TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

We ndo punda kabisaaa maana vanguard ya mwaka huo ni kama mtangulizi alivyosema wewe hata hujaingia kwenye website unaleta ujinga
Uongo huo ingia kwenye website ya TRA uweke chassis number ya gari yako hiyo Vanguard uone kodi unayotakiwa kulipa acha uongo au hata gari huna!!
 
Nini kinatokea kwamba taifa linategemea kodi hii sana kuliko vyanzo vingine vya mapato
si wanajua wabongo wanapenda sana magari kwa gharama yeyote, so wame capitalize kwenye huo udhaifu wetu.
 
Tuwakomalie wabunge wabadilishe hizi kodi za enzi za ujamaa kwenye magari. Japo unasema unalinda mazingira lakini kodi kubwa hivyo kwenye mtumba una viwanda vya magari?
Gari ni kitu kinachosaidia kukuza uchumi. Ingekuwa ni amri yangu ningeweka kodi karibu na sifuri. Kwenye magari ya kazi kama pickup na fuso watu wangenunua bila ushuru hata mia, ikiwezekana nawapa na hela ya asante😀😀

Kulalamika haya mambo haitusaidii kitu. Inabidi wabunge, wanasheria nk walifanyie kazi.
Usisahau bunge pia ni la kwao
 
Jamani ... Toyota Harrier 2006 kodi imeongezeka kwa kiasi gani ????
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.

Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.

“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.

“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.

TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
Serikali ya wanyonge.
 
Back
Top Bottom