja kinauzwa sh. Ngap,unatakiwa kuuza sh. Ngap na faida itakua Kias gani.

4. Mchele kiroba kimoja kg100 kinanunuliwa sh ngapi, unatakiwa kuuza sh ngapi na faida Kia's gani?

Hivi unadhan wafanyabiashara wakiamua kuuza kwa kutaka faida unazosema wewe kwenye makaratasi, unadhan Kuna mwananchi atalimika uko mtaani?

Au Ndo mtakuja mitandaoni kulalamika makali ya maisha, serikali itangaze Bei elekezi na iweke taski force kukamata na kuonea wafanyabiashara.
Unaongea vitu vipo out of context kuhusu vat na inaonekana wazi hujui hata vat inavyofanya kazi.

Hata mfuko wa cement uuzwe elf 50, kama mtu kanunua kwa risiti ya tra yenye vat na akaenda kuuza kwa kutoa risiti ya tra yenye vat atapata faida + kukomboa vat aliyolipia..

Nilichoona ni kwamba suala zima la vat bado huna elimu ya kutosha.

Halafu kuwa na akili hata kidogo basi, kwa akili yako umeona makampuni makubwa kama ya soda ndio yakwepe vat!! Haupo serious kuwafananisha cocacola / pepsi na wafanyabiashara ambao hawana hata wahasibu.
 
Nimejiridhisha kwamba kwa sasa TRA wana jambo lao kwa wakwepa kodi maana si kwa kelele hizi, wakiona unakwepa wanapita na wewe.

Mwezi uliopitwa nilipatwa na simanzi baada ya kuona ndugu yangu kapatwa na pigo zito la kulipa faini ya TRA, masikitiko yake yamenigusa na mwanzoni nilidhani kaonewa lakini hali ni tofauti.



Hawa kina diamond na huyo pck wanaolalamika ni kwasababu ni maarufu ndio maana wanasikika lakini wakae wakijua sio wao tu, hii ni operation kubwa sana iliyonasa wengi tena kihalali bila uonevu wala mabavu.



Binafsi nina ndugu yangu alianza biashara kwenye mwaka 2015 hivi, Enzi hizo Magu kaingia na msisitizo watu watoe risiti kwa mashine, hapa waliokuwa hawana mashine ndio walikiona cha mtemakuni, kukwepa huu mhaho wengi ilibidi wanunue hizo mashine ila wakawa wanatoa risiti chache za kuzugia, kwa sasa hali ni tofauti kabisa, hio style ya kutoa risiti za kuzugia utapigwa pini tu, yaani kwa sasa wanafatilia mfano biashara za kuuza bidhaa inabidi mzigo ulionunua uwe na risiti yake ya mashine ya tra na pia uwe unauza kwa kutoa risiti kwa mashine, huyu ndugu yangu alipodakwa ni kwamba alikuwa ananunua bidhaa na alikuwa anapewa risiti lakini yeye anatoa tu risiti chache za kuzugia kwa bidhaa alizouza, Tra wakastuka wakaenda dukani kwake kukagua mzigo wakamwambia wameona kwenye system yao anauziwa bidhaa nyingi na watu wanaomuuzia kwa risiti lakini yeye vitu anavyouza kwa risiti ni vichache, mzigo uliobaki uko wapi ? Akaanza kupiga kiswahili pale lakini haikusaidia, TRA wakahitimisha kihalali kwamba anauza bila kutoa risiti a.k.a anasaidia ukwepaji wa kodi.

Wakati anasubiri hatma ya kitachomkuta alitumia connections zake na kwenda kuwabembeleza Tra kwenye ofisi zao lakini wapi... Kwanza hata huko akagundua wapo wengi.

mwezi uliopita kapigwa faini ya takribani milioni 160 kwa kosa la kuuza bidhaa bila kutoa risiti.



Ana bahati hawakufunga akaunti zake ama kumpeleka mahakamani, hadi hapa alipo imebidi aanze kurejesha mdogo mdogo kwa maumivu makali sana, yaani kwa sasa yupo makini sana kuuza bidhaa kwa kutoa risiti za vat.

Ma huyu kapigwa faini kwa uzembe wake maana haiingii akilini ununue mzigo wenye kodi ya vat alafu wewe uwe mvivu wa kutoa risiti, ni kama vile unajipiga risasi mguuni.

Kimbembe kipo kwa wanaonunua mizigo isiyo na risiti za tra, hii mara nyingi ni kwa wale wanaouza magendo yaliyoingizwa nchini bila vibali, Yani hapa utayaita maji Mma!!
Kuna muda hata wateja wenyewe hawataki risiti kwa madai ya kwamba kodi zao zatumika vibaya
 
Ujio wa TRA kuwepo Benki umekaribia .mtafurahi na rohoo zenu.
sasa wauza madawa,matapeli,mnaouziana magari,nyumba na n.k wekeni pesa zenu ndani [emoji1787].
Wakiendelea na mchezo wa kugusa account za watu bank itakuwa ni sawa na kugusa papasi za konokono.

