TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.

Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.

“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.

“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.

TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
 
IMG_5473.jpg

Nimeiona mahali nimeshangaa
 
Hivi mtu anaposema bei halisi ana maana gani? Hizo bei za awali hazikuwa halisi? Bora angesema thamani ya shilingi au kupanda kwa bei ya magari hayo. Na kama hakuna badiliko then kwanini kodi iongezeke?

Ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa katiba kupandisha kodi bila idhini ya bunge. Badiliko la kodi ni lazima liidhinishwe na bunge
 
Hii kama ni kwel ina hatar sana, hyo vanguard 2013 kutoka 11M mpaka 31M

Kuna watu weshamuona jamaa mbwiga hivyo wanafanya makusudi ili kukomoa. Na yeye alivyo kweli mbwiga wala hana habari ata kuuliza tu. [emoji3][emoji3][emoji3] Mimi ata baiskeli sina hivyo poa tu. Wao waweke ata iwe milioni 20 kodi ya raum old model
 
Back
Top Bottom