TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

TRA sasa wanavunja sheria; mkwepaji wa kodi anapaswa kupata staili yake
hujui kilichokua kinatokea kuna kampuni X ilikuwa haina kesi na TRA bali TRA ilikua inamdai mtu A yule A akasema na shindwa kulipa kwa sababu naidai kampuni X,maafisa wa TRA kwa kurely na maneno ya A wakaenda moja kwa moja Benki na kukwapua not less than 400m bila hata kuwa na nakala yoyote ya uthibitisho wa madai ya A kwa kampuni X au uwepo wa hukumu ya mahakama iliyokuwa imethibitisha madai ya A dhidi ya kampuni X.Benki nao wakajichanganya kwa ama kwa kua mamluki au hofu wakala ruhusu fedha za X kutolewa bila idhini ya Kampuni X as today Benki walisha mpoteza mteja wao Kampuni X aliyekuwa na deposit kubwa kabisa.

400
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi

Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.

"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo

Chanzo: NIPASHE
Wawarudishie na fedha yao ili wakae waelewane.
 
Truth be told, mazoea mabaya ya muda mrefu yamewafanya wafanyabiashara wengi wawe na kasumba ya kutoridhia kutii sheria bila shurti --- lugha ya kutoa kodi kwa hiari hawaielewi kamwe.

Wamejifunza njia ya mikato, ujanjaujanja, wiziwizi, rushwarushwa, dilidili and the like. Sasa wakiletwa kwenye mstari, by definition, wao wanadhani wanaonewa. What!???
Mshkaji unataka kushindana na Rais?hautaweza na unajisumbua na aliyekutuma kutwa kumsema vibaya President Samia
 
Data za uchumi huwezi kuzipika. Zinakusanywa na IMF na ndiyo waliotuingiza kwenye nchi za uchumi wa kati. Muda utaongea kama tutaendelea kuwemo kwenye hizo nchi za uchumi wa kati au tutarudishwa tulikotoka. Kuwa na subira. Ninawajua sana watanzania aka wabongo; hawawezi kupata maendeleo bila kuwarusharusha kichura. Ukiwachekea chekea tu utavuna mabuwa.
Unachekesha we Mjinga unasema Data zilikuwa hazipikwi?Are you serious?
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi

Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.

"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo

Chanzo: NIPASHE
Ya kwangu mbona bado?
 
Unachekesha we Mjinga unasema Data zilikuwa hazipikwi?Are you serious?
Hajui kuwa mwezi wa pili tuliambiwa uchumi unakuwa kwa 7% ila msemakweli akatuambia mwezi wa nne kuwa uchumi umeshuka mpaka % Anadhani uchumi nao ulizikwa?
 
Muda utaongea. Kama staili hii ya kukusanya kodi kwa wabongo kwa kubembelezana inatufaa au haitufai, namba zitatuambia. Kama makusanyo ya kodi ya TRA kwa mwezi yatabaki tarakimu hizo hizo au kupanda angalao kidogo, basi utaratibu huu ni mzuri na wa kupongezwa. Kama makusanyo ya kodi kwa mwezi yataporomoka, basi utaratibu huu wa kujadiliana na kubembelezana kwa wabongo hautufai na itabidi utaratibu wa awali urejeshwe. Lakini ninavyowajua wabongo mhhhh, ngoja tusubiri na wala tusije tukasingizia corona!
Toka TRA inaanzishwa 1996 trend ya ukusanya mapato ilikuwa nzuri tu. Ilianza na 25b/= kwa mwezi hadi 800b/= kwa mwezi mwaka 2016. Msingi ya ukusanyaji ulijikita kwenye dhana ya " voluntary compliance". TRA walianzisha mpango huu ili kuwa user friendly kwa walipa kodi.

Sheria ya kuanzishwa kwa TRA kunaipa mamlaka kukusanya kodi za aina 11 au 12 tu lakini mabadiliko makubwa sana yakafanyika mwaka 2016 kwamba TRA pamoja na kodi hizo 11 ikusanye pia kodi na tozo zote in a unified system pia mtindo wa voluntary compliance ukaachwa , badala yale zikaundwa task force. Mwanzoni ilionekana mapato yanaongezeka kitakwimu, lakini ukianza kugawa hapo mapato kulingana na mchango wa kila taasisi, unapata picha tofauti.

Madhara makubwa ya mfumo huu ikawa ni kufungwa au kudorora kwa biashara nyingi kulikoelekea kupungua lwa makusanyo. Hivyo dhana yakusema watu hawapendi kulipa kodi si sahihi. Suluhisho ni kuweka mfumo sahihi na wa uwazi wa kulipa kodi na utapata matokeo chanya.
 
