pandagichiza
JF-Expert Member
- Jul 9, 2013
- 5,248
- 3,663
Vanguard ya 2013 ina umri wa miaka 8 kodi imepanda kutoka million 11 hadi 31 millionHujaelewa nini mkuu tukueleweshe?
Hebu fafanua hiyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vanguard ya 2013 ina umri wa miaka 8 kodi imepanda kutoka million 11 hadi 31 millionHujaelewa nini mkuu tukueleweshe?
Hakuna wabunge wanaoweza kufanya hivyoTuwakomalie wabunge wabadilishe hizi kodi za enzi za ujamaa kwenye magari. Japo unasema unalinda mazingira lakini kodi kubwa hivyo kwenye mtumba una viwanda vya magari?
Gari ni kitu kinachosaidia kukuza uchumi. Ingekuwa ni amri yangu ningeweka kodi karibu na sifuri. Kwenye magari ya kazi kama pickup na fuso watu wangenunua bila ushuru hata mia, ikiwezekana nawapa na hela ya asante😀😀
Kulalamika haya mambo haitusaidii kitu. Inabidi wabunge, wanasheria nk walifanyie kazi.
Yan mm nimetoka kuagiza gari mwez uliopita...mpk kufika bansarini ilikuwa 5.4 milionNimeangalia bforward ist ya 2002 ya milioni 5.1 na visenti vyake mpaka dsm bandarini ushuru wake ni milioni 5.6 na visenti nyake. Kweli kagiza gari kwa sasa ni anasa.
Umimi na ubinafsi ndio shida gari au transport ni kilainishi cha maendeleo na si fahari tushushe shuru tuvune zaidi kwenye madini yetu tukivuna tu chuma chetu vizuri cha liganga ukawa ni mgodi wa serekali tukaomba tu teknolojia ya uimarishaji chuma kutoka kwa wachina tanzania itakuwa ya kipekee afrika na duniani #Tusiwape wageni kila kitu, huu uwe ni mgodi wa taifa letu. [SIONI UBAYA HATA TUKAUZA NDEGE 2 TUKAINGIZA PESA KWENYE MGODI WETU] National iron miningsThis is not Africa but TANZANIA.
Ukienda Zambia hapo Kuna Gari zinatozwa Kodi milion 2 ila bongo gari Hilo Hilo Kodi Yake ni milion 12
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.
Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.
Taarifa ya TRA iliyotolewa katika gazeti la Mwananchi leo Ijumaa Januari 8 imekuongezeka kwa ushuru wa baadhi ya magari kuanzia Januari mwaka huu kutokana na uthaminishaji uliozingatia bei halisi za magari hayo, huku pia magari mengine yakishuka bei.
“Kimsingi ongezeko hilo limetokana na bei halisi ya magari husika na hivyo haimaaishi kwamba TRA imeongeza ushuru wa magari,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
TRA imesema kuwa magari yaliyotumika hutozwa ushuru wa bidhaa kutokana na umri wa gari ambapo umri wa gari huhesabiwa kwa kufuata mwaka wakalenda.
Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa maika minane hadi tisa pamoja na kodi nyingine hutozwa ushuru huo wa bidhaa kwa asilimia 15 na gari yeye umri zaidi ya huo hutozwa kwa asilimia 30.
“Hivyo ikiwa mwagizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa ikiwa gari yake ingewasili kabla ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.
Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waigizaji wa magari yenye umri huo waliagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezaka hivyo wakasema hakuna kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye magari.
TRA imesema katika taarifa hiyo kuwa uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la sheria hiyo.
Bongo kwenye vyanzo vingi vya mapato bado tunaminyana kwenye kodi za used vehicles. Huku ni kukosa ubunifuBongo pagumu sana....
ukienda Botswana,South Africa,Lethoto, Swaziland.....
vijana wanaendesha magari mazuri sana ya kisasa....ie BMW,Benz Jaguar etc....
lkn ukija bongo vijana wengi wanaendesha gari za ajabu ajabu.....Toyota IST,duet....carina,rav 4 Vanguad Noma sana!!
Uenda Kuna ex mchepuko wa mkadiaria Kodi kaagiza hyo vanguard Ila mkadiaria Kodi Hana uhakika n ya mwaka gani hvyo anataka kumkomoa tuu mtu wake waliomwagana.View attachment 1671963
Nimeiona mahali nimeshangaa
Ndo ufafanuzi wa taarifa zinazozagaa kuwa wameongeza ushuru???Amesema kama uliagiza 2020 lakini gari imefika 2021 basi hapo ushuru unabadirika kutokana miaka toka itengenezwe hiyo gari imeongezeka
duhNa vile mi ndio nilimshawishi ye alitaka kwenda yadi, nitawaambia nini watu, ngoja niangalie kokokotoo tena
Hiii ?Ndo ufafanuzi wa taarifa zinazozagaa kuwa wameongeza ushuru???
Nimekuuliza umeona hiyo taarifa inayozagaa yenyewe?? Ungekua umeiona ungenielezea vizuri kwamba gari ya 2013 ina Kofi ya uchakavu sh ngap mwaka 2020(December) na imeongezekaje kuwa hiyo mpya 2021(January)
Na kodi ya uchakavu ni kwa gari za miaka kumi au zaidi.
Ningeposti hilo jedwali sema nashindwa kuambatanisha picha kwa simu yangu hapa
Hapo ndo ungeona kaongea vitu visivyoeleweka/visivyohusiana na huo ufafanuzi wake
Kuna mshikaji wangu kaagiza rav 4 kako kwenye meli huko aliko kama amepata taarifa hii, sijui itakuwaje.
kwa chanzoo kweli ni magumashi ila ndio ziko ivoo ata ukiingia kwenye system ipo ivooHii ni ya uongo angalia hapo chini Chanzo chake! Unadanganywa na wewe unakubali kweli?
Umesoma au umebaka nilichoandika? Rudia.... Nimeandika hivi "hiii?"Hii ni ya uongo angalia hapo chini Chanzo chake! Unadanganywa na wewe unakubali kweli?
Hii ni ya uongo angalia hapo chini Chanzo chake! Unadanganywa na wewe unakubali kweli?
Uongo huo ingia kwenye website ya TRA uweke chassis number ya gari yako hiyo Vanguard uone kodi unayotakiwa kulipa acha uongo au hata gari huna!!