Haraka sana wenye pesa zao watazihamishia wanakojua, jambo ambalo litakuwa ni hatari sana kwa uchumi wa nchi. Rejea tozo kwenye miamala si simu.
 
Niwaambie TU wanajf
Hamna mfanyabiashara anapenda kukwepa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake

Tatizo Ni

1. mfumo wetu wa Kodi umekaa kinyonyaji sana, anaetunga sheria na kanuni za Kodi ni mwanasiasa bill kumhusisha mfanyabiashara na hayajui mazingira halisi ya biashara.

Ukiifuata sheria ya Kodi inavotaka unafilisika mchana kweupe na hakuna anaekuonea huruma, kiukweli Kodi zetu sio rafiki kwa mfanyabiashara yeyote mzalendo.

2. Matumizi ya Kodi,
Inaumiza Sana unalipa Kodi kizalendo afu unaskia Kodi yako uliolipa Kuna wahuni wanafuja fuja TU kwa maslahi Yao binafsi Tena kwa majigambo lukuki wakiitana majina wanayojua wao kana kwamba sisi wengine hatuna akili wametupa limbwata.Inaumiza sana na kuvunja Moyo.
Afu kibaya zaidi kuna watu kibao wanakula hela za umma lakini mpaka sasa hatujasikia aliewajibishwa,hakika huwez pata nguvu za kulipa kodi
 
Mkuu,
Hiyo risiti yenye VAT unayoiongelea 18% unajua ikipigwa kwa kila bidhaa unafiliska haraka?

Hivi unajua mfuko mmoja wa simenti au nondo kuna faida ya sh. Ngapi?

afu utoe risiti ya efd na serikali ikate kodi Yake pamoja na vat 18% [emoji848]

Hivi haya unayoshabikia unafanya biashara au uliwahi KUFANYA biashara kweli?[emoji848]
Hawajui ABC za biashara wengi ni waajiriwa
 
Wafanyabiashara wengi wanakwepa kodi huo ndiyo ukweli...Hata Dainamo yumo kwenye huo mkumbo.
 
Ujio wa TRA kuwepo Benki umekaribia .mtafurahi na rohoo zenu.
sasa wauza madawa,matapeli,mnaouziana magari,nyumba na n.k wekeni pesa zenu ndani [emoji1787].
hapo pagumu hatari maana wengine tunauza mpaka gari 3 kwa siku na hatulipi sh 10 sku wakifukunyua na kukuta zipo m kadhaa bank wanapita nazo zote kama upepo ukipambana wanakula kodi 20% na fine juu nchi ngumu hii[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
hapo pagumu hatari maana wengine tunauza mpaka gari 3 kwa siku na hatulipi sh 10 sku wakifukunyua na kukuta zipo m kadhaa bank wanapita nazo zote kama upepo ukipambana wanakula kodi 20% na fine juu nchi ngumu hii[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Kimsingi kila malipo yanatakiwa yalipiwe na kodi, huo ndio ukweli lazima tuwe na utamaduni wa kulipa kodi wenyewe sio hadi mkimbizane na TRA hapana sema watanzania ni wakwepa kodi in nature bila kufahamu ile kodi ndio maendeleo ya nchi yetu
 
Ujio wa TRA kuwepo Benki umekaribia .mtafurahi na rohoo zenu.
sasa wauza madawa,matapeli,mnaouziana magari,nyumba na n.k wekeni pesa zenu ndani [emoji1787].
Kibaka akikuvamia utalia na polisi ambao kodi yako ingesaidia kuboresha utendaji kazi wao (vitendea kazi)

Nyumba ikiungua utalia na zimamoto ambao umewazurumu kwa kukwepa kulipa kodi ambayo ingesaidia sana ktk kuokoa nyumba, uhai, mali na pesa zako huko ndani
 
Kimsingi kila malipo yanatakiwa yalipiwe na kodi, huo ndio ukweli lazima tuwe na utamaduni wa kulipa kodi wenyewe sio hadi mkimbizane na TRA hapana sema watanzania ni wakwepa kodi in nature bila kufahamu ile kodi ndio maendeleo ya nchi yetu
kwaiyo nikiuza gari yangu natakiwa kulipa kodi?
 
ILA WATANZANIA JAMANII KWA NINI TUNA HULKA YA KUKWEPA KODI SANA,!! HATA KAMA CHANZO NI MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI ILA TUMEZIDI BANA.
Usipokwepa kodi faida unatoa wp ww!!??
ulishawahi kufanya biashara ww!!??
 
Kimsingi kila malipo yanatakiwa yalipiwe na kodi, huo ndio ukweli lazima tuwe na utamaduni wa kulipa kodi wenyewe sio hadi mkimbizane na TRA hapana sema watanzania ni wakwepa kodi in nature bila kufahamu ile kodi ndio maendeleo ya nchi yetu
Unaijua viete,unaijua viete wewe ?
Mtu anajigamba kwa dharau wakati hiyo v8 kodi yangu imetumika kuinunua.
Utapata wapi moyo wa kulipa Kodi kikamilifu?
 
Back
Top Bottom