Hata mm Leo hi nimeshanga sna nilikuwa cjafanyiwa assessment ya mwaka huu nilijisahau kbsa juz wakaanza kukamata magari bas nikafanya jitiada za kufika ofc zao kuomba utaratibu wa kulipa nikabiwa niandike barua ya kueleza sababu zilizofanya kuchelewwa kulipa Kodi na kukadiriwaa bas nikafanya nikaandika barua ya kueleza kuwa nilikuwa naumwa sana na kuuguza Sanaa hvyo nikashindwa kufika ofisini bas wakakubali naleo nikaambiwa nilipe kiasi alfu penalt nikafutiwaa hvyo nikaambiwa nilipieee Kia's nilichonacho kuendelea na utaratibu wakt awali walinimbia napazwaa kulipa 250000 pmj na fineee. Kweli kwa leo hi nimewasifu Hawa vijana watoza ushuru wamekuwa waelewa Sanaa ..nikalipaa pale pale.

Nimefurahi mnk ingekuta kipind Cha meko uwez futiwa fine Tena kwa system za tra. Nilishangaa snaa cjatoa hat ongo yoyote

Mkuu weka hata koma na nukta basi, au ni hiyo kutopigwa penalt umefurahi mpaka hujali kuweka tena herufi kubwa na ndogo?
 
View attachment 1793042

Huo ndio utaratibu duniani njia za kistaarabu muda wakekukimalish kinachofuata watu wanavamia account yako wanakomba, halafu ndio mnaenda mahakamani kama unadhani umeonewa..

Kuna wanafanya kazi wachache TRA ni shida kwa kutumia sheria vibaya kujinufaisha, ila tatizo kubwa zaidi kwenye kodi Tanzania ni uelewa mdogo wa wafanyabiashara kwenye sheria na taratibu za kodi.

Anyway kwa utaratibu huu wa kubembelezana hakuna miradi itakayo kamilika ontime, something will have to give kati ya debt obligations, government running cost au miradi.

Sio ngumu kuelewa miradi ndio itakayo simamishwa, TANESCO washaanza na usambazaji wa umeme wakati hela za REA ni mkopo sasa sijui shida ipo wapi.

Hawa wabunge wetu na wafanyakazi wenye posho and other ‘benefits in kind’ mfano anaishi nyumba ya serikali, gari la serikali anawekewa mafuta, wanapata mikopo yenye interest nafuu kama sio bure na marupurupu mengine; watu kama hawa nchi za wenzetu wanatakiwa kulipa income tax yote hayo.

Ninauhakika huo utaratibu wahusika wangeujua upoje halafu bunge lipendekeze kuiga huo mfumo; ndani ya bunge kungewaka moto na malalamiko ya unyonyaji.

Swala la kodi Tanzania bado sana, na haya maamuzi ni kurudi nyuma; sio kusonga mbele watu inabidi wazoee utaratibu wa kodi.

Kama alifanya uporaji wote huo kwenye account za wafanyabiashara, na bado mradi wa SGR kipande cha Dar-Moro alishindwa kukimalisha kwa wakati, utakuwa mwendawazimu kudhani alikuwa anaenda mbele. Kimsingi mapato yalikuwa yanazidi kushuka, na sio kupanda kama unavyotaka tuamini.
 
Kazi iendelee, Safi sana Mama yetu Samia Suluhu Hassan, ww hakika ni mama
 
Muda utaongea. Kama staili hii ya kukusanya kodi kwa wabongo kwa kubembelezana inatufaa au haitufai, namba zitatuambia. Kama makusanyo ya kodi ya TRA kwa mwezi yatabaki tarakimu hizo hizo au kupanda angalao kidogo, basi utaratibu huu ni mzuri na wa kupongezwa. Kama makusanyo ya kodi kwa mwezi yataporomoka, basi utaratibu huu wa kujadiliana na kubembelezana kwa wabongo hautufai na itabidi utaratibu wa awali urejeshwe. Lakini ninavyowajua wabongo mhhhh, ngoja tusubiri na wala tusije tukasingizia corona!

Kwani kipindi cha dhalimu kodi ilikuwa inapanda au alikuwa anapika data? Alichokuwa anafanya ni kupora fedha za watu na kujifanya ni makusanyo ya hali nzuri. Lile dubwasha lilikuwa liongo na katili kupita kiasi. Kama mapato ni kidogo huo ndio uhalisia.
 
Back
Top Bottom