TRA ya USA waruhusiwa kuua ikibidi kukusanya kodi ya Serikali


Kwani nimeandikaje? Nimeandika TRA wa USA wanaruhusiwa kuua ikibidi kwenye kukusanya kodi ya Serikali, sasa kipi ni kigumu hapo kuelewa?
 
hapa Tanzania inafaa kutumia njia kama hiyo, maaana huku watukutu ni wengi sana, mabingwa wa kulalamika wanataka barabara nzuri, afya , maji lkn watata kulipa kodi.
 
Mmoja katuwekea tozo juu ya tozo juu ya tozo kwenye pesa ambazo tumezipokea baada ya kodi.
 
Kwani nimeandikaje? Nimeandika TRA wa USA wanaruhusiwa kuua ikibidi kwenye kukusanya kodi ya Serikali, sasa kipi ni kigumu hapo kuelewa?
Kwani kuua hapo ni ajabu?

Wauza madawa na majambazi watadeal nao vipi bila kuwapoteza?
 
Demokrasia inaishia kwenye kodi ya Serikali hapo hakuna mchezo na ndiyo maana wanaruhusiwa kushoot na hata kuuwa linapokuja swala la kodi, …

Lakini kodi zao hazichezewi kama hizi za kwetu
 
Hakuna TRA Marekani,tafuta jina la Revenue Authority ya Marekani ndipo uandike.
Huwa mnawahi kuandika posti bila kujipanga.
 

Leta link ya tangazo zima la hiyo kazi; acha kuleta vipande vipande hapa kwa nia ya kupotosha watu!

Unlike Tanzania (ambayo ina police force moja tu), Marekani ina police wa aina nyingi (decentralized law enforcement system). Kila agency ina law enforcement unit yake. Sasa sijui wewe unataka police wa IRS wasitekeleze majukumu ya kipolisi? Yaani wawe na duties zinazofanana na za tax audit personnel?
 
Kumjazia mnyonge matozo kila sehemu, kumsababishia gharama kubwa ya kuishi hadi mlo kwake kuonekana kitu cha anasa, hiyo ni kiwango cha juu cha mauaji ya halaiki na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Leo hii unapangiwa hadi kuumwa isizidi mara tatu ili utibiwe nhif, wakati huduma unalipia.
 
Juzi hapa kashindwa kulipa 23%. Ikabaki story tu
 
Bila kusahau kuwa ndani ya hiyo tr 1.8 kuna tozo hadi kero.
 
"To use deadly force,if necessary"hii haimaniishi kuua,hii idara ni zaidi ya idsra ya mapato,hawa wanabeba siraha,TRA bongo sio polisi Wala hawana mafunzo ya kutumia siraha kama takes la kazi,
Be willing to arrests,execution of warrants,Hili ni takwa kama la takukuru,sio TRA,
Hawa kazi yao sio kukusanya mapato,kazi yao ni kuzuia magendo,utakatishaji pesa,wanafanya kazi kama polisi,kwa hapa bongo ni Sawa na kikosi Cha KMKM,kikosi maalum Cha kuzuia magendo,kule Zenj,na kule Zenj idara ya mapato ni ZRB,ZRB hawabebi siraha,Wala hawaenendi kama idara ya polisi,ni civilian entity,kwenye majukumu yao huwa na polisi,lakini KMKM Hawa Wana vaaa combat Wana mafunzo ya kijeshi,Wana zuia magendo na pesa haramu,Sawa sawa na IRS,
IRS sio idsra ya mapato,kwa sababu ni law enforcement entity,Wana haki ya kubeba siraha,na kukamata kipolisi,Hawa ni Sawa na KMKM sio kama ZRB,Zanzibar revenue bureau,au TRA ya bara.
 
Acha ujinga tofautisha idara ya mapato na vikosi vya kuzuia magendo,fedha haramu,
Zenj Kuna KMKM na ZRB,KMKM huzuia fedha haramu na magendo Hawa Wana mafunzo ya kijeshi,huendesha operation zao kama polisi to law enforcement agency,ZRB ndio hukusanya mapato kama ilivyo TRA Bara.
Kutumia "deadly force",haimaanishi kill or murder,hii ni kutumia nguvu za ziada zenye kuweza kuleta madhara pale inapobidi ktk kuzuia magendo na fedha haramu kuingizwa kwenye uchumi.
"Execution"hapa imetumika kumaniisha kutekeleza,sio kuua,
 


Nchi inajengwa kiharamia??!!, kweli Wahenga walisema; "Usione utajiri wa mtu ukautamani kwani huwezijua undani wake".

Amerika licha ya kujidai kwamba inalinda haki na demokrasia za watu na Raia lakini wakati fulani inashindwa kufuata njia za kimahakama kuwahukumu watu wake bali inawakung'uta risasi Kwa ajili ya utajiri !!, utajiri unayo thamani kubwa kuliko utu!!!--- yawezekana ni katika muktadha huo huo ndivyo alivyofanyiwa George Floyd na ni katika muktadha huo huo Amerika wamekuwa wakivamia nchi mbalimbali na kuua raia kwa kisingizio cha kuleta Demokrasia kumbe ni kwa ajili kupora mali kwa njia ya; "kukusanya kodi/mapato popote hata ikibidi kuua", The USA is a satanic bloody hands rich country.
 
Asante kwa kutujulisha wananchi,unatulitea data, kiutalaam,wewe utakuwa ni msomi wa hali ya juu.
 
Kwa uchumi wa Tanzania,,TRA INGEKUWA INAKUSANY TRILLION 30..WANJISIFIA KWA KUJIWEKEA TARGET KIDOGO
 
Mnyonge gani ambae anakuwa na account bank? Pili kwenye miamala ya simu tozo ni 42% tuu..

Jingine mapato ya mnyonge wako yameongezeka mara dufu kufuatia kuongeka Kwa bei ya Mazao ambayo mliharibu..

Kamuulize leo mnyonge WA kijijini kwamba anataka kipi Bei ya Mazao iwe mbaya au iwe juu atakujibu.

Kwenye kilimo Cha mnyonge kafuta tozo 52 na katoa ruzuku juu..Wewe si unajua kusoma haya niambie hapa chini pameandikwajeπŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20220812-133429.png
    237.6 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…