TRA yawataka wafanyabiashara kusajili stoo za kuhifadhia bidhaa

TRA yawataka wafanyabiashara kusajili stoo za kuhifadhia bidhaa

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2018
Posts
2,005
Reaction score
19,579
Mwaka huu kazi kazi. Tukiwa kwenye majonzi ya kodi ya nyumba hasa kwa wale wanaoishi kwenye maghorofa, TRA inawataka wafanyabiashara kusajili store zenu.

1A725706-0027-4DD3-9EE7-630C4DFDF2BD.jpeg


502387E3-9624-4B36-8539-ACFFEE3A3F39.jpeg
 
Naona kuna watu watakimbia bidhaa zao soon

Wanajua mizigo inahifadhiwa sehemu nyingine
Hivi bidhaa zimeingia nchini zimelipiwa kodi sasa mimi nimeweka kwenye store inawahusu nini?

Kama kawaida yao
kwa kuwa wafanyabiashara wengi hawatoi risiti maana yake kuwa mizigo haiuziki ila wanaendelea kuagiza. siku wakianza ukaguzi wa store ndiyo watajua mauzo halisi.
 
kwa kuwa wafanyabiashara wengi hawatoi risiti maana yake kuwa mizigo haiuziki ila wanaendelea kuagiza. siku wakianza ukaguzi wa store ndiyo watajua mauzo halisi.
Na siku hiyo wengi watakufa kwa pressure maana wengi wanalipa kodi ndogo tu ya hapo dukani kumbe ana mzigo wa 150m au zaidi store, tena mbaya zaidi mkopo wa bank kaweka rehani nyumba

Kuna watu wengi wamevamia biashara
Ila naona wanaliwa timing tu

TRA wanaposema hivyo ujue wana taarifa zote za maghala yote na sehemu wanapohifadhi bidhaa zao hao wafanyabiashara

Ni kama wakati ule operation ya Magogo nchini wakati wa Magu
Wengi walikamatwa baada ya makachero kutumwa miezi kadhaa kabla ya msako na kujifanya wanunuzi wa magogo na mbao

Data zilipokamilika na kujua kila mwenye mbao au magogo ndio kazi ikaanza
Yaani walikamatwa mpaka maofisa wa misitu kibao wakawekwa ndani
 
Back
Top Bottom