secret file
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 5,843
- 8,637
Itakuwa ni kokoto tu hapo,Nini kimesababisha hyo Vanguard 2013 kutoka Kodi ya million 11 hadi million 31
mi5tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itakuwa ni kokoto tu hapo,Nini kimesababisha hyo Vanguard 2013 kutoka Kodi ya million 11 hadi million 31
Bongo pagumu sana....Kuna gari moja Zimbabwe jumla kodi waliikata kama one milion of TZS ila huku bongo gari ile kodi kwa wakati huo walikuwa wanachukua kama milioni 10 hivi.
Nenda hizi c center za be forward Japan au SBT kafanye utafiti juu ya hili
Achana naye mtu kama magu2016 hata haelewi TRA ni dude gani ndio atajua kikokotoo cha magari. TRA kwa sasa inatoza kodi in Advance mpaka kwenye nyumba za watanzania wanyongeUmeona kipeperushi kilichokua kinasambaa??? Ambacho watu "wanadai" ndo bei zilizobadilishwa?(kodi)
Tuanzie hapo. Halafu kielezee kwa hayo maelezo yake
Hiyo mbona ndio kodi yake siku zote? Au zamani ilikuaje?Nimeangalia bforward ist ya 2002 ya milioni 5.1 na visenti vyake mpaka dsm bandarini ushuru wake ni milioni 5.6 na visenti nyake. Kweli kagiza gari kwa sasa ni anasa.
Samahani wewe ni afisa tra temeke au pale bandarani?Kama hujaelewa ufafanuzi huo wa TRA basi wewe ni utopolo tu mkuu!
Wabunge wenyewe wako wapi?Tuwakomalie wabunge wabadilishe hizi kodi za enzi za ujamaa kwenye magari. Japo unasema unalinda mazingira lakini kodi kubwa hivyo kwenye mtumba una viwanda vya magari?
Gari ni kitu kinachosaidia kukuza uchumi. Ingekuwa ni amri yangu ningeweka kodi karibu na sifuri. Kwenye magari ya kazi kama pickup na fuso watu wangenunua bila ushuru hata mia, ikiwezekana nawapa na hela ya asante[emoji3][emoji3]
Kulalamika haya mambo haitusaidii kitu. Inabidi wabunge, wanasheria nk walifanyie kazi.
Wakina Gwajima na babu taleWabunge wenyewe wako wapi?
Na kwa nini siku zote watu hawakulalamika? Kwani huo mchakato haukuwepo?Hivi mtu anaposema bei halisi ana maana gani? Hizo bei za awali hazikuwa halisi? Bora angesema thamani ya shilingi au kupanda kwa bei ya magari hayo. Na kama hakuna badiliko then kwanini kodi iongezeke?
Ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa katiba kupandisha kodi bila idhini ya bunge. Badiliko la kodi ni lazima liidhinishwe na bunge
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.
Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.
“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.
“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.
Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.
TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
This is not Africa but TANZANIA.This is africa where having a car you may be counted as a rich man,and not mean of aiding helping social life to poor human being development