TRA yawataka wafanyabiashara kusajili stoo za kuhifadhia bidhaa

TRA yawataka wafanyabiashara kusajili stoo za kuhifadhia bidhaa

Kuna watu wanauzia stoo ie wachina wa viatu
Hao ndio wakwepa kodi wakubwa

Kuna wakati nilikuwa nataka Yale magodoro magumu na mazito ya bei kubwa, nikapelekwa na dereva mmoja
Yaani lilikuwa sio duka bali gate unagonga anafungua mlinzi unaulizwa unataka nini

Ukijibu unataka Godoro anaenda kumuuliza mchina kuwa kuna mteja akijiridhisha uko poa unaingia unalipa unasepa nalo
Ila ni kama magendo tu sijui kwanini wanaiba
Mimi nilikuwa nataka moja tu kwa hiyo sikujali sana nikaondoka zangu
 
NIDA itakuja kuwa mwiba mchungu kwa wananchi, usajili wa makazi utakuwa mwiba haswaaa.

Mdogo mdogo wote tutaingia kwenye mfumo.

Walianza wa umeme kulia
 
Na wafanyakazi nao wenye ukwasi usioendana na kipato chao waangaliwe na wao sio kwa mfanyabiashara tu
Tena hao ndio wangelipa kodi kubwa zaidi
Kama analipwa mshahara mkubwa sana wangekuwa wanakatwa hata 40%
Maana bado watakuwa take home yao kubwa tu
 
ukiona mtu anafanya biashara Tanzania, na biashara yake imedumu kwa zaidi ya miaka mitano (5) ujue huyo mtu ana roho ngumu sana. Bila hivyo ndani ya miaka mitano lazma uwe chali.

Ili uweze kufanya baishara Tanzania lazima uwe kama John Wick au Rocky Balboa. Uwe na roho ya paka, na uwe na vitu vifwatavyo

1. Focus
2. Commitment
3. Sheer will
4. Perserverance

Wengi wanakuwa na number 1 na 2 na hao ndio wengi wanaishia njiani. Tanzania bila sheer will and perseverance, hufanyi biashara. Angalia watu unaopambana nao ukiwa mfanyabiashara Tanzania

1. TRA
2. Fire
3. OSHA
4. Manispaa
5. Bwana afya
6. Serikali za mitaa na madiwani
7. TMDA
8. Polisi
9. Wafanyakazi wako (muda wote wanawaza kukuibia)
10. Majirani, ndugu, na marafiki zako
11. Wafanyabiashara ambao mko sekta moja na ni majirani.
12. Majambazi na vibaka
13. Mafuriko na majanga ya moto
14. Maagano ya ancestors wako

na mengineyo mengi mno. Hapo inabidi uwe mwamba ndio utoboe!
 
Back
Top Bottom