TRA wanatumia migambo kama 10 kwenye kafrem kadogo

TRA wanatumia migambo kama 10 kwenye kafrem kadogo

Idadi ya migambo wakati wa kukusanya kodi siyo kigezo cha uhalali wa ulipaji au ukwepaji kodi.
Wakija migambo 1000 kama umelipa kila unasho paswa kulipa hautaona shida yoyote ya uwingi wa migambo.
Suala la msingi la kujadili ni makadirio ya kodi yanakuwa na uhalisia au yana umiza tu wafanyabiashra?
Suala la pili kodi ikikusanywa inatumikaje?

Tulipe kodi tusitafute huruma za wananchi tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu kama walipa kodi.
Titi nikikueleza kilichojiri nafikiri ungeshika tama...
Kwa kweli ndo nimemalizana nao jion hii ila uwii bora ukutane na panya road sio tra
 
Acha waupige mwingi na chief au daktari maana mwendazake yeye pekee na TRA yake walikuwa makatili siyo friendly kwa wafanya bia na shara.
Ile hotuba flani amazing ya kuwa kuna na kuwapulizia mgongoni wafanya bia na shara walipe kodi kwa matakwa yao bila shuruti au kuharakaishwa tunao ona mbali tulijua ni furahisha genge kutafuta umaarufu (popularity) uhalisia hakuna mtu au mfanya bia na shara anapenda kulipa kodi /ushuru/tozo kwa hiyari akiwa na furaha.

Muda ndiyo jibu mtaelewa tu mwamba JIWE alikuwa sahihi na mzalendo hasa.
Hivi nani anapenda kodi ikusanywe kikatili kisha waitumbue mafisadi watu wachache huku hakuna maji, umeme, bei za mafuta na vyakula juu?
AU ikusanywe kibabe lakini irudi kuwajengea wananchi wote barabara, miundombinu ya umeme, masoko, miundombinu ya maji na huduma za faya na elimu kwa wote?
Demokrasia ni illusion kwa ajili ya delusional people kwa manufaa ya wanaojidai ni watetezi wa demokrasia.
Aisee hawa watu ni laaana.
Yaaani hawataki hata kukuelewesha wala kukusikiliza kwa chocote.
Nafanya biashara manispaa siwez acha kulipa leseni...huo udambwi mwingine wa mashine na makadirio na ujinga mwingi jamani..hilusikilizwiiii hata kidogo ni msobe msobe mpaka sero lao hapo temeke
 
Back
Top Bottom