TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Amesema sheria inatuhusu kushikilia akaunti ya mtu kama njia zote za majadiliano zimeshindikana,, halafu anasema wameamua kuzifungulia akaunti hizo ili wawe wanakaa mezani kujadiliana... Sijaelewa., Je hiyo sheria inayowapa nguvu ya kushikilia akaunti imeondolewa ama ni maneno matupu?
 
Mfanyabiashara akiamua kuwa mkeli akilipa ushuru tozo, lesesni , nssf,na Kodi zote,unazozijua Kama:-
1.Income tax
2.Witholding tax
3. Vat
4.payee
5...
6....

Ukijumlisha zote Ni around 75% ya mapato yote ukitoa gharama za uendeshaji
Faida inaweza kuwa 5% sometimes negative(loss)

Huyu mfanyabiashara hawezi kukua kibiashara,
Anaifanyia kazi selikali tu.

Nadhani tutumie wataalamu wa Kodi tukokotoe, Kodi,tozo, lesseni vyote visizidi 30% ya mapato

Good thing mapato ya makampuni yanatumwa tra kila siku
 
Hii itafanya Kodi ziwe rafika zinazolipika kwa hiari na kuondoa udanganyifu, pia itakuza biashara na mitano zaidi
 
Account zimefungwa makusanyo ya Kodi yataongezeka vipi?

Mataga akili zenu mmezizika chato na mwendazake
 
Safi sana Mama. Sasa hivi kila mtanzania ni kazi na bata na mapesaaa ya kutosha mtaani mpaka msemo wa laki si pesa milioni ni ya bia mbili tu urudi.

Wakati wa madanga kurudi kuishi masaki na kuendesha ma range rovers umewadia sasa, kweli mama Ni kama, Piga kelele kwa mama ake... bado nawaza huu msiba mzito nalia kwa style gan , ya kulala, kutembea au kukumbia
 

Huyu mama ananiudhi sana Jaman , Sijui huwa anawaza njnj , yanj ananikera hatari
 
Huyu mama ananiudhi sana Jaman , Sijui huwa anawaza njnj , yanj ananikera hatari
Msamehe anajaribu kutatua malalamiko ambayo yalikuwa baseless nia yake ni njema, tatizo ni kwamba hayo mambo anayodhani anatatua ndio sababu za kugota kwa maendeleo in the first place.
 
Ngoja nikupe mfano mwepesi ya list ya tozo zilizopo kwenye income tax kama wewe umeajiriwa baadhi ya nchi EU, halafu unakabiashara kako pembeni, una saving accounts, umewekeza kwenye kampuni unapata dividend, unakaa nyumba ya serikali/kampuni, unatumia gari la serikali/kampuni, umefanya vizuri kazini umelipwa bonus.

Kwanza utapigiwa hesabu ya thamani gari unalotumia kama vile bado mpya: utatakiwa kulipa 18% kodi ambayo ni thamani ya hilo gari kwa mwaka kutoka mfukoni kwako.

Nyumba kama thamani yake ni 100m wanaweza toa 30m, hiyo 70million utalipa 2.25% kodi kutoka mfukoni kwako.

Umekopeshwa kama vile wabunge wa Tanzania labda 150m mkopo auna riba utatakiwa kulipa 2.25% ya hiyo hela kama kodi kila mwaka.

Mafuta kuna annual ya allowance kama unawekewa zaidi ya 5m kwa mwaka utaambia ulipe kodi labda 2m

Posho unayopokea unalipa kodi

Na mazazaga mengine ya ‘benefit in kinds’ unayopata.

Hizo tozo zote zinajumlishwa kwenye mshahara wako baada ya kulipa PAYE, wana jumlisha na faida yako ya biashara baada ya VAT, saving interest za bank ulizopata ndani ya mwaka na dividend received kwenye share za biashara. Hapo utatolewa personal allowance.

Halafu ndio mziki wako wa kodi unaanza, sasa inategemea upo kundi gani kutokana income zako zote kuna makundi matatu; sikia tu wale wenye income kubwa mziki wake kwenye income tax. Baada ya kulipa hapo kinachofuata ni National Insurance contribution payments.

Hayo ya pension utalipa kama wengine (if anything wataita allowable expenditures) yaani nyie vikodi vya VAT mnalalamika kweli. Kodi huko kwa wenzetu ni balaa hasa kwa matajiri.
 
Wakati wa madanga kurudi kuishi masaki na kuendesha ma range rovers umewadia sasa, kweli mama Ni kama, Piga kelele kwa mama ake... bado nawaza huu msiba mzito nalia kwa style gan , ya kulala, kutembea au kukumbia
Safi kabisa tulibanwa mpaka tukapunguza kuhonga.
 

Hakuna mtu anayependa kuzaliwa bila kumjua baba/Mama yake, kama ulipata hiyo privilege mshukuru Mungu
 
Kuna watu walipeleka nguzo kwenye kiwanda cha kuchakata nguzo Iringa na Mafinga, inasadikika fedha zao zilizuiwa kwa amri kutoka juu, sijui inahusiana na haya yanayosemwa hapa?
 
Shetani Magu alikuwa kiumbe hatari sana. Tuanze kudili na mitoto yake. Mimi naanza na yale mawili yenye vitambi.
Jifunze kusamehe na kusahau Mkuu, yawezekana hakujua alitendalo
 
Hapo sawa kabisa
Ila walipe madeni yao sababu dawa ya deni ni kulipa,haiingii akilini mtumishi anayelipwa kiduchu akamuliwe lkn mfanyabiashara mkubwa anakwepa Kodi hii haikubaliki.kwa nchi za wenzetu wakwepa Kodi huwa wanapigwa risasi hadharani ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…